Kama UKIMWI wa 2005 kurudi nyuma ungekuepo sasa, hali ingekua mbaya sana

Haya huwa ni matukio ya kukumbuka ushujaa na ukubwa wa M/mungu[emoji123]
 
Ukimwi wa Sasa umefubazwa na Dozi na imefika time Virus wamechoka na wao maana wamepiga kazi saana.

Ukimwi wa zamani ulikiwa Bado wenyeweJiniani ilikuwa hata miaka 5 hutoboi. Ila kwa Sasa Kuna watu Wana miaka 20 Wana moto na wako poa tu na wengine hawali hata hizo dosage.

Na research zinadevelop Hadi dawa ya HIV inaweza kupatikana kabla ya 2026.
 
Kipindi hicho ilikuw ili uanze ARV ni mpaka CD4 ziwe chini zishuke lakini baada ya kuja na mpango wa kuanza kutumia ARV as soon as u are diagnosed regardless of CD4 count...ndio mambo yalipobadilika....ukianza kutumia ARV mapema basi sio rahis kufika huko unakokusema kama hao wa zaman walivyokuwa
 
Kuna diwani alitoa maoni kipindi kile waathirika walikuwa wanalipwa kila mwezi,mwamba akasema wapangwe mstari wapigwe risasi.
 
Walikuwa wanatoka maupele mwili mzima,miguu inavimba hadi inatoa maji.Juliana ilikuwa ni balaa.
 
Dah! Ngoma ya miaka hiyo acha kabisa. Yaani ukiipata tu, kama ulikuwa unaishi mjini, unarejeshwa na ndugu zako kwenda kufia kijijini kwenu. Hatari sana.

Naona ARV's zimesaidia sana kupunguza hofu ya huu ugonjwa kwenye jamii yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…