Kama una ndoto ya kwenda Ulaya, Marekani, Canada n.k, pitia uzi huu

Kama una ndoto ya kwenda Ulaya, Marekani, Canada n.k, pitia uzi huu

Kama watu walidhubutu kwenda mpaka kwenye sayari ya Mars bila kujali "risk" ambayo ingeweza Kuwapata na kurudi salama, si tatizo kujaribu maisha mahali ambako wanadamu wengine wanaishi.

Inawezekana hata Korea kuna American towns, pengine.
I love that spirit

Sent from my Infinix X655C using JamiiForums mobile app
 
Salamu kwenu nyote.

Kikwetu tunasema, “ndege asiyeruka hawezi kujua wapi ulezi umekomaa”.
Leo ninapenda kuwapa ABC za namna ya kufika nchi za wenzetu kwa wale wenye ndoto za kubadili mazingira ya Tanzania na kwenda nje kutafuta.

Binafsi nimeishi nchi kadhaa za wenzetu kwa vipindi tofauti na kwa sababu tofauti. Nimeishi UK(3yrs), Italy(3yrs), Spain(1yr), UAE(1.5yr). Lakini pia nimefanya kazi za mda mfupi katika nchi anuai kama Germany, France, Portugal na Austria. Nimetembelea pia nchi nyingi, Europa, Middle East, Far East(S. Korea), USA na visiwa vya St. Lucia.

Katika uzi huu nitakupeni nchi chache ambazo ni nzuri kutoboa kama ukifika, nitakupeni mbinu za kufika huko na nitakupeni shughuli za kuweza kufanya kama ukifika huko.

Hapa chini nimekuwekea nchi kadhaa ambazo ni tija sana kwa mtu ambaye anawaza kwenda nje. Nchi nzuri kiutafutaji, usalama na wepesi wa maisha.

1. South Korea. Nchi hii kama mtu ana ndoto ya kwenda nje kutafuta maisha basi nafasi ya kwanza kuwaza na Kusini mwa Korea.
-Nchi hii nimeiweka nafasi ya kwanza kwa sababu zifuatazo
1. Nchi yenye viwanda vingi
2. Uchumi wake ni mzuri sana
3. Uhaba wa nguvu kazi shauri ya jeografia yake
4. Malipo mazuri kwa wafanyakazi
5. Nchi salama kuishi na ubaguzi siyo mkubwa
6. Rahisi sana kupata kazi/Lazima kupata kazi
South Korea ni nchi ambayo kwa jeografia yake ipo mbali sana na “labour zone countries” ambazo ni bara lote la Africa, India, Bangladesh, Pakistan, Srilanka na Latin America.
Uhamiaji katika nchi hii ni mdogo sana ukikinganisha na nchi za Ulaya, USA na Canada
Malipo kwa kazi nyingi za nguvu yaani non professional jobs au manual works ni kuanzia $50/hr.
Changamoto; namna ya kuingia katika nchi hii. Zipo namna mbili au tatu za kukusaidia kufika Korea Kusini ambazo ni
A. Uende kama mwanafunzi- hapa utahitaji kupata udhamini wa kimasomo, na student visa. Kama bado upo shule au chuo unaweza kujaribu bahati yako

B. Uende kama mtalii- hapa itakupasa kuwa na tourist visa ambapo utatakiwa ku prove uwezo wako kiuchumi kama kweli unaweza ku afford kwenda na kurudi na kulipia gharama za accomodation ukiwa katika ardhi ya Korea; uthibitisho huu utautoa katika embassy ya Korea kusini nchini Tanzania.

C. Uende kama mkimbizi- hii ndo njia rahisi ambayo nimeona watu kadhaa wanautumia na imewasaidia kufanikisha ndoto zao kuingia ktk nchi hii ya Korea. Katika njia hii mkimbizi utatakiwa uombe hifadhi ktk nchi ya Korea kwa kutoa sababu ya kukimbia nchi yako. Wachache niwajuao wamewahi kutoa sababu za kiusalama kwamba wanawindwa ktk jamii kutokana na sexual orientation zao. Lakini hao niwajuao wote ni straight hivyo njia hii imetumika kiujanja tu. Hapa sintaingia ndani sana kuepusha maswali lakini binafsi nakubaliana na Machiavelli anaposema “la fine si giustifica il mezzo” yaani “the end justifies the means”.

Kazi za kufanya: kutokana na wingi wa viwanda na uhaba wa nguvu kazi kuna kazi nyingi za kufanya kwenye viwanda, supermarkets, car wash n.k. Kazi zote malipo ni mazuri sana.

NB: LUGHA KTK TAIFA HILI NI CHANGAMOTO KWANI WACHACHE WANAONGEA KI ELIZABETH

2. Canada. Hii nchi ndo namba mbili kufikiria kama kweli mtu unafikira ya kwenda nje kusaka tonge. Lugha mbili zinatumika sana ktk nchi hii; KiElizabeth na Kifransa.

Canada nayo kama ilivyo Korea Kusini, ina uchumi mzuri, pesa ina thamani, ubaguzi hakuna, wakimbizi wachache, fursa bado zipo, nchi salama na gharama ya maisha ktk miji mingi ipo chini sana.

Ajira bado ni nyingi sana kwa profesional personales na non professionals. Kuna shughuli nyingi za kutunza wazee, mashambani, viwandani, usafi n.k.

Namna ya kufika katika nchi hii.

Kwenda Canada ni rahisi nadhani kuliko kwenda nchi nyingine yoyote ile duniani. Wepesi wa kufika Canada unatokana na ukweli kwamba hii nchi inatoa nafasi nyingi kwa watu wanaopenda kwenda kusoma katika taifa hili.

Ni rahisi sana kama mtu unaweza kupata kiasi kidogo cha pesa cha kufanya maombi ya kujiunga na chuo kikuu chochote kinachopokea international students. Hapa ni lazima ujue programs na courses ambazo ni rahisi kupata nafasi ambapo nyingi sana ni zile zinazohusiana na Elimu Ahera. Ukishapata nafasi utatumiwa documents za kuprocess visa, kisha utakata ticket na kutinga Toronto au Vancouver. Simple sana.

Lakini pia unaweza kwenda kama tourist na kishafika kule unaprocess visa ya kuishi na kufanya kazi Canada.

Kwa leo naishia hapa kwanza, nitaendela na kuangazia mataifa ya USA, Germany na UAE.

“La Aquila non capit muscas”.


:::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::::

SEHEMU YA PILI.

Namna kufika Germany na UAE na shughuli za kufanya.

Germany- Kwanza kwa asiyefahamu, Ujerumani ni nchi inayoongozwa na maneno ya Paulo Mtume aliyowaandikia Wathesalonike katika barua ya 2; 3:10. “Asiyefanya kazi na asile”.
Ukiwa Germany ni mwiko kuishi bila kufanyakazi yoyote. Sijui kama sera imeshabadilika lakini wakati naenda kupiga kazi wakati wa kiangazi, ilikuwa mhamiaji akikamatwa anazurula....anakamatwa na kupewa kazi yoyote ili ale chakula kwa kukifanyia kazi. Kuombaomba na kupewa bure katika nchi hii ni dhambi. Napendekeza mtu kwenda katika nchi hii kwani kupata kazi ni rahisi.
Kwa Ulaya au nje ya nchi hakuna kitu cha muhimu Kama kuwa na kazi. Hii ndo sababu nashauri sana kuangalia nchi ambazo itakuwa rahisi kupata kazi.
-Namna ya kufika Germany. Nchi hii ni mojawapo ya nchi zinazounda Umoja wa Ulaya(European Union).
-Kwa hiyo ukiweza kupenya mojawapo ya taifa linalounda umoja huu basi inakuwa rahisi sana kuingia Germany.
-Unaweza kwenda kama mtalii wa nchi mojawapo ya taifa la EU kisha ukazamia Germany kusaka sega la asali.
NB: Ukikamatwa Germany na passport lazima urudishwe nchini mwako mara moja kwa gharama zao. Sera hii ipo pia Switzerland and Netherlands.
-Kwa hiyo cha kufanya, ukifika nenda Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani, wapatie passport yako halafu utakapoamua kurejea nchini tena itakubidi kuifuata ubalozini.
-Germany pia inatoa nafasi za masomo kwa hiyo unaweza kujaribu bahati yako kuomba udhamini.
-Kiingereza kinaongelewa lakini ukifahamu Kijerumani utakuwa katika nafasi nzuri sana.
(Nakumbuka namna nilivyopata chance ya kuwa naenda kupiga kazi Germany, ni baada ya siku moja kuwa na mazungumzo na Mjerumani mmoja ambaye alikuwa ni visiting lecturer chuoni kwetu. Aliponiuliza natokea wapi nikamjibu Tanzania halafu nikaongezea, moja ya nchi iliyotawaliwa na babu yako...nilifanya hivyo in an amazing casual way kiasi kwamba aliniona mtu cheerful nisiye na resentments. Tulitokea kuwa mabest sana na hata kuwa ananifanyia michongo ya kazi zenye malipo matamu).
Mwisho ukiwa Ujerumani-fanya kosa lolote lakini siyo kuchelewa chelewa. Uchelewaji ni kitu Mjerumani hawezi kuvumilia. “Be obedient to Kantian punctuality”.

UAE [emoji1256] (United Arab Emirates)
Kwa asiyefahamu, unaposema [emoji1256] una maanisha muunganiko wa vinchi saba ambavyo makao makuu yake yapo Abu Dhabi. Kiongozi Mkuu pia yupo Abu Dhabi huku msaidizi wake akiishi Dubai.
Abu Dhabi ndiyo imeshikilia uchumi mkubwa kwa sasa ikifuatiwa na Dubai kisha Sharjah.
Umoja huu, mbali na Abu Dhabi, Dubai na Sharjah, unajumuisha pia Ajman, Umm Al Quwain, Fujairah na Ras Al Khaimah.
-Wale vijana wa Ilala wanaofuata spea za magari Dubai, chimbo lao lipo Sharjah.

Namna ya kufika- Wepesi wa kufika Dubai ni kwamba kama unatokea Tanzania unaweza kwenda bila visa na ukakata visa on arrival. Kwa maana hii Mtanzania yeyote anaweza kutinga Dubai bila shida yoyote.
-Unaweza kwenda kama mtalii kwa kukata visa ya miezi3 au 6 na kishafika kule ukaprocess working na resident permit. Visa hii utahitajika kukata ticket mbili yaani go and return lakini kwa sasa technology itakusaidia kwa kukata ticket moja ya go na return unaweza kupata “DUMMY TICKET”.
-Pamoja na kuwa [emoji1256] una vinchi saba, binafsi napendekeza Dubai kwa sababu zifuatazo;
  • Mchanganyiko wa watu wa mataifa mengi
  • Ni mji ambao ni very westernized
  • Uchumi ni mzuri na kazi bado zipo japo competition ni kubwa sana kutokana na kuzungukwa na labor-zone states yaani Africa, India, Pakistan, Afghanistan, Srilanka, Bangladesh, Lebanon, n.k.
  • Gharama ya maisha ipo chini sana ukilinganisha na nchi nyingi zilizoendelea
  • Thamani ya pesa ni nzuri sana (1AED=630Tsh)
  • Ni karibu sana hivyo panafikika(nauli inafika hadi chini ya laki5 za Kitanzania)
  • Ni rahisi sana kutuma pesa nyumbani kutokea Dubai
  • Kuna sehemu za kuabudi za wahindi ambapo wanatoa breakfast, lunch na dinner bure kabisa hivyo kwa mzamiaji unaweza kuishi kwa kuvizia mlo sehemu hizo.
Ukiwa Dubai unaweza kufanya kazi za kuajiliwa kama vile Ulinzi, Usafi, Ujenzi n.k au unaweza kujiajili mwenyewe kwa kufanya shughuli zifuatazo
Unaweza kuingia mjini kati yaani Deira City Centre na ukapiga kazi ya kupakia na mizigo kwenye magari.
Unaweza kufanya kazi ya kusukuma toroli la mizigo katikati ya mji hasa hasa Deira
Unaweza pia kujiajili kuuza nguo, mikoba ya wanawake, Viatu nk, ambapo itakubidi ujue machimbo ya wachina unapoweza kupata mzigo kwa bei nafuu...sehemu kama Baniyan Square shughuli hii inapigwa sana na waafrica.
Kuna wa Wabongo wengi pia maeneo kama Etisalat wanapiga shughuli ya kuuza mishikaki, vitumbua nk.
Kama wewe ni risk taker unaweza pia kupiga deal la kuuza pombe; kikubwa ni kujua chimbo la kupata mzigo zaidi Sharjah na sehemu ya kuuzia. Hii kazi inalipa sana.

Mwisho kwa mtu anayewaza kutoka nje ya nchi Dubai ni sehemu ya kufikiria kuanzia kabla ya kuwaza kwenda kuishi katika taifa kubwa kama [emoji631].
Maisha ya Dubai na Bongo binafsi sikuuona utofauti mkubwa sana.

Next time nitakuelezeeni namna ya kufika USA na naamini kila mtu anapenda sana. Kwa kila mwaka huwa nasaidia walau watu 2 kufika USA na huu ni mwaka wa 3 nafanya hivyo.

“Aquila non capit muscas”
So kusoma Canada hauhitaji kupata scholarship ili uweze kusoma au kupewa visa ya kusoma huko?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna hawa mawakala wa ajira nje ya nchi recent nmeona wana kaz kwa wadada huko UAE na wanasema wanakulipia usafir uwe tu na passport je hili la kupokonywa passport ukifika lina ukwel.
 
Kuna hawa mawakala wa ajira nje ya nchi recent nmeona wana kaz kwa wadada huko UAE na wanasema wanakulipia usafir uwe tu na passport je hili la kupokonywa passport ukifika lina ukwel.
Yaaap ina ukweli
Sikutishi ila niliwahi sikia story moja ivi mdada alitafutiwa kazi na alivo fika hio nchi alinyanganywa passport na kazi alio ambiwa ilikuwa sio.... Yeye alitumikishwa kingono...
 
Ingekuwa unachosema ni kweli Lema asingepata asylum seeker akiwa Nairobi.

Canada wanachelewa tu kutowa viza, application zako wanakaa nazo muda mrefu lakini wakikupa viza imetoka hiyo.

Mpaka Sasa Canada ndio nchi inayohitaji watu zaidi, na kilichowasaidia kutoingiliwa na wabinjukaji wengi Jirani yake ni Marekani, kwahiyo ukitaka kubinjuka Canada upitie Marekani kitu ambacho hakipo au wale mabeach boy wanaoungia kwa meli.
Usijifananishe na Lema yeye ni politian anajulikana wewe saga jiwe nani anakujua
 
Wewe ulikuwa nje ya wapi hiyo ya upweke wakati watu mbefele wanaruka madebe daily..usitujaze ujinga mabaharia
Kaka acha kabisa, Maisha ya Ulaya ni ya upweke wa balaa kwa mtu aliyetoka Africa, huwezi kwenda ka jirani wala sehemu kwamba nikale nipige soga na watu, Pesa sio kila kitu ila ukiwa na furaha ndio kila kitu.

Nilikua nawaza home mpaka nakonda, chakula nacho magumumashi hakina ladha, miezi 3 ya mwanzo nilipata tabu sana aisee.

saivi nakata mitaa kama sina akili nzuri
 
Vancouver, Toronto na Ottawa ni mji expensive sana sio housing rent tu hata car insurance ni expensive diaspora wengi wa kutoka africa wanapenda show off waonekane wanaishi miji mikubwa ila deep down wanaumia
Je mji wa Montreal vipi?
 
Sasahivi Ulaya kumejaa Wahamiaji wa nchi zenye VITA mpaka wenyeji wameanza kuwachukia Wahamiaji. Nchi nyingi za Ulaya kwa sasa zinaangalia namna gani ya kudhibiti wimbi la wahamiaji na kuweka masharti magumu zaidi. Kuna baadhi ya nchi zimeanza kujadili kwenye mabunge yao namna ya kudhibiti hadi Wanafunzi wanaoingia Ulaya kwa ajili ya masomo.

Kutokana na wingi wa wahamiaji, kuna baadhi ya nchi za Ulaya Magharibi (kunakodhaniwa ndiko kwenye Ustaarabu zaidi) vijana wahamiaji wameanza tabia za kukaba watu kama ilivyo Panya Road kwa Bongo. Wenyeji wanachukizwa sana na hii tabia ya watu wa wakuja na kuwaharibia Ustaarabu wao.

Vyama vinavyounga mkono masuala ya kuleta wahamiaji vimeanzwa kupigwa chini na vinaingia vilivyo na mtizamo hasi dhidi ya wahamiaji. Maisha ya Ulaya kwa sasa yameanza kuwa magumu na upatikanaji wa vibarua umeanza kuwa adimu. Yote kwa yote bado Ulaya huwezi linganisha na Afrika.

Watu wangeenda Katavi kulima au pale Uvinza kuchimba hata chumvi kuliko hizi habari za kukimbilia Ulaya Amerika.
Inabidi vijana wajifunze kuipenda nchi yao na kujituma
 
Watu wangeenda Katavi kulima au pale Uvinza kuchimba hata chumvi kuliko hizi habari za kukimbilia Ulaya Amerika.
Inabidi vijana wajifunze kuipenda nchi yao na kujituma

Acheni kuwadanganya vijana Mbona ninyi watu wazima mmeshindwa kuendesha bandari hadi mnaamua kuiuza. Acheni unafiki mtu akipata fursa popote aende, dunia ni yetu sote.
 
Acheni kuwadanganya vijana Mbona ninyi watu wazima mmeshindwa kuendesha bandari hadi mnaamua kuiuza. Acheni unafiki mtu akipata fursa popote aende, dunia ni yetu sote.
Una point lakini hata nyumbani kuna fursa pia na inawezekana ni kubwa kuliko nchi za watu, hata mimi ningependa vijana wasafiri ili wakirudi wawe na akili zaidi, nchi zilizoendelea kuna mengi ya kujifunza
 
Back
Top Bottom