Kama una zaidi ya watoto wanne, na unaishi mjini, kuna ushauri wenu hapa

Tulipokwepa kulima ndipo tukachagua maisha haya ya kulipia bili za kilimo. Pesa nyingi huenda kwenye chakula.

Shida ni moja, kwa vijijini wanawake wanashiriki kwa 100% katika uzalishaji wa hayo mazao ya kilimo na wanaume zao so maisha yanakuwa sio mzigo kwa upande m'moja. Ila huku mjini, mwanaume ndie bread winner kwa 100% ndio maana ndoa zinavunjika siku hizi maana wameshtuka kuwa wanageuzwa punda wakati mwanamke anachopata ni nadra sana kuchangia pato la familia (sio wote).
 
Kuna wakati unakutana na mzee barabarani amepigwa na jua la utosi, huku akiongea mwenyewe; kumbe changamoto anatakiwa familia ipate mkate wa kila siku
 
Umeandika kama ni rahisi vile !!!
 
ushauri mzuri ila hapo pa 70 per day mhh kuna utata familia za kawaida chai haizidi hata 2000 sasa huo chai ya 20k ni chai ya mifupa ya watu ama. kuwa realistic kwenye makadirio yakohyo mtu kama anakata 2m kwenye msosi analipwa bei gani? na unapozungumzia kula vizur unamaana gani kwakua hata ukihitaj mlo kamili kwa familia hiyo bado hutazidi 15k kwa mlo mmoja
 
Familia ya mjini inayokunywa chai ya 2000 lazima watoto wadumae akili.
 
Daaaah aiseee na hizi tozo hao watoto wanne si utaongea peke yako njia nzima.
 
Kuna kitu, wanaita 'standard breakfast', achana na hii ya kujaza matumbo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…