Kama una mpango wa kuja South, zingatia mambo haya sita kabla ya kuanza safari yako

Kama una mpango wa kuja South, zingatia mambo haya sita kabla ya kuanza safari yako

Misambwanda kama yote kila unae muona kamzidi mwenzie Nyashi ila zina ukimwi balaa zivalie condom hata 5🤣😂na ukimwi wao mkali halafu madem wanapenda pesa sana wanajali maslahi na kaka yangu aliowa mke huko kafulia mke akasepa ila Mungu bwana dem anaumwa kansa bro ndo anahudumia kwasasa atafanyaje na mama wa mwanae.
aiseee...so huko sauz misambwanda kama yote au sio alafu nasikia huko kugegedana nje nje wala hawamaind ni full shisha nyama mitungi blanti hii mikasiiii
 
Habari zenu wanaJF wenzangu, ama baada ya salam ningependa kuendelea na mada yangu hapo chini.

Nianze kwa kusema kuwa dunia ina mengi, na kamwe hauwezi kuyajua kama haujaambiwa au kuyaona. Ndio maana waswahili wanamsemo wao unaosema "tembea uyaone". Hii haimaanishi kwamba utembee uyaone magorofa, magari au barabara, bali uone mambo mapya ambayo hapo kabla ya kutembea ulikuwa haujawahi kuyaona au kuyasikia popote.

Sasa leo ningependa nije na mada inayowatahadharisha ndugu zangu wabongo, ili kuwafungua macho na akili ya kujua yale ambayo hapo kabla walikuwa hawajayajua kuhusu South Africa, Dzonga, Afrika borwa, Afrika kusini, bondeni, Kaburu na kila jina linalotambulisha taifa hili.

Ni mambo sita tu ambayo ningependa kukutahadharisha nayo, uyazingatie kabla ya safari. Ila kama kuna mengine ya kuongezea basi wenzangu ambao wako humu pia wataongezea mengine katika comment. Na uzi wangu wa leo unajikita katika mambo yaliopo ndani ya mipaka ya South tu. Kuhusu changamoto zingine za njiani kabla ya kufika South nk, hizo sintozizungumzia kwa sasa. Maana thread za changamoto hizo zipo nyingi na mimi nishawahi kuandika moja.

Tuendelee hapo chini na yale unayotakiwa kuzingatia.

1. Hakikisha una document zote muhimu zinazohitajika safarini. Na kama uliambiwa kuwa gharama ya safari ni laki tatu, basi uandae angalau laki nne, ili moja uiweke pembeni itakusadia mbele ya safari. Kumbuka kuna dharura njiani, dola au rand kupanda nk.

2. Wakati unapanga safari, jitahidi kwanza ujue kingereza. Na kama una kichwa kizito cha kujifunza ngeli, basi upambane ujue hata salam, kuomba kitu au kuaga. South ni nchi inayoongea lugha 11. Ambapo lugha 9 ni za wenyeji na 2 za wazungu. Lakini lugha ya taifa na ambayo inapewa kipaumbele zaidi ni English.

Sasa ukijua English, hata kama hauna elimu ya maaana, uwezekano wa kupata kazi ni mkubwa ukilinganisha na wale ambao hawajui English. Ndomaana wazimbabwe wamedhibiti kazi nyingi na haswa zinazomilikiwa na wazungu, maana wao English kwao ni kama maji na mtungi, halafu wanaongea British safi kuliko waafrika wengine. Kutokujua English kumewanyima watu wengi (haswa kutoka bongo) fursa za kazi, hivyo kusababisha wengine kuamua kufanya deal hatari, halali na zisizo halali ili mradi mtu aishi.

3. Kabla ya kuanza safari hakikisha una address au contacts za wenyeji wako zaidi ya mmoja. Nchi hii kuna watu wengi wameuwawa, wameibiwa, wamekamatwa na kurudishwa nyumbani kwa sababu ya kukimbiwa au kuzimiwa simu na wenyeji wao kabla ya kuingia au baada ya kuingia South. Na hii sio kwa wabongo tu, bali ni nchi zote za East Africa watu wana tabia za kuwaingiza maboya ndugu, jamaa na marafiki zao kwamba waje tu watawapokea na kuwafanyia mpango wa kuishi, lakini ndugu, jamaa au marafiki hao wanapoingia tu mwenyeji huzima simu, hubadili namba nk. Hivyo ukiwa na address au namba za sim zaidi ya 3, itakusaidia ku deal na mwingine baada ya mmoja au wawili wa mwanzo kukuzimia simu.

4. Usiwaze kwamba utafanya kazi fulani tu, bali wewe ujiandae kufanya kazi yoyote (ya halali) kujiingizia kipato. Hili swala la watu kuja huku wakiandaa akili, na saikolojia zao za kichwa kwamba anakuja kufanya kazi fulani tu. Ndio limesababisha baadhi ya wabongo kupoteza mwelekeo wa maisha, na kujikuta wanajitupa katika biashara hatari na zisizokuwa halali.

5. Usilete usela mavi usiokuwa na maana. Vijana wengi waliotaka kuleta usela wa Mbagala, Mburahati, Manzese, Temeke, Tandika nk tumewazika wakiwa bado wadogo. Hii ni kwa sababu huku watu hawana muda wa kukimbizana na mwizi wajichoshe. Ukileta usela mavi, watu wanakutafutia target, wanafumua ubongo, kazi imekwisha. yumbani watu wanarudisha nguo au maiti na kesi hamna. Pia usije kwa lengo la kutafuta na kufanya starehe kupitiliza mpaka ukasahau kilichokuleta. Maana kama starehe hata bongo zipo na umeziacha, kama mademu bongo wapo na umewaacha, kama tungi pia bongo lipo umeliacha. So focus kwa kile kilichokufanya utafute nauli uje. Sio kuendekeza kulewa na chupi za Kaburu utapotea mazima na hakuna mtu atakaekurudisha katika chanel yako tena.

6. Ukifika hapa kama wewe ni mpya usikimbilie kukaa kiti cha mbele katika daladala (tax), hata kama imejaa na imebaki siti moja ya mbele, ni bora usubiri nyingine alafu ndio upande. Hii ni kwa sababu huku majimbo mengi daladala zao hakuna kondakta anaezunguka ndani ya daladala kuomba nauli. So ukisema unakimbilia mbele kukaa na dereva, utashangaa watu wanakusanya hela zote huko nyuma, alaf wanakutupia wewe ndio uhesabu na kama kuna mtu ametoa hela kubwa umrudishie chenji, na ikiwa pungufu uhakikishe waliokupa wanazieneza. Dereva yeye hupokea nauli ambayo imeshahesabiwa tayari na iwe imetimia. Ikipungua hata sh hamsini basi ataanza na wewe uliepokea hela kabla ya kuendelea na waliopo ndani ya gari. Pia asilimia kubwa ya madereva wa hapa wana silaha mbali mbali ndani ya gari zao, kama sio bunduki basi fimbo inayofanana na mkia wa taa. So hela yake isipoenea na wewe ndo New comer (mpya) haujui lugha, basi imekula kwako. Hata ujitetee kwa English yako ya kuunga unga hatokuelewa. Naomba niishie hapa.
Hii ya daladala ndo nasikia naona ingenilamba 😁nilikuwa napanda Taxify na Uber.
 
Misambwanda kama yote kila unae muona kamzidi mwenzie Nyashi ila zina ukimwi balaa zivalie condom hata 5🤣😂na ukimwi wao mkali halafu madem wanapenda pesa sana wanajali maslahi na kaka yangu aliowa mke huko kafulia mke akasepa ila Mungu bwana dem anaumwa kansa bro ndo anahudumia kwasasa atafanyaje na mama wa mwanae.
Da brother wako ashapoteza channel tayari. Ila ndugu zake bado mnanafasi ya kumrudisha tena online.
 
Duuu wastani wa.watu 500 kwa wiki?????? Ni wengi mno
Hali ni mbaya. Lakin kwa sasa kuna safisha safisha inaendelea kila jimbo. Nina imani mpaka mwakani uhalifu utakuwa umepungua kwa kiasi kikubwa sana.

Waziri wa mambo ya ndan wa sasa ni mkaburu, hivyo jamaa hataki mchezo kabisa. Wezi na watu wasiokuwa na vibali washaanza kukimbia nchi mmoja mmoja bila hata kukimbizwa 😂😂😂
 
Misambwanda kama yote kila unae muona kamzidi mwenzie Nyashi ila zina ukimwi balaa zivalie condom hata 5🤣😂na ukimwi wao mkali halafu madem wanapenda pesa sana wanajali maslahi na kaka yangu aliowa mke huko kafulia mke akasepa ila Mungu bwana dem anaumwa kansa bro ndo anahudumia kwasasa atafanyaje na mama wa mwanae.
Mie na condom dnt mix. Ngoma tayari ninayo so wala hamna shida kama wao wana ngoma. Tutakuwa tunamix tuu ya sauz na ya tz ili ipatikane breed mpya.
Suala la hela ata bongo wanalenda hela maana ukitongoza tuu, kodi imeisha, mara bday inakuja keshokutwa so in general all livings this with two legs and mbususu inbetween wanapenda hela.
 
Uzi huu umenikumbusha mbali sana way back.

Nimeshuka OR TAMBO chap natoka nje nakutana na wabongo wanaongea kiswahili pale tukawakataa. Mana tayar nilikuwa na mentality kuwa wabongo wa kule wengi miyeyusho

Tunaenda kuchukua tax ili tuende Station pale tunaona polisi wanatuzuia tusichukue ile tax eti sio salama na badala yake wakatuelekeza tax nyingine.

Tumepanda ile tax rasmi ya airport ndio dereva akawa anatuambia hizo tax bubu wengi majambazi wanakuambia bei rahisi ili ukubali mkifika njiani anakuambia hela kubwa kama Huna anakutolea mguu wa kuku na kukupora ulichonacho na anakuacha njiani...

Nikajisemea kichwani hii Africa bado ni bara la giza yan mtu yupo tayar kukudhuru ili apate tu hela akanywe pombe na kustarehe na wanawake

The first time kumuona mzungu omba omba ni South aiseee nimekaa nakula msosi mixer kuku kwa rand 25 tu naona mzungu anakuja kachoka kama katoka mbagala kibonde maji

'Anasema can we share a plate my friend?

Doh.
 
Hali ni mbaya. Lakin kwa sasa kuna safisha safisha inaendelea kila jimbo. Nina imani mpaka mwakani uhalifu utakuwa umepungua kwa kiasi kikubwa sana.

Waziri wa mambo ya ndan wa sasa ni mkaburu, hivyo jamaa hataki mchezo kabisa. Wezi na watu wasiokuwa na vibali washaanza kukimbia nchi mmoja mmoja bila hata kukimbizwa 😂😂😂
Kama ni hivyo safi sana...👌
 
Back
Top Bottom