Kama unaomba hivi, imani yako itashuka na utamchoka Mungu mapema

Noma sana!
 
Mara nyingi Sala zangu huwa si ndefu ila Nina Imani na Mungu Kuna saa anawahi kujibu mpaka nashangaa....Kuna point of no return niliwahi fika nikamwambia Mzee Baba ehhh Mimi nimechoka na siendi Kwa waganga wewe ndie Kila kitu changu Mungu Bora unichukue au ujibu hitaji langu.....aisee sijawahi omboleza hivyo mbele za Mungu......Asubuhi Mungu akanijibu Kwa kishindo kikuu....Mungu yupo jaman....
 
Kwa sababu Mungu ni muweza wa yote na kila jambo alishakupangia , na pia yeye habadiliki na anajua kila kitu kabla haujazaliwa,hakuna haja ya kuomba tena ili mambo yako yabadilike , wewe sema tu Mungu fanya kama unavyotaka inatosha.
 
Ubarikiwe sana mtumishi
 
Sijawahi hata siku moja kulalamika kwenye sala zangu. Huwa nashukuru kwa afya, uzima, riziki na huwa nawaombea familia yangu Mungu awalinde na awatimizie mahitaji yao kwa kadri wanayostahili. Na hatua inayofuata huwa naomba ulinzi wake wakati wote na baada ya hapo huwa naomba mahitaji yangu baada ya hapo namshukuru kwa kunipa nafasi ya kuzungumza nae kwa njia ya maombi na dua, 🙏

Note : Hakuna kitu chenye thamani kushinda uhai na afya tulizonazo hayo mengine huwa yanampata mwengine kwa kudra zake tu.
 
Amen, amen. Kuna mtu anawasalisha hiyo sala ya Bwana mara saba kwa kuirudia halafu ndio imetoka hiyo.
 
Zamaniiii nikiwa mtoto mdogo nilifikiri Kuomba kwa jina la Yesu ni lazima kusema katika jina la Yesu kumbe....[emoji1787]
 
Zamaniiii nikiwa mtoto mdogo nilifikiri Kuomba kwa jina la Yesu ni lazima kusema kusema katika jina la Yesu kumbe....[emoji1787]
Jina linawakilisha mamlaka. Ni sawa upewe ofa ya kutumia Jina na cheo cha rais wa Jamuhuri popote utakapokwenda.

Jila la Yesu ambalo mamlaka zote ziko chini yake, tumepewa kulitumia kana kwamba yeye mwenyewe ndio yupo hapo.
 
Amen, amen. Kuna mtu anawasalisha hiyo sala ya Bwana mara saba kwa kuirudia halafu ndio imetoka hiyo.
Ile ni kama ukurasa wa Yaliyomo, au Skeleton. Kisha kila kipengere kinatakiwa kigeuzwe kama a
Chapter katika maombi.

Ila hata hivyo ukifanya kama huyo jamaa kwa imani, mambo yanajipa.
 


Amri ya Kwanza kabisa ubaoni!

'I am God Almighty your God, you shall have no other gods before me!'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…