Kama ulianza kutumia Internet mapema miaka ya 1990 na 2000 njoo hapa tukumbushane Internet Cafe tulizoenda, Vimbwanga, Kero na Kumbukumbu

Kama ulianza kutumia Internet mapema miaka ya 1990 na 2000 njoo hapa tukumbushane Internet Cafe tulizoenda, Vimbwanga, Kero na Kumbukumbu

Morogoro mjini internet cafe ni manyisa hapo ni 1996+
Ma matunda hahaa nilikuwa nikiingia cafee na vuta task manager na kusimamisha ile stop watch yao...ili muda usiisheee

Yahoo messenger na msn si mchezo

Hizi ilikuwa wachagua room ya kuingia na nchi kisha unakutana na wadau wa kila namna na kumbuka code hii ASL ilikuwa maarufu sana

Yaani uki mpa hi mtu alie online anakuchapa na ASL
akimaanisha umtajie Age yako, Sex yako (jinsi) na Location yako.

Game ya super mario
Project IGI
Delta Force etc

Social platform za enzi

Tagged (huu mtandao ukanipatiaga mtoto bikira haha)
My space
Hi5

Hii blog pendwa kabisaaa miakaya 2000s ilikuwa "utamu kujing'ata ulimi" ilipata misukosuku baada ya adobe photoshop 7 kutumika chakachua picha ya bwana yuleee. But ilikuwa blog pendwa saana kurekebisha tabia haha.

Duuuh muda waenda kasi sana
 
Ile Cafe ya kaributanga licha ya kua na room za maboksi zilikua na vijispeaker kabisa vile vidogo vya mezani.
Basi uko zako bize unasikia next room minyanduano live. Yaani ilikua zaidi ya danguro.
Kipindi hicho Kuna mzibo dotcom utaangalia miziki mipya ya East coast team use wimbo wa Sema nao Kuna lady jd. Gk wametinga kombat za jeshi.
Utaanzaje Kua wakishua wakati haumiliki email address?
Hydery plaza ilikuwepo moja ya kifaza sasa dizaini siku hiyo nimetulia kumbe niko worldsex, umeme ukakata. Sasa ulivyorudi ikadisplay palepale ilipozimia. Mdada mhudumu anapitia kila kompyuta kuweka mambo sawa.
Halahaulaa kakuta mnyanduo live nahangaika kuclick kuondoa page imestuck. Akaishia kuniangalia tu akasepa zake.
 
Nakumbuka nilipoteza account yangu ya jf 2012 internet cafe, email yangu ya sasa nilifungua 2008 mpaka leo ninayo, facebook account yangu nilifungua 2011 mpaka leo ninayo.
Intaneti cafe zilitusaidia sana .
 
Bagamoyo kulikuwa na Internet Cafe mitaa ya ADEM, Nilikuwa naenda kuperuzi ngoma kali za mamtoni pamoja na SMS kali za mitongozo kisha nazituma kwa watoto wa kishua mitaa ya mbezi beach.

Bila kusahau kusearch jinsi ya kupata pesa bila kufanya kazi. Ki ukweli internet cafe ilinipa maujanja na nilipiga pesa kwa wale wakuja. Wazungu wa Bagamoyo walinipata vema mzanaki mimi.
 
Kulikuwa na Dar talk(something km hivi),kabla ya facebook kulikuwa na Skype..kulikuwa na BBM MESSENGER ilikuwa kama WhatsApp vile,thanks kwa mchina kuleta hizi cmu maana ilikuwa ukidownlpad hata media yenye mb 10 tu inakuandikia 36 years to complete!![emoji23]
Yahoo messenger, Nimbuzz
 
Binafsi nilianza kutumia internet mwaka 1996 hivi, kabla ya kuanza kutumia internet unatafuta dial up connection, kwa kupiga sim ya computer kwa service provider, ikisha connect ndio nafungua microsoft outlook ili kusoma email.

Provider mkubwa kwa hapa Dar nakumbuka miaka hiyo alikua Raha.com, africa online, cats net wengine siwakumbuki.
 
Kwenye 1998 hivi tulikuwa na morali wa kwenda mbele, ikawa ukitaka kuandika emails za kuomba chuo unaenda posta kariakoo na mbarua wako unampa mhudumu wa pale posta unalipa shs 800 ana-type na kuituma kupitia Africa online, wewe unakaa nyumbani kusubiri prospectus yako kupitia S.L.P.

About 1998-1999 tukawa tunaenda UD-ardhi na mshikaji wangu ambaye sister wake alikuwa anasoma pale, anatupeleka computer room kulikuwa na internet connection lakini mouse hamna tunakomaa na keyboard tu (ilikuwa ngumu sana).

About 2000-2001 nilikuwa naenda IFM kwa mshikaji wangu aliyekuwa anasoma pale,Kila mwanafunzi alikuwa na password yake, akawa ananiachia natumia na mpaka sasa ninayo address niliyofungua pale (jinalangu2001@yahoo.co.uk).

Internet cafe yetu maarufu ilikuwa Richmond pale kariakoo karibia na round-about. Japo zilikuwepo zingine ndogo mdogo mitaani.

Sasa kati ya 2002 na 2003 nikapata Compaq pc Pentium ya windows 98 lakini ilikuwa inatumia floppy disks tu. Mwanangu mmoja akitoka bongo records na cd yenye ngoma zake za album anataka tuziingize kwenye computer lakini ndo hivyo tena haiwezekani. Mungu si Mayele nikapata HP Pentium II tower yenye windows ME na CD-ROM, then windows XP, hapo sasa nikaanza kuhifadhi mangoma ya Wana. Then nikanunua CD writer (kazi ikaanza). Flashdisk ya Kwanza ya MB 128 niliinunua KVD kwa shs 35,000.

Baadae Zantel wakatuletea dial-up connection (simu za mezani) kwa shs 96,000, unaweka vocha ya elfu 5 au 10 unapata network Safi.

Sasa kilchoendelea baadae, Sote tunaona. Bado kugusana tu kupitia mtandao.
 
Mnakumbuka enzi za marafiki.com na dar hotwire?
Mnapiga soga kwenye live chat ukimwelewa bibie unazama nae room, hapo mtongozo unaendelea.
Kwa wale wa yahoo messenger lazima uzijue swaga za kule, ingilish kidogo na vifupisho mfano asl pls. hapo utavuna dame wa kizungu, utamuimbishaa ukiona timer inakaribia kuisha unamtumia email address umwendelezee huko.
Daah maisha yalikua poa sanaa!
 
Mwaka 2001 naingia Internet Cafe Garden Street ili Ni check email zangu nafunguwa Yahoo nakutana na American under attack, Hakuna ukurasa unaofunguka wala Hakuna access ya kuingia inbox.

Ndege zote zilizopo Marekani haziruhusiwi kuondoka wala zinazota kuingia haziruhusiwi.

Aisee nilimmind sana Osama Bin Laden, aliharibu Mipango ya watu wengi na hapo nimeshajiandaa kuingia Embassy enzi hizo Kinondoni next week tu.
 
Kulikuwa na Dar talk(something km hivi),kabla ya facebook kulikuwa na Skype..kulikuwa na BBM MESSENGER ilikuwa kama WhatsApp vile,thanks kwa mchina kuleta hizi cmu maana ilikuwa ukidownlpad hata media yenye mb 10 tu inakuandikia 36 years to complete!!😂
Dar Hotwire
 
Back
Top Bottom