Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sea boyz Magomeni, Kariakoo karibu na msikiti wa Manyema, Morogoro rd karibu na kituo cha mafuta opp na Mtendeni Pr Schoo, Posta Kisutu na mwisho kabisa Stambuli Cafe millenium tower Makumbusho. Nyingi ya hizi cafe zilimilikiwa ama na wahindi au waarabu. Mimi nilijifunzia kompyuta kitambo sana nj ya nchi, na niliporudi nilikuwa mwamba kweli kwani watu wachache sana ndio walikuwa wanajua kutumia kompyuta na hata pia waliokuwa na anuani za email walikuwa wachache sana.MUHIMU: UZI HUU SIO WA KUKUMBUSHANA COMPUTER GAMES
Binafsi nilianza kwenda Internet cafe 2002, computer zilikuwa zenye visogo 😂 .
View attachment 2648381
Mitanado maarufu kwa hapa bongo ilikuwa ni Marafiki.com na DarHotwire, baadae zikaja Jamboforums (kwa sasa jamiiforums), Hi5, Bongo 5,
View attachment 2654435
tulikuwa tunalipia kwa muda kuanzia nusu saa, Ukilipia wanawasha program ya kuhesabu muda, iliitwa time watcher muda ukiisha inaloki computer, Wajanja walikuja na mbinu za kuruka hiki kiunzi 😂
View attachment 2654432
Speed ilikuwa chini sana, kufungua ukurasa wenye picha unaweza subiri dakika nzima, ukitaka soeed nenda asubuhi sana.
View attachment 2654433
Kuwa na email ilikuwa ndio ujanja wa enzi hizo, Tulichat na kutumiana barua kwa email. katika watu 100 waweza jikuta pekeyako unayo basi unapata ka feeling flani ka v.i.p, email maaarufu ilikuwa hotmail, yahoo na msn.
View attachment 2654431
Enzi hizo tulitumia floppy disk kuhifadhi mafaili, ni kipindi ambacho bado cd na flash hazijawa common.
View attachment 2654434
Enzi hizo websites www.-----.com ilibidi uwe uzitunze kichwani ama uwe na ki diary maalum, Sio kama sasa google imerahisisha sana
View attachment 2654446
Waliokuwa hawana speed ya kutumia keyboard. walijifunza kwa kutumia program inaitwa mavis bacon
View attachment 2654448
///////////////////////////////////////
Hali imebadilika, kwa sasa unaweza kuwa na smartphone au laptop yako unaingia net, Hali haikuwa hivyo kwa miaka ya nyuma kabla ya 2010s, Kipindi hicho ilikuwa ni mwendo wa cafe.
Miaka ya 2007 angalau tulianza kutumia internet kwenye simu za Nokia batani na tovuti maarufu ilikuwa waptrick lakini hizi tobuti bado zilikuwa simple sana, bado tulilazimika kwenda internet cafes kupata mambo kamili,
2010s ndio Modems za kutumia kwenye laptops na simu za kisasa zaidi zenye uwezo mkubwa wa kuperuzi internet zilipoanza kujaa sokoni ndipo wengi tukaacha kwenda internet cafe na hii ikapelekea cafes nyingi kufungwa ama kugeuzwa kuwa stationery.
Bila kusahau Matunda'sMorogoro mjini internet cafe ni manyisa hapo ni 1996+
MB 1 ilikuwa Sh 400Hiyo bongo5 nakumbuka nilikuwa nanunua mb 10 kwa shilling 500 na haziishi