Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Kama una stress pitia hapa, usiache kutupia na wewe maneno yako

Mtumishi wa MUNGU mmoja akiwa kwenye gari alisimamishwa na Trafic Police,police akiwa anahitaji rushwa alianza kuuliza maswali mengi, mara mbona gari lako linatoa moshi mwingi? mbona gari lako matairi yameisha, hatimaye polisi akamuamuru padre waende nae kituoni. Njiani polisi alimuuliza , umesema wewe ni Mtumishi wa MUNGU, je unabiblia ndani ya gari, akajibu ndio ninayo, polisi akamuambia , pack ...gari pembeni na unipe biblia. Mtumishi akapaki gari na kumpa biblia yule polisi,Polisi akasita kupokea, akamwambia Mtumishi 'fungua na usome Mathayo 5:25-26 "Mtu wa Mungu akasoma ": "Patana na Mshtaki wako upesi,wakati uwapo pamoja naye njiani: yule mshtaki asijekukupeleka kwa kadhi na kadhi akakupeleka kwa askari,ukatupwa gerezani. " Amin nakuambia,Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho" Mtu wa Mungu akampa yaliyo yake kaizari. Polisi akatabasamu na kusema 'msifanye migumu mioyo yenu".. Enenda kwa amani
 
Bibi alienda kupiga Xray, Doctor akamwambia moyo umetoboka katikati na pembeni umevimba pande mbili. Bibi akasema we mtoto wewe nadhani umechanganya negative ya picha ya mtu alipiga matako yake? Nenda kalete ya kwangu
 
Mzee mmoja aliwakataza vijana kuvuta bangi karibu na nyumba yake,Wavuta bangi wakaamua kumwamisha huyo mzee na nyumba yake,kwanza wakavuta bangi ya kutosha wakavua mashati wakaanza kusukuma ile nyumba, kibaka akapitia yale mashati, mmoja wao alivyogeuka nyuma hakuyaona akajua wameshafika mbali akawaambia wenzie tukazane tumefika mbali hata nguo zetu hazionekani wakaendelea mpaka bange zilivyoyeyuka kchwani wakaona wako palepale.
 
Leo Kwenye Basi Kuna Wadada Wawili Walikua Wanagombaniana Seat Moja, Dereva Kwa Hasira akasema "Mwenye sura mbaya ndo akalie hiyo Seat" Yani mpaka tunafika Wote Wawili Walikua Wamesimama. Kuna Madereva Wana Hekima Kama Mfalme Solomon 😀😂😂```
 
Bibi alienda kupiga Xray, Doctor akamwambia moyo umetoboka katikati na pembeni umevimba pande mbili. Bibi akasema we mtoto wewe nadhani umechanganya negative ya picha ya mtu alipiga matako yake? Nenda kalete ya kwangu
[emoji3]
 
Mzee kaingia pharmacy,

MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa

MFAMASIA: Kitu gani?….Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka …majimaji yaliyomo kwenye kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;

MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au chumvi au pilipili?

MFAMASIA: Kama chumvichumvi

MZEE: Hakuna sukari

MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa

MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano nashukuru sana, dokta alinambia nipime mkojo wangu kama nina kisukari, kumbe sina asante bwana mdogo
 
Jamaa kaenda kumtembelea rafiki yake Levi, kule sehemu za kwetu, akakaribishwa bonge ya ugali na nyama nyingi tu, wakati anakula akagundua kuwa shemeji yake, mke wa rafiki yake hali nyama; JAMAA: Aise hili ni bonge ya lanchi hii, lakini Levi mbona sisi tu tunakula nyama shemeji Gulo hagusi kabisa anaishia mchicha tu? Tabia gani hii? LEVI: Hapana sijamkataza, ila shemeji yako Mngoni halagi nyama ya FISI kama sisi JAMAA AKAZIMIA HAPOHAPO
 
Jamaa kaamka asubuhi sana Jumamosi, mvua inanyesha kang'ang'ania kuwa anaenda ofisini. Kawasha gari yake, kufika njiani hali ilikuwa mbaya kaamua kurudi. Kafika home kavua nguo kaingia tena kitandani, kamnong'oneza mkewe aliyekuwa usingizini; "Yaani hali ya hewa huko nje mbaya sana" Mke: Si ndio nimemshangaa huyu mpumbavu eti kaenda kazini...
 
Back
Top Bottom