Kama umezaliwa bila ulemavu wowote usiache kumshukuru Mungu hata mara moja kwa siku

Pole best kwa yalokupata.Mungu ni mwaminifu utakua Sawa tena.Hayo makosa yako ya huko pm ndo yameniacha hoi.(sijui ni huku kukosa walau D mbili).Sa moderator unawasemaje?Af kingine kwani hao wanaokusema ushawahi kutana nao uso kwa macho?Akili yangu hapa haielewi kitu.
 
Asante mkuu naendelea vizuri,.
Yaani cha ajabu Hakuna mtu niliyewahi kuonana nae humu in person
 
Aisee
 
Sasa hivi watu wakiwa wanaitana PM nitakuwa nacheka tu
Njoo PM kwanza...

Huu Uzi umenikumbusha nilipokua shule, kulikua tunasoma na watu wenye uhitaji maalum. Sasa nikawa nawaza inamaana Hawa jamaa wanapokua kwenye matukio, zile sauti na maelezo yanayotolewa, vichwani mwao wanakua na mawazo gani au picha gani inawajia? Walikua na changamoto za kuona.
Cha ajabu Sasa, akikushika mkono au akisikia nyayo zako atakuita jina lako hata usipoongea. Walikua na uwezo mkubwa sana wa hisia.

Kama Lee alivyosema, Kuna vitu tunaona kama ni haki yetu au ni sawa kuwa navyo, tunasahau Kuna watu hawana na sio kwamba sisi ni bora kuliko wao au tumefanya cha zaidi kustahili.
 
Ndio hmimi sioni kabisa mwaka wa 14 sasa. Ukishazoea hali uliyonayo unaishi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…