Jebel
JF-Expert Member
- Jul 10, 2021
- 386
- 2,615
- Thread starter
- #521
Una point lakini hata nyumbani kuna fursa pia na inawezekana ni kubwa kuliko nchi za watu, hata mimi ningependa vijana wasafiri ili wakirudi wawe na akili zaidi, nchi zilizoendelea kuna mengi ya kujifunza
Siwezi kukupinga lakini mkuu hembu nijibu kwa hili;
Mimi nimeenda nchi za watu nikajichanga hadi nikapata mtaji, mwaka jana nikarudi nyumbani Tanzania kuwekeza, mwaka huu nimeamua kujikita kwenye biashara ya mazao(mahindi) nikachukua mzigo wa 50M nikapeleka Uganda. Kufika tu mpakani mara mpuuzi mmoja akaropoka kufunga mipaka bila kutoa notice in advance. Huwezi amini nimekata 6M kwenye mzigo huo.
Je, bado unaweza kutetea hoja yako ya kuwepo kwa fursa nyingi Tanzania je? Mimi naona kama vikwazo ni vingi kuliko support kwa nchi yetu.