Kama ulianza kutumia Internet mapema miaka ya 1990 na 2000 njoo hapa tukumbushane Internet Cafe tulizoenda, Vimbwanga, Kero na Kumbukumbu

Kama ulianza kutumia Internet mapema miaka ya 1990 na 2000 njoo hapa tukumbushane Internet Cafe tulizoenda, Vimbwanga, Kero na Kumbukumbu

mwaka 2009/2010 nilikuwa natumia simu kuingia facebook sasa simu nilikuwa natumia ya sista angu nilivyomrudishia simu yake nikamiss kuperuzi . siku hiyo nikaenda internet cafe basi nikaingia zangu fb kumbe huyo mzee apita pita kuchungulia ali vyoona nipo fb aisee alifoka eti mambo gani hayo ya kihuni huni watoto wa siku hizi sijui mpoje aisee nilinyanyuka nikasepa zangu kimya kimya.
Mwaka huo nakumbuka niliwah kwenda internet cafe kufungua account ya fb
 
Time Watcher ile ina nembo ya jicho

Windows Xp Vista, ule mlio wake..

User interface yake..jinsi ya kucopy files..

Lile gemu la draft , mortal kombat, need for speed
Hii time watcher itabidi nianze kuitumia kwa wanangu wasitumie sana simu na pc 😂 😂

1686135068854.png
 
mwaka 2009/2010 nilikuwa natumia simu kuingia facebook sasa simu nilikuwa natumia ya sista angu nilivyomrudishia simu yake nikamiss kuperuzi . siku hiyo nikaenda internet cafe basi nikaingia zangu fb kumbe huyo mzee apita pita kuchungulia ali vyoona nipo fb aisee alifoka eti mambo gani hayo ya kihuni huni watoto wa siku hizi sijui mpoje aisee nilinyanyuka nikasepa zangu kimya kimya.
Na kipindi hicho ishu za freemason zilikuwa ndio zimeshika moto basi wazee wakiona mtu anatumia facebook wanaiunganisha na freemason.
 
Miaka ya 2002 maeneo ya Sea boys internet Cafe hapo Magomeni Mapipa.
Pia Tegeta pale kighorofani na pale Morogoro jirani na ofisi ya Abood ya mjini Masika.
Tumetoka mbali sana.
 
Miaka ya 2002 maeneo ya Sea boys internet Cafe hapo Magomeni Mapipa.
Pia Tegeta pale kighorofani na pale Morogoro jirani na ofisi ya Abood ya mjini Masika.
Tumetoka mbali sana.
Pia millenium towers internet cafe pale Mhudhuriaji maarufu Marehemu Roy wa G records alikuwa anajifunza kupiga biti pale miaka ya 1999
 
Nimeanza na Hotmail, yahoo mail na marafiki.com Miaka ya 1998 / 1999 wakati huo ulizuka Uvumi Kwenye Mitandao kuwa ikifika 2000 new millenium kutatokea Tukio kubwa la kidunia wengine wakisema ndio mwisho wa dunia .

Nimetumia Cafe kadhaa za upanga , fire , kisutu, nakiete mwenge , kariakoo livingstone
 
HAPA KWETU TEGETA, I C ZILIKUWA CHACHE SANA. PALE TGT PK BAR, NJIA PANDA KWA MASISTA, KIBAONI NA WAZO MAGHOROFANI. NILIJIFUNZA MAMBO MENGI YA DUNIANI KUPITIA HIZO I C. NILISOMA SANA BBC, VOA NA DW. SIKUWA MPNZ SANA WA XXX. NILICHAT NA MARAFIKI WENGI NA HASWA WA NJE YA NCHI. HAPO MATUMIZI YA CM ZA MKONONI HAYAJASHAMIRI SANA. MWALIMU WANGU WA INTERNET BAADAE AKAWA MY WANGU. KWA7BU NILIKUWA NINA VIJISENT, NALIPIA MASAA MAWILI, HALAFU NATUMIA SAA MOJA, NA YEYE NAMUACHIA SAA MOJA. HOTMAIL AU YAHOO NDIYO ILIKUWA HABARI YA MJINI. UKIWA NA E-MAIL, HUKO SKONGA MADUU KAMA WOTE. KTK MAGAZETI KUNA UKURASA WA KUTAFUTA MARAFIKI, UNACHUKUA E-MAIL, UNACHAT NAYE THROUGH INTERNET. KINACHOENDELEA HAPO MTAJUA WENYEWE. KTKT YA KUNDI LA WATU WENGI HAWANA NA HAWAJUI MATUMIZI YA E-MAIL, WEWE MWNY E-MAIL UNAJIONA MTU WA PEKEE SANA.
 
View attachment 2648410
Kama hukutumia MSN Messenger, Yahoo, Skype chatroom za DarHotWire & Bongo5, Waptrick......and the likes, endelea kufurahia ujana wako!!!
Kwakweli kama hujatumia waptick kwenye simu za batani Nokia miaka ya 2007 bado huwezi kujiita mkongwe...

Cheo maalum cha wahenga kipo kwajili ya wale walioanza kutumia 90s mwishoni na 2000s mwanzoni 😂😂
 
😊Matunda Cafe Morogoro, nakumbuka back in days kulikuwa na vipazia full kuwaangalia akina Nikki Tyler,Vanessa Blue n.k life was good kwani privacy iliheshimiwa

Computer no .7😁
Kuna internet zilikuwa maalum kwajili ya kuwarahisishia kazi wapiga chabo .
 
Nimeanza na Hotmail, yahoo mail na marafiki.com Miaka ya 1998 / 1999 wakati huo ulizuka Uvumi Kwenye Mitandao kuwa ikifika 2000 new millenium kutatokea Tukio kubwa la kidunia wengine wakisema ndio mwisho wa dunia .

Nimetumia Cafe kadhaa za upanga , fire , kisutu, nakiete mwenge , kariakoo livingstone
Nami nilijisajiri email mbili kwa siku moja, yaani yahoo na hotmail. Nikaja 'kulazimishwa' kuwa na gmail na hizi simu za sasa. Nilijiunga kwenye Cafe ya Barmeda, Mwanza mjini. Sasa, wakati ule kijiunga na hiyo yahoo, ilikuwa usumbufu sana. Unaulizwa na kujibu maswali kibao! Na, tulipoanza kutumia simu, napo ikawa shida, mara unaambiwa umetumia simu tofauti na uliyokuwa unaitumia, basi wanaifungia hiyo email yako. Kuirudisha, inakuwa shida sana. Yahoo yangu ishachukua miaka .miwili kuirudisha. Hawa jamaa wa gmail walipokuja, wamewanyoosha sana. Unajisajili ndani ya dakika tano tu, bila maswali ya hovyo hovyo! Nao, yahoo, wameshabadilika, hawana urasimu tena!
 
Iringa moja, 2000, nataka email niwasiliane na rafik ang denmark... naingia cafe namueleza jamaa... ananiwekea time watcher af anasepa akijua nafahamu kitumia..... dah nilishangaa adi muda unakaribia kuisha ndo napata akili ya kudesa kwa mwana hapo pembeni.... nikaishi kujua mouse inafanya kaz gani.... ila kuanzia keaho yake nikawa naenda kujifunza.... ndani ya wiki nikawa vizur
 
Magomeni kulikuwa na internet cafe moja kubwa sana kama sijakosea jina kwa kusahau ilikuwa inaitwa kama sio Sea Boys basi ni Home boys ilitamba sana miaka hiyooo..

Ilikuwa ghorofani ina computer kibao kama 50 hivi
hatimaye nimekutana na mshirika wangu
 
Back
Top Bottom