Kama una ndoto ya kwenda Ulaya, Marekani, Canada n.k, pitia uzi huu

Kama una ndoto ya kwenda Ulaya, Marekani, Canada n.k, pitia uzi huu

Hhaaha sio kila aliyoko ughaibuni maisha yake yako poa mwngine anaogopa kukudanganya.

Na hawakatishi tamaa Ila wanajarbu kuwaambia ukwel halisi wa maisha yao Ila kwa wãbongo ni ngumu kuamini
Sawa mkuu
 
Maajenti ngumu kupatikana mkuu nimejalibu sana na wengine wanakutaka ulipie kwanza hata job hujapata unaambiwa ulipe kwanza 2500$ sasa Mimi nitaitoa wapi? Kwa kumbukumbu zangu sizani hata baba alishawahi kuzishika mkupuo Leo unaniambia nitoe ili nipate job .inauma na kusikitisha lkn hakuna kukata tamaa
Siku ukidanganywa na ukalipia ndo mwisho wa mawasiliano
 
Shida wabongo ambao wako huko ukiwatafuta shida wanakatisha tamaa sana kwahyo inakuwa ngumu kupata rafiki wa kweli na watu wa huko ndo shida kupatikana
Siongelei marafiki wa Ki bongo, ni ujinga uliopitiliza friendliest yako ya Facebook ni watu wa mtaani kwako au watu uliosoma nao tu.

Tafuta exposure hata marafiki unaoadd Facebook.
 
Wakuu naona waganda wanaondoka sana kiwanja kwa kusingizia mashoga na wanaikimbia nchi yao kwa kusakwa na serikali ya museven naona hiyo ni fursa pia kwa upande wa wasafiri kafiri ukifika mambele unajilipua tu kwamba wewe shoga na unatoka uganda, utapewa mwanasheria, na hifadhi kwa kuhudumia kwa mwaka mzima Chakula, Hifadhi tena Sehemu classic kabisa then kesi ikienda poa unapewa ukaadhi maisha yanaendelea fanya chao chap wazeeee
Tafadhali naomba unieleweshe zaidi kuhusu hii mbinu na mimi nataka,
Natakiwa kwenda Uganda au wapi ili kuclaim ukimbizi na je natakiwa kujifanya Mganda ili waweze kunipokea?

Msaada zaidi tafadhali
 
Kaka acha kabisa, Maisha ya Ulaya ni ya upweke wa balaa kwa mtu aliyetoka Africa, huwezi kwenda ka jirani wala sehemu kwamba nikale nipige soga na watu, Pesa sio kila kitu ila ukiwa na furaha ndio kila kitu.

Nilikua nawaza home mpaka nakonda, chakula nacho magumumashi hakina ladha, miezi 3 ya mwanzo nilipata tabu sana aisee.

saivi nakata mitaa kama sina akili nzuri
Tatizo letu watz huwa ni wazuri sana kwenye kukoment kama hivi,ila tukiombwa connections tunakimbia.
 
Tafuta ujuzi /fani hakikisha una "skills set" watu wengi wanaishi sio kwasababu tu wana degree bali wamebobea kwenye ujuzi fulani na wanategeneza pesa vizuri tu.
Mkuu sisi wenye fani za mikono kama kunyoa hatuna fursa za canada?maana nina bajet nzuri tu yakunifikisha canada ila connections tu ndio sina.
 
Nchi zote ulizotaja watu wake wanajanaza USA kila leo wewe huiweki US namba moja how?

Wabongo wanaosoma kimombo hadi chuo kikuu na bado kinawashinda leo unataka waende SK ambako hawajui hata salam zao!

Mtu yeyote anayetaka kwenda nje should first shoot for the stars (USA) if they fail ndo waende huko vichochoroni huko. There's a reason US ni superpower.

Aidha SK haina wageni wengi sio sababu ya its geographical location bali hawana utamaduni wa kujichanganya na wageni. This is also true kwa Japan. Watu wanaenda Greenland huko ndo iwe Sk tu hapo? Ukienda SK jiandae kwa maisha ya kipweke na box tu.
Uzuri wa South Korea
Kazi ni nyingi na malipo ni mazuri.
Watu wa kule ni very appreciative kwa kazi unazowafanyia.

Kitu nisichojua vizuri ni gharama za maisha tu.
 
Tatizo letu watz huwa ni wazuri sana kwenye kukoment kama hivi,ila tukiombwa connections tunakimbia.

Hakuna muujiza wa kufika nje bila pesa ndugu yangu

Mtu unamsaidiaje ana 3m?? 3m nauli tu haikufikishi North America.

Minimumu uwe na $25,000 hapo unaweza fika.

Conenction mtu anaweza kukusaidia ni kukuhifadhi utakapofika angalau uzoee mazingira hadi utakapopata kibarua, ukiwa nyumbani hujatoka pesa lazima iwe nayo
 
Hakuna muujiza wa kufika nje bila pesa ndugu yangu

Mtu unamsaidiaje ana 3m?? 3m nauli tu haikufikishi North America.

Minimumu uwe na $25,000 hapo unaweza fika.

Conenction mtu anaweza kukusaidia ni kukuhifadhi utakapofika angalau uzoee mazingira hadi utakapopata kibarua, ukiwa nyumbani hujatoka pesa lazima iwe nayo
Kwa nini unadanganya hadharani bila hofu? Unaijuwa $25,000/= wewe?

Ukiweza kupata $25,000/= Bongo, Marekani ukafuate nini?

Si vizuri kucoment vitu usivyovijuwa.
 

Attachments

  • Screenshot_2023-03-14-07-36-08-10.png
    Screenshot_2023-03-14-07-36-08-10.png
    31 KB · Views: 97
Kwa nini unadanganya hadharani bila hofu? Unaijuwa $25,000/= wewe?

Ukiweza kupata $25,000/= Bongo, Marekani ukafuate nini?

Si vizuri kucoment vitu usivyovijuwa.

Jitahidi uwe unasoma vitu basi mara moja moja

Canada wanahitaji uwena ada + 13,000 = $25,000

Same as to US, hiyo $25,000

Hatuhitaji maisha ya stress tunahitaji maisha ya kawaida yaliyo bora, nibora utumie $25,000 kupata maisha bora

Nimekuchagulia ndege ya bei rahisi

Screenshot_20230314_043259.jpg
 
Jitahidi uwe unasoma vitu basi mara moja moja

Canada wanahitaji uwena ada + 13,000 = $25,000

Same as to US, hiyo $25,000

Hatuhitaji maisha ya stress tunahitaji maisha ya kawaida yaliyo bora, nibora utumie $25,000 kupata maisha bora

Nimekuchagulia ndege ya bei rahisi

View attachment 2550219
Bado hujui hata ulichoandika, aliyekumezesha huu ujinga amekuingiza chaka.

Ingekuwa ni hivyo ni matajiri peke yake ndio wangekuwa wanakwenda hizo nchi.

Upo gizani hujui lolote kaa kimya.
 
Kwel maisha ughaibuni pesa ipo saanaa lakini na gharama za kuishi pia ni kubwa sana kuendana na kias unachopiga kwnye mshahara wako ,mkija pia mfahamu kwnye hizo calculation mnazopiga mjue Kuna kitu kinaitwa tax hyo kitu achana nayo hasa hasa kwa Europe unaweza kulia kwa kuiona mkwanja unavyopigwa panga lakini ndo Hali halisi

Huku tunajifunza upigaji kazi bila kuchoka na ukijisahau kuchekwa ni suala la kawaida bongo maana huku starehr ndio mahala pake .

Na pia Kuna kitu kinaitwa homesickness kwa msafiri yoyote anaitambua hii Hali muhimu ni hasira na malengo tu

Anyway kila la kheri wapambanaji nawakarbisha Stockholm, Sweden
Mchongo wake Sweden ukoje
 
Nini faida ya kupata Green Card?
Wanagharamia safari na makazi huko niendako?
Green card ni fulsa inayotolewa na serikali ya Marekani kwa mtindo wa bahati nasibu na zinatolewa nafasi 50,000 ambapo watu kutoka maeneo mbalimbali duniani wanaruhusiwa kushiriki na nadhani inakuwa mwezi October kila mwaka,ukijaaliwa kupata nafasi hiyo unapata fulsa ya kupelekwa uko wewe na wategemezi wako ambao katika fomu yako uliyoijaza umewaorodhesha na ukifika uko unapatiwa makazi,kazi na wategemezi wako nao wanaendelezwa
 
Back
Top Bottom