Mtoa uzi naona umenikumbusha jambo fulani ambalo nilishawahi kunitokea humu.
Nilileta uzi humu wa kutafuta mchumba wa kwenda kuyajenga, baadhi yao wakanifata pm na hata kubafilishana namba za sim. Balaa lilikuja kwenye kutumia picha yaani kuniona tu alikatisha mawasiliano maana yake alijua atanikuta nipo kwenye jumba la kufahari. Yaani sijui hata nilimkera nini nilijitafakari sana. Mwengine alinuna baada ya kumwambia naona kibonge akaanza kuniuliza "kwani vibonge huwataki?" Nikamjibu kawaida basi na yeye akapotea ghafla kisa nimemwambia ni kibonge wala sikua na nia mbaya.
Kwa wafupi wanawake wengi wa humu wanaojipambanua hawana lolote, avatar unayokutana nayo hapa ukimuona mwenyewe yaani ni shida hata kumtambulisha kwa marafiki zako inashindikana kwa aibu.