Braza Kede
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 5,168
- 8,982
duh hii kali. sasa ulienda kudai ela yako kwa mwenye nyumba au uliogopa kuongezwa viboko?Ukweli uchawi Upo tena uhakika
Mimi Nina visa 3 mwenyewe kwenye maisha yangu.
Cha kwanza kilinitokea nikiwa na miaka 6 mwaka 92 na cha pili kilinitokea mwaka 2008 nikiwa mkubwa na elimu yangu kwa hakika uchawi Upo tena sana
Mwisho nilipanga nyumba mtaa wa mecco Mwanza nyumba nzuri ipo katikati ya nyumba nyingi sana nikalipa zangu kodi 1.5m kipindi hiko nimehamia mwanza kikazi Niko zangu single
Usiku nilichapwa viboko sijawahi Ona ananichapa simuoni kesho yake nikasema labda ndoto,saa 2 tu usiku bakora za kutosha,nikaamua kwenda kulala guest asee
Baada ya siku nikahama
Hii nyumba mpaka leo ipo pale mecco kwa ambao hamuamini uchawi nenda kashuhudie mwaka wa 6 haina mpangaji wala binadamu anaishi pale
Waganga na waombaji hawajafua dafu
Inasemekana walimuua mwenye nayo wakaidhurumu malipo ndio hayo.
😄😄😄nimecheka sana na hii storiNakumbuka miaka ya nyuma niliamua kuanzisha biashara ya bar maeneo ya wazo hill, target kubwa ikiwa ni marafiki zangu ambao walikuwa wanafika sana kwa mwanangu mmoja ambaye alijenga huko na wanakunywa sana hata idea ya kuanzisha iyo bar walinipa wao kwa sababu ilikuwa ndio michongo yangu
Ile bar ilianza vizuri sana na mimi binafsi sikuwa hata na muda wa kwenda sana huko ila nilimuachia dada mmoja mchakarijaji kweli kweli kama manager mimi weekend mnaenda kufunga mahesabu
Iyo siku balaa lilianza kuanzia mida ya saa moja usiku hamna mteja yoyote aliyefika pale na siyo kawaida mida ya saa 3 usiku wakaja watu wawili kila mmoja na gari yake mwanamke na mwanaume, mwanamke akaagiza kreti nzima ya soda, na mwanaume akaagiza ya bia, na wanataka ziwepo hapo hapo walipokaa, mhudumu akaenda kuchukua walivyoleta wakakuta wameongezeka wamekuwa wanne na hapo walipokaa ni juu kwenye ghorofa na kupita ni lazima mtu wa counter chini akuone...mhudumu akawauliza mbona sijawaona mkipita wakasema sisi tumekuona ongeza kreti ya soda na bia, akawabia kunyweni kwanza hizo wakamkazia macho akaenda kuongeza na bia wanazotaka na soda ni za aina zozote zilizopo, muhudumu kirudi akakuta wapo 8, na gari nje zimeongezeka, akaambiwa aongeze tena 8, zile 2 za mwanzo zimeisha, akampigia mtu wa bia za jumla amletee japo alikuwa amefunga akakubali
Zilipofika kupanda juu akakuta wameongezeka wamekuwa wengi na hakuwaona wakiingia ghafla akamuona mmoja anapiga hatua kupanda juu, yani yupo parking kapiga hatua kupanda ghorofa ya kwanza, alizimia hapo hapo jamaa wa jikoni alikuja kukutwa amepooza baada ya kutibiwa kiasili alipona na yule wa counter aliokotwa kwenye kile kibwawa kisichokauka pale wazo ukielekea madale, hizo taarifa ziliniogopesha sana na uwekezaji wangu ukaishia hapo hapo sikuwahi hata kufuatilia kijiko pale...kumbe mwenye nyumba alikuwa na mambo yake alinipigia simu nikamwambia nimesafiri hivyo vitu avichukue
Maskini, last seen ya madame ni septemba 2021 na apo damu ilikuwa inakatakata. Yuko hai kweli huyu? Kama sio apepe.Cjawahi kuona mazingahombwe live Ila nimekuwa na tatizo la kuishiwa damu na hata Nile nini kuipandisha ni mitihani. Hili tatizo Sikuwa nalo kabla. Tatizo lilinianza baada tu ya kuishi wilaya flani kibiashara ambapo nilipigwa vita sana niifunge ile biashara nikakomaa.
Umetudanganya! Mguu wa kwanza umetoka halafu unaepataje usingizi?Kijiji kimoja mkoa X, mzee mmoja alipowaona kuku wa jirani wanashambulia mahindi shambani mwake akaamua kuwatimua kwa kuwapiga na mawe.
Alipoamka asubuhi akajikuta mguu mmoja umetoka uko pembeni hakuna damu wala nini, akiwa katika taharuki nini afanye akalala tena kuamka kesho yake mguu wa pili pia umetoka uko pembeni.
Mpaka leo huyo jamaa yuko na ameshakuwa mzee haelewi nini kilimkuta anatumia wheel chair, uchawi upo.
C&C = Copy & Paste.Ni 2016 nilivyokuwa nime maliza kidato Cha 4 nikaona Kwa muda ambao nasubiria matokeo niende mgodini, mahesabu yangu yalikuwa kama nikifanikiwa huko basi mambo ya shule naachana nayo.
Nikapata wazo kabla ya kwenda mgodini niende kwanza Kwa mganga maana stori zilizo kuwepo ni kwamba ukienda Kwa mganga akakusafishia njia inakuwa ni rahisi kufanikiwa huko, ikabidi nifunge safari mpaka singida kiyomboi huko alikuwepo mtaalam ambaye alikuwa amevuma Kwa wakati huo.
Nilivyo fika akaniambia gharama ni laki mbili tu, nikampa laki akaniambia hiyo laki nyingine nitaenda kumalizia siku nitakapo rudi kutoa shukrani, hapo hapo akaanza kuniangalizia kutumia vifaa vyake, Baada ya hapo akanipeleka sehemu Kuna kama msitu flani hivi tukaingia kati kati, tulivyo fika mle akaniambia nikae chini huku nimevaa shuka tu jeusi akaniambia baada ya muda utaona kamba mazingira haya utaichukua uje nayo nyumbani, yeye akawa ameondoka.
Niliendelea kukaa pale huku nikiangaza huku na kule Ili nione kamba lakini wapi, nikiwa nimesha kaa muda mrefu mara akaja nyoka mkubwa nilipo kuwa na akawa ananisogelea taratibu huku katoa ulimi, ilibidi nikimbie Kwa woga mpaka nyumbani Kwa mganga nikamueleza hilo tukio, alinifokea sana na akataka kunifukuza kwake, kiukweli yule nyoka kumbe ndo kamba yenyewe ndo alicho maanisha mganga.
Nilimsihi mganga anisamehe na mwisho akanisamehe, kesho yake akanipeleka sehemu tena Kuna mlima mkubwa ni sehemu ambayo watu hupita wakati wanaenda mashamba ya mbali, tukiwa tupo chini bondeni kabisa mganga akaniambia Anza kupanda hii barabara na upite katikati yake mpata utakapo fika mwisho, mganga yeye akawa ametoweka nikaanza kupanda taratibu, nikiwa kati kati ya mlima niliona farasi wa 4 wakubwa kama tembo Wana shuka Kwa kasi ya ajabu huku nyuma Yao Kuna vumbi jingi mno, nilijikaza Ili nisiwapishe lakini nikashindwa nilijikuta najirusha pembeni, muda ule ule ndani ya saa Ile Ile nilijikuta Niko nyumbani kwetu Morogoro tena ndani ya chumba changu.
Nikiwa natafakari hapo nikabanwa na haja ndogo, nikawa nimeinuka kwenda bafuni kukojoa, Ile tu natoa uume nikojoe nikaona mabadiliko nikawa nimejiangalia nikakuta Sina korodani ni uume tu, nilishituka sana nikawa na hofu ya ajabu, kesho yake ilibidi nirudi tena singida, nilivyo fika huwezi amini nyumba ya yule mganga sikuikuta na Kila niliye mwuliza alisema huyo Mzee alisha hama siku nyingi , ilibidi nikae sehemu nikihisi labda naota ila ukweli haikuwa ndoto ni ukweli.
Mpaka Leo Sina korodani na siwezi kushiriki tendo, naishi maisha ya huzuni sana na Sioni hata faida ya elimu niliyo nayo Wala mshahara ninao upata, najuta sana maamuzi niliyo yafanya yame geuka msiba wa milele maishani mwangu, Na hakuna ndugu yangu hata mmoja anaye jua hiki kitu nahofia kuwaeleza japo huwa nasikia wakiniongelea kuwa Mimi ni hanisi mana hawanioni nikijihusisha na mambo ya Wanawake.
C&C
Kwaiyo amekopi 😀C&C = Copy & Paste.
Majanga kama haya ishia kuyakopi au kuyasoma, yasikukute.
Hiki kisa cha uongo!Enzi hizo nikiwa na age ya 6, nilitumwa kununua maziwa afu nje nilishuhudia nguvu ya giza nene balaa, nilirudi home nikiwa na jagi lenye ramani ya maziwa tuu mana ckumbuki yalimwagika muda gani.
Niamini mkuu 😎Hiki kisa cha uongo!
UongooooooooNishawahi sikia kisa kinschohusishwa na uchawi
Kuna masela wawili walienda kwa mganga ili wapate utajiri
Mganga akawapa dawa akawaambia wakaoge usiku makaburini na wakitoka mlangoni kwa mganga hawatakiwi kugeuka nyuma
Basi unaambiwa safari yao iliandamwa na misukosuko yakutisha, mara wasikie muungurumo wa simba akiwa nyuma yao na vimbwenga vingi lakini walijitahidi kukaza ili kutovunja sharti la kugeuka nyuma
Sasa ulipofika usiku majira ya saa 8 ikabidi waende makaburini kuoga ili kumalizia zoezi lao la mwisho ili wawe mamilionea
Walipofika makaburini wakavua nguo wote nakubakia uchi kisha wakapanda juu ya kaburi ili waoge
si unajua ukiwa katika ile mood flani hivi unaoga halafu umefumba na macho ili maji yasiingie machoni.
wakastukia tu paap! wameshikwa makalio kwa nyuma.
Aaah unaambiwa wote ilibidi wageuke nyuma kwa haraka huku wanakimbia na kupiga makelele
Kesho yake kijiweni wakaanza kulaumiana "aaah wewe ndiye ulizingua, we ungekausha bila kupiga mikelele mi nisingechochora kwani kushikwa tako kitu gani bwana" yani leo nisingekua nakunywa kahawa hapa ningekua nimejikoki huko kwenye hotel zinazotambulika na dunia"
MakubwaKisa cha kwanza ambacho kinanivutia hadi leo ilikua mwaka 1998, Niko na jamaa yangu, Tunatokea Shule ya Wasichana Kifungilo tunarudi shuleni kwetu Magamba Secondary (now Sebastian Kolowa University)! Usafiri miaka ile usafiri ulikua wa shida sana, tukawa tunasubiri usafiri pale Mkuzi, SAA Tisa au kumi hivi jioni. Mvua ikaanza kunyesha, wenyeji wakasema kuwa Mvua haitanyesha kwa kuwa Mzee Fulani yuko shambani kwake anauza mapeasi yake.
Ghafla yule Mzee akawa anapita, aiseee seriously kwa Mara ya kwanza tangu nizaliwe sijawahi kuona MTU hanyeshewi na mvua! Yaani mvua inanyesha lakini yeye hanyeshewi kabisa
Sent using Jamii Forums mobile app
Ni weweYuko dogo mmoja alikua anasoma B sekondary. Alikua anamchukua mke wa mtu. Mtu mwenyewe alikua nje ya nchi kimasomo. Ndugu zake msomi hawakupendezewa shemeji Yao aliwe na student. Kuna siku dogo wakapanga na bibie wakapeane penzi kwenye minazi. Enzi hizo gesti wanaingia wenye pesa zao.
Dogo alikua dent hana pesa. Basi kweli muda kufika mke akafika na mechi ikaanza bila refa. Dogo akapakua mzigo kufika kileleni utamu Ulipozidi ni kawaida mtu kufunga macho. Basi dogo wakati anafyatua risasi alimkumbatia mke wa mtu kisawasawa huku amefunga macho. Ile kumaliza na kufumbua macho akajikuta alikua anafanya mapenzi na kisiki cha mnazi na sio mtu. Dogo kutoka pale hakurudi shuleni. Alipanda basi la Dar na kuacha shule. Sidhani kama alisharudi wilaya ya B.
Ukaanza kutoroka mchanaMwaka flani wilaya ya rombo nimetoroka zangu shule usiku wa giza nene kias kwamba hata miti unaiona kwa tabu sana ,nikakatiza mitaa flani ilikua kipindi cha baridi lakini ghafla nikaanza kuhisi joto la hatari mara paaap kumekua kweupe kama mchana wa saa sita na jua kali aiseee nilitimua mbio ile hali ilidumu kama dk moja hivi
Ikawa mwanzo na mwisho kutoroka shule usiku.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ganja
Wakati mwingine hata hatuwaoni ila wanatudhuruDawa ya mchawi usimuogope! Wakati mwengine uoga wetu ndiyo ujasiri wao!