Kama ulianza kutumia Internet mapema miaka ya 1990 na 2000 njoo hapa tukumbushane Internet Cafe tulizoenda, Vimbwanga, Kero na Kumbukumbu

Nilifanya utundu kwenye time watcher mhindi akanishtukia akasema usije tena hapa, wewe itafundisha na nyingine.
 
Mhudumu anakwambia marufuku kuangalia pono!
 
A
A-Tech Njombe
 
Marafiki com
Ku chat na wajuba

Wote mnaondikaga chart badala ya chat mlaaniwe.
 
Dah nimetumia sana Cafe, enzi hizo ni dialup, Raha Tower, pale Samora na Mission Street, Bibi Titi x Morogoro sasa hivi ni City Mall kulikuwa na shule ya computer pale, Cafe kibao uindini na floppy zangua za 1.4 MB ukitaka kudownload game inabidi uigawanye vipande kumi kila moja na floppy yake, ukifika home floppy ya 5 imekufa! Siku mambo yakawa yes nikanunua Zip Drive kitu kilikuwa kinabeba 100MB, kama mfalme mjini!
 
Enzi za Computer Window 95. ndio atleast ilikuwa speed nafuu.. Window 486 ilikuwa Jau sana Cafe' ni kusubiri tu Game ifunguke ucheze.

Nakumbuka kuna uvumi wa kupata kazi New Caledonian Offshore na website yao so lazima ujisajili and ukimaliza wanakutumia na barua na documantations zote Mshahara mnono kuvuna mafuta na Gas maisha ya baharini..

Yahoo,MSN Messenger,Darhotwire,IPP Media,Darchat,Jambonet,Marafiki dotcom,Zanzibar chat, ESPN, NBA ,Livescore kila siku baadae huko ZEUtamu dot com wakaja kuharibu na edit photo ya jk.. somebody mtoto wa kigogo alikuja kamatwa .

Email zote nilifungua chache niliziacha

Hivi yule jamaa wa Jambo Mod alijiita Invisible aliishia wapi. mkuda yule
 
Ewe mdada wa internate cafe maili moja Kibaha karibu na pale yanapotokea magari nakukumbuka sana.
Mdada uyo namjua mpaka sasa yupo fb mweupe flani hivi mdada wakichaga
 
Daah,nimekumbuka mbali sana, nilianzia TipTop manzese 2002, nikahania Seaboys Magomeni Mapipa, baadaye nikahania cafe ya UDSM block 7, tatizo la hii cafe ya UDSM ni comp nyingine kutokuwa na mouse,unakomaa na keyboard tu ila ilikuwa na speed nzuri.
 
Daah,nimekumbuka mbali sana, nilianzia TipTop manzese 2002, nikahania Seaboys Magomeni Mapipa, baadaye nikahania cafe ya UDSM block 7, tatizo la hii cafe ya UDSM ni comp nyingine kutokuwa na mouse,unakomaa na keyboard tu ila ilikuwa na speed nzuri.
Cafèe ya UDSM mizinguo. Haina privacy wa kunicheki 'MIPICHA' yetu.
Pale Seaboys na ile nyinge upande wa pili Magomeni zilikuwa na Privacy partition ya Internet.
Hatari sana.
'MZIBO'.net ilikuwa hatari sana na DarhotWire..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…