Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Watu wengi wanapopatwa na shida, magonjwa na majanga, huamua kufunga na kuomba kwa muda mrefu, wakitarajia kuwa Mungu atawatatulia shida zao. Jambo wasilolijua wengi ni kwamba ili Mungu atupatie haja zetu tunapomuomba, ni lazima tukidhi vigezo na masharti aliyoyaweka.
Kama unafanya mambo yafuatayo, hata ukifunga na kuomba kwa siku 7, siku 21 au siku 40, unapoteza muda wako tu, Mungu hawezi kukupa unayotaka:
1. Kama una dhambi moyoni na hutaki kutubu
Zaburi 66:18
"Kama ningaliwaza maovu moyoni mwangu, Bwana asingesikia.”
2. Kama matendo yako ni ya dhambi
Isaya 1:15-17
“Mnapoinua mikono yenu kuomba nitauficha uso wangu nisiwaone. Hata mkiomba kwa wingi sitawasikia...”
3. Kama una uhusiano mbaya na mume au mke wako
1 Petro 3:7
“... ili maombi yenu yasizuiliwe.”
Mwanandoa asiyemheshimu mwenzake, maombi yake yanazuiliwa.
4. Kama unafunga na kuomba ili watu wakuone na kukusifu
Mathayo 6:5-6
“Usiwe kama wanafiki... kwa maana wamekwisha kupata thawabu yao.”
5. Kama hutaki kujinyenyekeza na kuacha njia zako mbaya
2 Mambo ya Nyakati 7:14
“... watu wangu, wakijinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.”
6. Kama unadharau Neno la Mungu na hutaki kulitii
Methali 28:9
“Yeye azibaye sikio lake asisikie sheria, hata sala yake ni chukizo.”
Maombi ya mtu asiyejali Neno la Mungu hayakubaliki.
7. Kama unaomba kwa ajili ya tamaa zako binafsi
Yakobo 4:3
“Mnaomba wala hampati, kwa sababu mnaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.”
8. Kama unawaonea maskini
Mithali 21:13
"Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, yeye naye atalia, lakini hatasikiwa..”
9. Kama huombi kwa Jina la Yesu, unapoteza muda wako bure.
Yn 14:13-14
"Nanyi mkiomba lo lote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana..."
Ili tupate majibu ya maombi yetu, ni lazima tuombe kwa Jina la Yesu tu.
10. Kama huyatendi maagizo yote ya Mungu
Luka 6:46-49
"Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, lakini hamyatendi nisemayo?"