Kama ulianza kutumia Internet mapema miaka ya 1990 na 2000 njoo hapa tukumbushane Internet Cafe tulizoenda, Vimbwanga, Kero na Kumbukumbu

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
MUHIMU: UZI HUU SIO WA KUKUMBUSHANA COMPUTER GAMES

Binafsi nilianza kwenda Internet cafe 2002, computer zilikuwa zenye visogo 😂 .



Mitanado maarufu kwa hapa bongo ilikuwa ni Marafiki.com na DarHotwire, baadae zikaja Jamboforums (kwa sasa jamiiforums), Hi5, Bongo 5,



tulikuwa tunalipia kwa muda kuanzia nusu saa, Ukilipia wanawasha program ya kuhesabu muda, iliitwa time watcher muda ukiisha inaloki computer, Wajanja walikuja na mbinu za kuruka hiki kiunzi 😂



Speed ilikuwa chini sana, kufungua ukurasa wenye picha unaweza subiri dakika nzima, ukitaka soeed nenda asubuhi sana.



Kuwa na email ilikuwa ndio ujanja wa enzi hizo, Tulichat na kutumiana barua kwa email. katika watu 100 waweza jikuta pekeyako unayo basi unapata ka feeling flani ka v.i.p, email maaarufu ilikuwa hotmail, yahoo na msn.



Enzi hizo tulitumia floppy disk kuhifadhi mafaili, ni kipindi ambacho bado cd na flash hazijawa common.



Enzi hizo websites www.-----.com ilibidi uwe uzitunze kichwani ama uwe na ki diary maalum, Sio kama sasa google imerahisisha sana



Waliokuwa hawana speed ya kutumia keyboard. walijifunza kwa kutumia program inaitwa mavis bacon


///////////////////////////////////////

Hali imebadilika, kwa sasa unaweza kuwa na smartphone au laptop yako unaingia net, Hali haikuwa hivyo kwa miaka ya nyuma kabla ya 2010s, Kipindi hicho ilikuwa ni mwendo wa cafe.

Miaka ya 2007 angalau tulianza kutumia internet kwenye simu za Nokia batani na tovuti maarufu ilikuwa waptrick lakini hizi tobuti bado zilikuwa simple sana, bado tulilazimika kwenda internet cafes kupata mambo kamili,

2010s ndio Modems za kutumia kwenye laptops na simu za kisasa zaidi zenye uwezo mkubwa wa kuperuzi internet zilipoanza kujaa sokoni ndipo wengi tukaacha kwenda internet cafe na hii ikapelekea cafes nyingi kufungwa ama kugeuzwa kuwa stationery.
 
Kulikuwa na Dar talk(something km hivi), kabla ya facebook kulikuwa na Skype.. kulikuwa na BBM MESSENGER ilikuwa kama WhatsApp vile, thanks kwa mchina kuleta hizi simu maana ilikuwa ukidownlpad hata media yenye mb 10 tu inakuandikia 36 years to complete!!😂
 
Mwaka 2009/2010 nilikuwa natumia simu kuingia facebook sasa simu nilikuwa natumia ya sista angu nilivyomrudishia simu yake nikamiss kuperuzi. Siku hiyo nikaenda internet cafe basi nikaingia zangu FB kumbe huyo mzee apita pita kuchungulia alivyoona nipo FB aisee alifoka eti mambo gani hayo ya kihuni huni watoto wa siku hizi sijui mpoje aisee nilinyanyuka nikasepa zangu kimya kimya.
 
😊Matunda Cafe Morogoro, nakumbuka back in days kulikuwa na vipazia full kuwaangalia akina Nikki Tyler, Vanessa Blue n.k life was good kwani privacy iliheshimiwa

Computer no .7😁
 
Sie wengine internet cafe ilikuwa ni centre ya kucheza games za mortal combat, need for speed na mpira tu
 
Nakumbuka Kicheko Internet cafe Moshi, Arusha Cybernet, Golden Rose cafe, kuna zingine internet cafe zingine mbili sikumbuki majina ila zilikuwa zinatazamana na stendi ndogo Arusha... nilichati sana marafiki.com. Nakumbuka nilipata demu kwenye mtandao wa marafiki ila alikuwa akiishi mbali..

Ilikuwa tuonane baada ya miaka kadhaa ila nilimkimbia aliposema tutaonana Arusha kwasababu atapita alikuwa anaelekea Samunge kwa babu wakati babu bado hata hajavuma. Kwa wakati ule watu wa Arusha tulikua tunajua babu anatibu ngoma tu bahati nzuri baadae akasema na magonjwa mengine anatibu.
 
Hili game nimelicheza sana enzi hizo
2007
Nilikuwa DESKTOP
hp COMPAQ pentium 3 speed 900mhz
Ram 512sdr HDD 20gb(IDE) ikiwa na DVDrom CDwriter
Then mwaka 2008 nikaupgrade kwenda 80gb IDE
dah! Unajua 80gb nilinunua sh ngapi nilinunua 120000/= aisee kwakuwa nilikuwa nishaanza michezo ya torrent MOVIE sikuwa na namna nikalipia tu mana storage ilikuwa haitoshi
 

marafiki.com ilihit sana enzi zake.
 
Darhotwire, mzibo, worldsex, yahoo, hotmail.

Internet cafe mitaa ya Vingunguti mbili tu. Kwanza ilianza moja hapa jirani na Kongwa bar kwa mbele kama unaenda machinjioni halafu baadae ikaongezeka nyingine. Dah kweli umri umeenda halafu bado sina kitu aisee!

Popote ulipo bro Denis (st elydam 2003). Ahsante kwa kunifundisha computer wakati huo ingawa nilikuwa nalipia saa zima, anatumia dakika 50 kwa mambo yake halafu zikibaki dakika kumi ndio anaanza kukufundisha😃😃😃😃.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…