Labda ungeainisha ni aina ipi ya Mafanikio unayoyazungumzia. Being Successful it's a perspective statement/ Word. Kila mtu anatafsiri mafanikio yake kutokana na imani yake au desire. Mafanikio hayana Universal meaning...Je kwa mujibu wa mada yako unazungumzia Mafanikio yapi?
-Ndugu zangu Ma-Budha wanaamini Mafanikio ni kufikia Vast spiritual Enlightenment wao wanaita Nirvana
-Kwetu Stoics na Cynics tunaamini mafanikio ni kufanikiwa kutojishikiza katika materials au aina yoyote ya Emotions.
-Wakatoliki tunaamini Mafanikio ni kufa kifo cha utakatifu ili uweze kufika mbele za Bwana.
-Ndugu zangu wachaga wanaamini Mafanikio ni kua na pesa miiiingi sana
Mtoa mada unazungumzia Mafanikio Tangible au non tangible... Spiritualphysical au mentally?
Karibu mkuu,
Mimi ni Mstoa na ninaamini mafanikio ni kufikia uwezo mkubwa ulio ndani yangu na kuiishi misingi mikuu minne ya ustoa ambayo ni;
1. Hekima (wisdom)
Kwa kujifunza yaliyo sahihi na kuyaweka kwenye maisha yangu ili yawe bora zaidi na yawe na manufaa kwa wengine.
2. Haki (justice)
Kuwatendea wengine yaliyo ya haki na kuwa na uadilifu.
3. Ujasiri (courage)
Kuweza kusimamia kilicho sahihi bila kuhofia chochote.
4. Kujidhibiti (moderation)
Kuwa na kiasi kwa kila jambo.
Tofauti ya Ustoa na falsafa nyingine ni ustoa haukuwekei ukomo wa nini unaweza kuwa nacho au huwezi kuwa nacho.
Unaweza kuona Epictetus alitoka kuwa mtumwa mpaka mwalimu wa Falsafa.
Seneca alikuwa tajiri mkubwa wa Roma.
Na Marcus Aurelius alikuwa mtawala wa Roma.
Hivyo kupitia Ustoa, mafanikio ni kuijua asili yako na kuishi kulingana na asili hiyo.
Na hiyo pia ndiyo maana rahisi ya mafanikio kwa yeyote, jua unachotaka sana na pambana kukipata.
Na siyo kuhangaika kuridhisha wengine.