Kama ulianza kutumia Internet mapema miaka ya 1990 na 2000 njoo hapa tukumbushane Internet Cafe tulizoenda, Vimbwanga, Kero na Kumbukumbu

Matunda cafe Moro nilikuwa natoroka shule kwenda kujibu email za rafiki yangu aliyekuwa abroad 🤣🤣🤣
 
Sea boyz Magomeni, Kariakoo karibu na msikiti wa Manyema, Morogoro rd karibu na kituo cha mafuta opp na Mtendeni Pr Schoo, Posta Kisutu na mwisho kabisa Stambuli Cafe millenium tower Makumbusho. Nyingi ya hizi cafe zilimilikiwa ama na wahindi au waarabu. Mimi nilijifunzia kompyuta kitambo sana nj ya nchi, na niliporudi nilikuwa mwamba kweli kwani watu wachache sana ndio walikuwa wanajua kutumia kompyuta na hata pia waliokuwa na anuani za email walikuwa wachache sana.
 
Umenikumbusha mbali sana nilikuwa na dogde tuition naenda internet cafe kucheza need for speed,mortal combat,vice city,san andreas,project IGI na muda ukifika nami nageuka zangu kama nimetoka tution kumbe nimetok internet cafe....kuna siku game zilinoga mpaka nikasahau muda wa kurudi nyumbani kiza kikawa kinene mno.....kilichonikuta nitakuja kusimulia nikirudi🏃‍♀️
 
Internet nilikuwa na Access free, kwa rafiki yangu SALCOM internet Cafe.
 
Waptrick (Hapa ukitaka miziki ya zamani mingi utaikuta humu);

Wapdam (hii ilikuw kama substitute);

Redwap (Hapa nilikuw natafuta sana WARUMI ukitaka kuwaona unaingia humo);

Ikaja TUBIDY (hii kudownload videos za nyimbo etc)

Nakumbuka enzi hizo kulikuw hakuna kujiunga BANDWIDTH ya MB's ni kuweka VOCHA alafu iliwe mdg mdg...

Facebook ilikuja kutakeover nakumbuka mpk hii leo nimemiliki account si chini ya 5 kule😅.. ikaja whatsapp then instagram..

Pia kuna kipindi hapo kati kulikuw na mvumo wa movies za kihindi, na kinaijeria. Pia nyimbo za kihindi ktk simu za kichina ndio zikawa zinatrend hasa...

Aisee kitambo.. NOTE: simu nimeanza kutumia nikiwa na 7 yrs, sahiv nipo under 30 yrs.. account yangu ya JF ya kwanza nimefungua 2013..😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…