Kama una tabia hizi 10, huwezi kamwe kufanikiwa kwenye maisha

Hata mimi nilitaka kuuliza hivyo hivyo. Tunapojadili mafanikio, tunaongelea nini hasa? Katika muktadha wa Kitanzania ni mpaka uwe tajiri wa aina gani ndiyo uhesabike umefanikiwa?
Mafanikio ni kupata unachotaka na maisha yako kuwa bora mkuu.
Asikudanganye yeyote nje ya hapo.
 
Tajiri anauzaga vitabu jamiiforums?
Mnanishangazaga sana mnapowadharau watu wanaouza vitu.
Hii dunia inaendeshwa na sales people.
Heshimuni sana watu wanaofanya sales, hata kama ni ya kiwango kidogo kiasi gani.
Hata wagunduzi wakubwa wa teknolojia, zimeweza kuwafikia watu baada ya kuuza.
Usidharau kuuza mkuu.
 
Asante kwa maelezo, uwe na wakati mwema.......
 
Nikushauri tu ndugu, kwenye uandishi jaribu kuzungumzia vitu kiuhalisia, usizungumzie nadharia. Hayo uliyoyaandika hapo kila siku yanazungumzwa na motivational speakers hakuna kipya hapo.

Na usipo badilika utapata tabu sana.

Sent from my SM-J701F using JamiiForums mobile app
 
Ukisoma comments za huu Uzi ndio utajua IQ ya watanzania kwanini iko chini sana.

Kama mtu anashindwa ku-logic na kuwa analytical kwa hizo hoja kumi (10) anaenda kuhoji utajiri wa mleta mada na kuuza vitabu !!! Basi sishangai tunapata Viongozi wanaenda kujenga international airport Chato.


Ili uamini IQ ya watanzania Ni ndogo nimechukua huu Uzi nikamtupia rafik yangu mkoja mkenya Feedback ambazo kanipa ni tofauti na yanayoandikwa humu.


Watanzania tutahidi kuwa analytical. Simaaninishi ni lazima ukabaliane na Uzi ila kuwa na critics zilizojiegemeza kwenye hoja na sio mtu. Kuelekeza critics kwa mtu badala ya hoja hizo 10 ni moja ya dalili uwezo wetu wa kujenga hoja ni mdogo.

Haya ndio Mambo hata kwenye interview allkisimama mtanzania na mkenya tunaishia kuduwaa.
 
Mchokozi sana wewe 😂😂😂.
 
Wewe kwa hizi akili ndio maana ulitimuliwa kwenu huna tofauti na mifugo


 
Karibu mkuu,
Mimi ni Mstoa na ninaamini mafanikio ni kufikia uwezo mkubwa ulio ndani yangu na kuiishi misingi mikuu minne ya ustoa ambayo ni;
1. Hekima (wisdom)
Kwa kujifunza yaliyo sahihi na kuyaweka kwenye maisha yangu ili yawe bora zaidi na yawe na manufaa kwa wengine.
2. Haki (justice)
Kuwatendea wengine yaliyo ya haki na kuwa na uadilifu.
3. Ujasiri (courage)
Kuweza kusimamia kilicho sahihi bila kuhofia chochote.
4. Kujidhibiti (moderation)
Kuwa na kiasi kwa kila jambo.
Tofauti ya Ustoa na falsafa nyingine ni ustoa haukuwekei ukomo wa nini unaweza kuwa nacho au huwezi kuwa nacho.
Unaweza kuona Epictetus alitoka kuwa mtumwa mpaka mwalimu wa Falsafa.
Seneca alikuwa tajiri mkubwa wa Roma.
Na Marcus Aurelius alikuwa mtawala wa Roma.
Hivyo kupitia Ustoa, mafanikio ni kuijua asili yako na kuishi kulingana na asili hiyo.

Na hiyo pia ndiyo maana rahisi ya mafanikio kwa yeyote, jua unachotaka sana na pambana kukipata.
Na siyo kuhangaika kuridhisha wengine.
 
Hyu jamaa ni tajiri kwa level za kibongobongo hasa kwa vijana, namjua tokea anaanza harakati zake.na ana miradi tofauti tofauti sio kuuza vitabu pekee yake

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mkuu uzi wako umeelewek vizuri tu ...hapy kwenye kusoma au kujifunza ndo inakuwa kipengele kwa wengi kusoma tunasoma ila mara nyingi udaku ndo unapendwa sana be blessed tukutan kweny watsap..
 
Umenifumbua macho kwa kiasi fulani ila mwishoni hapo ni kama ulikua unaniandaa kwa ajili ya hivo vitabu ulivotaja...japo BIG thanks tutayafanyia kazi.
 
Ndio wabongo tulio wengi tulivyo. Negativity imeshakuwa part ya maisha yetu, tena wengine wana heshima kubwa humu jamvini lakini utopolo wanaouandika kwenye huu uzi huwezi kudhania.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Kwani ilikuwa ni nyumba ya mama yako ndugu???



Sent from my SM-J701F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…