Makirita Amani
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,915
- 3,422
- Thread starter
- #61
Umeelewa vizuri sana mkuu,Mtego mkubwa wa huu uzi uko kwenye hiyo namba ya simu na KISIMA CHA MAARIFA full stop
Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Karibu sana tufanye kazi pamoja.
Na wala hakuna ninachofanya hapa, nimeahirikisha tabia hizo kumi za kuachana nazo, ambazo ukizifanyia kazi, utaona matokeo ya tofuati.
Ila kama huwezi kufanyia kazi mwenyewe, kama unataka watu wa kushirikiana nao, kama unataka mwongozo basi karibu kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
Hiyo ni jamii ya tofauti kabisa na inayokuzunguka.
Sababu pekee ya kuweka hili hapa najua kuna mtu amekwama mahali, amejaribu kupambana kwa namna nyingi lakini hatoboi, lakini mtu huyo akipata mwongozo sahihi, anaweza kupiga hatua.
Kuna mtu alikutana na makala yangu hapa Jamii forums miaka ya nyuma, akaendelea kunifuatilia, akaja kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA na mpaka sasa amepiga hatua sana.
Ni shuhuda za aina hiyo zinanisukuma kushirikisha maarifa haya hapa mara moja moja ili kuwafikia wale ambao wamekuwa wakitafuta njia sahihi ya kupiga hatua kwenye maisha yako.
Najua wengi hapa ni changamsha genge tu, mmekuwa mnapinga haya tanu nimeanza kupost maarifa haya ya mafanikio hapa jamii forums mwaka 2013, lakini hilo halinisumbui sana, wale wachache wenye uhitaji kweli wamekuwa wanachukua hatua na matokeo wanayaona.
Hivyo kama kuna ambaye nafsi yake imemgusa kwamba hapa kuna jawabu la yale unayopitia, sikuambii hata ujifunze na KISIMA CHA MAARIFA ambapo kuna ada ya kulipa.
Nakuambia tembelea www.amkamtanzania.com kila siku bure kabisa, jifunze, chukua hatua na utapata matokeo mazuri sana.
Kwa kifupi sitaki upoteze fedha yako kwa kununua hata kitabu changu kabla hujajaribu yale ninayotoa bure na yakaonesha manufaa kwako.
Karibuni sana wote.