Kama una mpango wa kuja South, zingatia mambo haya sita kabla ya kuanza safari yako

Kaka wewe tulia. Baada ya mwaka mmoja kuanzia sasa nchi itakuwa salama kuliko wakati mungine wowote uliopita. Waziri wa mambo ya ndani ni kaburu. Aisee huyo jamaa noma. Muulize mtu yoyote aliepo hapa akwambie kinachoendelea.

Kuna misako na operation inayofanyika nchi nzima haswa siku za weekend kuanzia ijumaa kama leo. Mkikutwa wanaume wa3 ndan ya gari au wawili lkn mpo mpo tu mnashushwa na kusachiwa nyinyi na gari lenu. Kijana ukiwa na kibegi kisichoeleweka unasimamishwa na kusachiwa. Kuna baadhi ya maeneo ya hatari kuanzia saa 2 usiku wanatembea wazee wa kuvaa kiraia. Wakikuotea unazurura zurura bila mpango hiyo imekula kwako.

Wale wahamiaji haram, wauza madawa na wahalifu wengine wote kwa sasa wanaishi matumbo joto.
 
South Africa ili kuukomesha uhalifu wangefanya operation km aliyofanya raisi wa el Salvador ...inatakiwa wapige msako nchi nzima kukamata wahalifu halafu wanapelekwa kambi maalum yenye mchakamchaka kama jeshini wakaw huko hata miaka mitano wakifundishwa stadi mbalimbali za ufundi wakirudi mtaani watumie ujuzi wao kujiajiri.
 
Kuna group la mabaharia(Sailsman) Facebook admin ni MSANGI. Aisee .........kilasiku MAITI zinatangazwa. Wengi ni bomba au madawa. Inamaana South Africa Kuna Watanzania wengi kuliko Tanzania?
Wahuni nnya wakiona Msangi anawachana na kuwasaidia wanammaind utasikia" anachoresha kiwanja " huyo anayesema anachoreshwa kachoka kuliko kichaaa wa kwenye madampo ya bongo basi tu
 
Mkuu unajua kila uongozi una stahili yake ya kutawala. Lakini vilevile hiyo style unayosema haiwezi kuwa dawa ya moja kwa moja ya tatizo, ila itasaidia tu kupunguza uhalifu uliokuwepo au uliopo.

Nasema hivyo kwa sababu hata hizo nchi ambazo unazitolea mfano, watu walikuwa wanauwawa kila siku lakini bado watu wanaendelea kuingiza na kuuza madawa. Yani serikali inanyonga hawa kesho wanaibuka wengine, mpaka Marekani, Ulaya na watu wa haki za binadam wakaamua kuingilia kati baada ya kuona kuwa njia inayotumika haimalizi tatizo, sema tu inaongeza vifo vya watu kila siku.

Na hapa mkaburu anaweza kufanya zaidi ya hayo uliyosema. Nafikiri unafaham vizuri historia ya makaburu kwa watu weusi, lakin sasa serikali haipo kwenye mikono yao. Na pia sheria zilizopo sasa haziruhusu hayo kufanyika. Ila hata hivyo kinachofanyika sasa nakuhakikishia kuwa kinaenda kupunguza uhalifu kwa kiasi kikubwa, kwani msako uliopo sasa hivi sio wa kitoto na jamaa hana hata miezi mitatu ndan ya ofisi.

Kuna watu watapotezwa kimya kimya bila raia uraiani kujua kinachoendelea. We subiri tu mkuu.
 
Chief isijekuwa ni nguvu ya soda!! Binafsi south africa ni nchi ambayo ningependa sana kuitembelea ila suala la uhalifu huwa linaniogopesha sana
 
Chief isijekuwa ni nguvu ya soda!! Binafsi south africa ni nchi ambayo ningependa sana kuitembelea ila suala la uhalifu huwa linaniogopesha sana
Kwa hawa weupe wa hapa nnavyowajua mkuu, hapa hakuna cha nguvu ya soda. Huu mziki utaendelea mpaka usalama utatamalaki nchi nzima.

Labda itokee huyu mweupe alieanzisha operation hizi atolewe ktk nafasi yake. Lakini kama ataendelea kuwepo, ujue miaka miwili ijayo hakuna mtu atakaekuwa anatembea hata na kiwembe mfukoni. Trust me mkuu.
 
Lol wangemuacha tuuπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ™ƒ
 
Namba sita ni kiboko πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…