Kama ulihisi UVCCM Simiyu ni kiboko, hebu angalia hawa UVCCM Mkoa wa Mara wakigawana rushwa hadharani

Kama ulihisi UVCCM Simiyu ni kiboko, hebu angalia hawa UVCCM Mkoa wa Mara wakigawana rushwa hadharani

Atashambuliwa aliyerekodi clip na jamvi la siasa JF badala ya wala na watoa rushwa
 
Wakuu mimi simu haina chaji, nyie umeme mnatolea wapi aisee? Au tumerudi kwenye maisha ya powerbank
 
Ulikuwa hujui?ccm huwezi kupata uongozi pasipo kuwapa hongo wajumbe,kama huna hela usijiingize kabisa kwenye siasa za ccm,huko ndiko chuo cha wizi nchi hii kilipo,tokea ukiwa mdogo unaelewa kuwa uongozi unapatikana kwa kutoa rushwa tu so tafuta fedha kwa njia zozote zile ili upate madaraka
 
Nakubaliana na wewe ila tukio hili kutokea kwenye ardhi aliyozikwa Baba wa Taifa inaonesha ni kwa kiasi gani CCM imekwisha
 
Hii video nimeiona sehemu ikabidi nipate uhakika kisha niipost.

Hawa ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Mkoa wa Mara wakigawana Rushwa hadharani bila woga wala soni. Kama vijana wadogo wanalelewa hivi, je hiki chama kina nia kweli ya kutokomeza rushwa?

View attachment 2423201
Dawa ni kuondoa ccm madarakani uingie mfumo mpya tusonge mbele bhana.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Baada ya Nyerere Kufariki ccm ilijipambanua Kama Chama Cha ufisadi na rushwa

Unahonga Ili upate cheo tena ndani ya Chama je nje ya Chama?

Suluhisho watu siku tuamue tuingie barabarani but shida ya watanzania wakishashiba Mihogo na ugali wanasahau kwamba rushwa inakwamisha Sana maendeleo yao.

Leo hii nchi ipo kwenye giza la umeme sababu ya Rushwa ya mikataba mibovu Kama Richmond, Dowans, IPTL na juzi symbion kalipwa mabilioni bila kodi.

Hiki Chama kinafundisha watoto jinsi ya kuiba pesa za watanzania bahati mbaya mtu akisema ukweli anpewa majina ya kila namna.

Suluhisho la haya ni kuingia barabarani tu hakuna option nyingine!!! Other wise tuendelee kupigwa.
Naam ccm itoke hakuna muda wa kusubili.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mambo yankawaida sana hayo kwa CCM.
Nchi nzima ndivyo mambo yanavyoenda. Hawana wasiwasi kabisa wanagawana tu ufisadi.
 
CCM itolewe kama nduli Idd Amin Dadaaa alivyoondolewa
wachapwe viboko 24. 12 wakati wanaingia gerezani na 12 wakati wanatoka ili wakawaoneshe wake na waume zao
 
Huu ni uzushi tu, hiyo video haiwezi kuthibitisha hiyo ni rushwa, umbea umbea Tu, ni imetengezwa kwa makusudi si unaona hata wao wenyewe wanaagali kama vile wanajua ?
Umbea ka mwingine tu
 
Back
Top Bottom