Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

Ina maana watu wanakula kitimoto daily
 
mkuu hongera sana, mimi nimeweka m 3 tu kila ofisi, na nimefanya hivyo kwa sababu nina laini binafsi za float, wakipata mteja wananishtua fasta nawatumia salio. Halafu pia eneo nilipo ni rahisi sana kupata cash au float, mawakala tunasaidiana, pia mawakala wakuu wapo, unawapigia wanakutumia fasta
 
hv mawakala huwa mnakabiliana vp na hawa matapeli mfano mtu anakuja kudeposit pesa afu anakupa noti feki (unatumia njia gan kutambua noti feki)
na pia kuna wale matapeli wanakuja wanakutumia sms kiujanja kwamba wamewithdraw kumbe hamna ktu, pasipo kujua ww unawapa hela wanasepa badae kuangalia salio unakuta hamna ktu
 

Mkuu naomba umfundishe mdogo wangu hii kazi ya kutengeneza simu . Nicheki 0757786054
 
kwa aliyefanya hii biashara mikoani atupe uzoefu wakuu
popote inalipa

ukianza angalia tu sijui hii biashara ni ya sehemu flani tu "tayari una feli"

Biashara ni nini?

Biashara ni kuangalia jamii ina tatizo gani kisha unaenda watatulia kwa njia ya wao kutoa pesa

so

ukienda kufanya biashara hii mkoani sitegemei kukuona umeenda tengeneza matoroli halafu ukaenda yaweka

sehemu zenye kazi official..unapoamua fanya hiii biashara kwanza utambue Toroli halibebi mtu,toroli linabeba

Mizigo inaweza kuwa mbao/matofali/mizigo ya sokoni/maji ya kuuza/nk nk

Ukishajua kazi ya hilo toroli lako nadhani mkoa wowote unaweza peleka matoroli na ukapiga pesa.

USHAURI

jitahidi uanze na zaidi ya vi toroli vi 6 kwenda mbele,sio chini ya hapo

Toroli 1 ni hela yako ya kula kwa siku then vitoroli hivi vi 5 ni hela ya kuweka
 
Shukrani mkuu, acha tukomae tu maana serikalini kwenyewe tumeajiriwa mishahara haikutani. Hakuna namna.
 
Kwa kawaida ukishazioea noti, ikipita bandia mikononi mwako haushindwi itambua. Ukiingalia hologram iliyopo ktk noti inatosha kuitambua. Hao wezi wengine mara nyingi kama umekiuka misingi ya kazi hii. Huwa tunafundisha wakishazoea ni nadra sana kuibiwa. The last time kuibiwa ni February 2017, TSh 800k, ila ulikuwa ni ushirika wa mfanyakazi wangu na rafiki yake wa nje walishirikiana.
 
sawa sawa.
 
Nishawahi kufanya deep conversation na two most successful businessmen, mmoja ana sheri za Mafuta na maroli mwengne anamaduka ya hardware na anamaroli, pia nmetoka kuhitim elimu ya utawala biashara, hivo matumizi ya imani hayaingiliani kabisa na issue za location na changamoto zingne, in short uchawi kwenye business upo
 
Mkuu vitambulisho vya machinga vinapatikana wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…