Kama ulihisi UVCCM Simiyu ni kiboko, hebu angalia hawa UVCCM Mkoa wa Mara wakigawana rushwa hadharani

Kama ulihisi UVCCM Simiyu ni kiboko, hebu angalia hawa UVCCM Mkoa wa Mara wakigawana rushwa hadharani

Hii video nimeiona sehemu ikabidi nipate uhakika kisha niipost.
Hawa ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Mkoa wa Mara wakigawana Rushwa hadharani bila woga wala soni. Kama vijana wadogo wanalelewa hivi, je hiki chama kina nia kweli ya kutokomeza rushwa?


View attachment 2423201
Ndo tutegemee uchaguzi huru na haki kwa msingi huu?
 
Mkuu unajuaje kama hiyo ni rushwa na wala si posho za mkutano?
Kama nilivyosema awali nimefuatilia kwanza ndio nikaipost, hakuna posho ya aina yoyote iliyotolewa siku hiyo ya uchaguzi.
 
Alafu mbona kama wanagawana elfu kumikumi au ishirini ishirini hivi...hela mbuzi kabisa.
 
Baada ya Nyerere Kufariki ccm ilijipambanua Kama Chama Cha ufisadi na rushwa

Unahonga Ili upate cheo tena ndani ya Chama je nje ya Chama?

Suluhisho watu siku tuamue tuingie barabarani but shida ya watanzania wakishashiba Mihogo na ugali wanasahau kwamba rushwa inakwamisha Sana maendeleo yao.

Leo hii nchi ipo kwenye giza la umeme sababu ya Rushwa ya mikataba mibovu Kama Richmond, Dowans, IPTL na juzi symbion kalipwa mabilioni bila kodi.

Hiki Chama kinafundisha watoto jinsi ya kuiba pesa za watanzania bahati mbaya mtu akisema ukweli anpewa majina ya kila namna.

Suluhisho la haya ni kuingia barabarani tu hakuna option nyingine!!! Other wise tuendelee kupigwa.
Ishu sio kuandamana bali unaandamana kwa ajili ya nini??

Sidhani kama sisi ni waoga kiasi hicho ila nadhani ni kukosa ajenda ya pamoja ya kutufanya tuandamane.
Baadhi yetu ukosefu wa kitu fulani ni fursa kwa wengine, hivyo wanatamani kiendelee kuadimika wafanye biashara. Na bahati mbaya zaidi unakuta hicho kitu kinawanufaisha watu wengi mno hivyo kua na unafiki ndani yake harakati zikianza.

Mfano ishu ya maji, walalamikaji ni waishio mijini ambapo maji yalikua yakipatikana lakini mikoa mingine maji sio tatizo kabisa mfano Mbeya, hivyo mtu wa Mbeya kulalamikia maji sio rahisi coz hajui ugumu wa kuyapata.

Mfumuko wa bei, wafanyabiashara wengi wananufaika na hiki kitu japo kwa nje wanalaumu ila deep down wanafaidi sana baadhi yao.

Tatizo tunakosa hiyo sababu ya kuwatoa watu majumbani, labda ule uchaguzi wa 2015, kama chadema ingeamua mbwai na iwe mbwa watu wangejitoa coz ilikua ishu inayojumuisha watu wengi mno.

Uchaguzi wa 2020 asngetoka mtu, tayari watu maslahi waliyaweka mbele.
 
na waliopo pichani tunawajua kwa sura na majina yao aibu hizi huku kwetu Mara hazikuwepo
Nafikiria chama kitachukua hatua stahiki kwa haya yaliyojitokeza, mtoa rushwa na hao mnaowafahamu waliopo pichani
 
Hii video nimeiona sehemu ikabidi nipate uhakika kisha niipost.
Hawa ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Mkoa wa Mara wakigawana Rushwa hadharani bila woga wala soni. Kama vijana wadogo wanalelewa hivi, je hiki chama kina nia kweli ya kutokomeza rushwa?


View attachment 2423201
Hii ilitosha Kwa Chama makini kufuta uchaguzi wote.

Halafu ktk haya yakiendelea Eti Kuna watu wanataka tumtetee mkt kuwa "Anaupiga mwingi'' eti'
 
Hii ilitosha Kwa Chama makini kufuta uchaguzi wote.

Halafu ktk haya yakiendelea Eti Kuna watu wanataka tumtetee mkt kuwa "Anaupiga mwingi'' eti'
Ni kweli chama makini hakiwezi kuruhusu haya. Ukisema ukweli unaonekana umeisaliti nchi
 
Back
Top Bottom