Kama umezaliwa bila ulemavu wowote usiache kumshukuru Mungu hata mara moja kwa siku

Kama umezaliwa bila ulemavu wowote usiache kumshukuru Mungu hata mara moja kwa siku

Wakuu habari za siku nyingi,..

Sikua najua how they feel, sikua najua ni kwa namna gani wanateseka mpaka mda huu ambapo Mungu ameamua anipitishe na mimi kidogo, huenda bila hivyo ningeendelea kuwachukulia kawaida…

Iko hivi,. Nimepatwa na uziwi wiki ya pili sasa ,. I don’t know the mechanism mpaka ilikua hivyo ila nachokumbuka ni kwamba nilipatwa na malaria makali pamoja na kichomi at once,. Nilikua to that point ambayo sikua naelewa chochote zaidi ya jina langu ambalo hata sikua nasikia kama naitwa,..

Namshukuru Mungu naendelea vizuri somehow,. Ila guys viziwi ni wanateseka sana,. Imagine masikio ni mazito, yameziba halafu mda wote unafeel like uko jirani na mtambo ambao unapiga kelele halafu huwezi kurealize ni kelele za kitu gani,,. Means hatakama unataka kuzungumza kitu unahisi wote wanasikia makelele inabidi uongee kwa sauti ya juu sanaaa,. Halafu wanakushangaa unapayuka , which is not easy 😌🥹… Yaani masikio mda wote yako na ganzi hata mtu akufinye husikii maumivu just imagine..

Nipo najiwazia hapa viziwi hii ndio hali wanaifeel for the rest of their lives 🤔, na je ikitokea na mimi nakua kiziwi ina maana ndio nitateseka hivi maisha yangu yote ??? ,.. Thanks Lord nimewahi treatment leo moja limeanza kusikia i hope yote yatasikia tena,. ( Mniombee wananzengo siko poa niko wodini bado,. Malaria nayo nayaniendesha ).

NB: Mtu kama upendezwi na mada za mtu au humuelewi hapa jukwaani ni better ukamuignore kuliko kureport kwa mods nao bila kufanya utafiti vizuri wanapigana ban,. Sio wote tuko humu just for fun,. Yaani wewe uliyenireport sijui hata nikufanye nini maana kuna watu nilikua nao seminar huko Pm na wametoka kunipa tu hela napigwa ban imagine😔😔.. Yaani naitwa tapeli kwasababu ya chuki zako binafsi,. SIJAPENDA
Masikio duh.
Ulipatwa na "Tinnitus" Kuwa makini sana aisee, masikio ni inshu complex sana. Wengine tuna several years na hali hiyo uliokuwepo nayo.

Kuwa makini sana madawa ya malaria unazotumia
 
Ungekuwa dar ungeenda pale Magomeni,kuna hospital kubwa inaitwa Ekenywa..ni maalumu sana kwa masuala ya masikio. Wana vifaa vya uchunguzi na wataalamu walio bobea kwa issue za masikio.

Naweza kukupatia contact za mbobezi mmoja anafanyia kazi pale.
Kwa bongo angalau pazuri ila hamna cha maana ,zaidi ya kupimwa na zile earphone zao , utapewa vidonge wmisho wa siku utaambia utafute vidude vya masikio.
 
Daaah aisee...

Nakumbuka nilisumbuliwa na maumivu ya nyonga nilikua siwezi kutembea kabisa.

Baada ya kupata matibabu nakufanikiwa kupata unafuu kdg nikapewa magongo kama msaada wa kuweza kutembea (kufanya mazoezi)

Aisee kutumia yale mavitu kama msaada wa kutembea ni mtihani sana ikiwa ulikua unauwezo wa kutembea pasi na shida yoyote na ninamshukuru Mungu nikafanikiwa kurudi katika hali yangu ya kawaida {kupona}.

Imagine mtu maisha yake yote yeye ni kutumia magongo tu kutembea mpaka umauti utakapomfika.

Mshukuru Mungu kama upo sawa na tuwaombee ndg zetu wanapitia changamoto kubwa sana.
 
Masikio duh.
Ulipatwa na "Tinnitus" Kuwa makini sana aisee, masikio ni inshu complex sana. Wengine tuna several years na hali hiyo uliokuwepo nayo.

Kuwa makini sana madawa ya malaria unazotumia
Aiseee,. Thanks nitakua makini
 
Daaah aisee...

Nakumbuka nilisumbuliwa na maumivu ya nyonga nilikua siwezi kutembea kabisa.

Baada ya kupata matibabu nakufanikiwa kupata unafuu kdg nikapewa magongo kama msaada wa kuweza kutembea (kufanya mazoezi)

Aisee kutumia yale mavitu kama msaada wa kutembea ni mtihani sana ikiwa ulikua unauwezo wa kutembea pasi na shida yoyote na ninamshukuru Mungu nikafanikiwa kurudi katika hali yangu ya kawaida {kupona}.

Imagine mtu maisha yake yote yeye ni kutumia magongo tu kutembea mpaka umauti utakapomfika.

Mshukuru Mungu kama upo sawa na tuwaombee ndg zetu wanapitia changamoto kubwa sana.
Kwakweli tumshukuru sana Mungu,. Nasoma huku naogopa
 
Jamaa anasema anaskiaa fuuuuuuuuuuuuh alafu hasikii mkuu pole sana asee..
Ivi kidini ni kwanini vilema wanazaliwa kusudio la mungu ni nini hasa kuwapa watu ulemavu?
 
Pole sana mama, Mungu akujaalie uponyaji urudi katika hali yako ya kawaida.
 
Back
Top Bottom