Kama unaomba hivi, imani yako itashuka na utamchoka Mungu mapema

Maombi ni moja ya njia ya kuondoa wasiwasi na kuongeza imani katikati ya changamoto na sintofahamu za maisha.

Lakini kama hujui kuomba vizuri unaweza kujikuta yanakuongezea stress, wasiwasi, hata kushusha imani yako kwa Mungu. Na hii imepelekea watu kucheza miguu miwili. Mmoja kwa Mungu mwingine kwenye utamaduni kificho.

Kosa liko wapi.
Unapoanza maombi unaanza kwa kutanguliza shida na masumbufu yako badala ya kutanguliza ukuu na uweza wa huyo Mungu kwanza.

Tumia muda mwingi katika utangulizi kumtambua Mungu, uweza wake, ukuu wake sifa zake na utukufu wake. Hii itakufanya akilini mwako uone Ukuu wa Mungu na katatizo kanafifia hata kabla hujakataja. Ukifika wakati wa kueleza unachotaka basi unakuwa na uhakika na huyo unayemuomba maana unajua akilini fika anauwezo gani.

Kutanguliza kuvurumisha matatizo yako kama kipaumbele, unayakuza kuliko uwezo wa Mungu akilini mwako. Hivyo unamkuza shetani na uwezo wake kwako Kuliko Mungu. Unampa nafasi kubwa kuliko Mungu. Hivyo maombi ya kumbrand shetani na uwezo wake huwa yanaarika majini badala ya malaika. Yanajaza hofu, mashaka na wasiwasi.

Mfano wa hili fundisho ni story ya Mfalme Yehoshafat 2Nyakati 20. Namna walivyoanza maombi ni kwa kumtambua Mungu na uweza wake kisha wakamsakizia matatizo yao. MUNGU ALIINGILIA KATI KWA KASI YA AJABU.

HII NDIO MAANA YESU ALIFUNDISHA TUANZA KUOMBA KWA KUSEMA " BABA YETU ULIYE MBINGUNI, JINA LAKO LITUKUZWE, UFALME WAKO UJE".
Hii ni kama flame work wewe hapo unatakiwa kujaza maneno mengi kwenye hii sentensi ya Yesu.

Ni hayo tu.

Kama umepata kitu, sema amina.
Ndugu sijakuelewa.....
Unazungumzia sala au maombi?
 
Me huwa na smoke ka weed kdg mida ya sa7 hvi alafu naanza kubonga na Mungu kimnyakmnya.
 
Amina..

Kuna nguvu kubwa kwenye maombi ya kumtukuza na kumshukuru Mungu...

Kama Sala ya Baba Yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe...
 
Maombi ni moja ya njia ya kuondoa wasiwasi na kuongeza imani katikati ya changamoto na sintofahamu za maisha.

Lakini kama hujui kuomba vizuri unaweza kujikuta yanakuongezea stress, wasiwasi, hata kushusha imani yako kwa Mungu. Na hii imepelekea watu kucheza miguu miwili. Mmoja kwa Mungu mwingine kwenye utamaduni kificho.

Kosa liko wapi.
Unapoanza maombi unaanza kwa kutanguliza shida na masumbufu yako badala ya kutanguliza ukuu na uweza wa huyo Mungu kwanza.

Tumia muda mwingi katika utangulizi kumtambua Mungu, uweza wake, ukuu wake sifa zake na utukufu wake. Hii itakufanya akilini mwako uone Ukuu wa Mungu na katatizo kanafifia hata kabla hujakataja. Ukifika wakati wa kueleza unachotaka basi unakuwa na uhakika na huyo unayemuomba maana unajua akilini fika anauwezo gani.

Kutanguliza kuvurumisha matatizo yako kama kipaumbele, unayakuza kuliko uwezo wa Mungu akilini mwako. Hivyo unamkuza shetani na uwezo wake kwako Kuliko Mungu. Unampa nafasi kubwa kuliko Mungu. Hivyo maombi ya kumbrand shetani na uwezo wake huwa yanaarika majini badala ya malaika. Yanajaza hofu, mashaka na wasiwasi.

Mfano wa hili fundisho ni story ya Mfalme Yehoshafat 2Nyakati 20. Namna walivyoanza maombi ni kwa kumtambua Mungu na uweza wake kisha wakamsakizia matatizo yao. MUNGU ALIINGILIA KATI KWA KASI YA AJABU.

HII NDIO MAANA YESU ALIFUNDISHA TUANZA KUOMBA KWA KUSEMA " BABA YETU ULIYE MBINGUNI, JINA LAKO LITUKUZWE, UFALME WAKO UJE".
Hii ni kama flame work wewe hapo unatakiwa kujaza maneno mengi kwenye hii sentensi ya Yesu.

Ni hayo tu.

Kama umepata kitu, sema amina.
Uko sahihi,hata kwenye mahusiano ya kawaida mwanamke aktanguliza njaa anachosha,ndio maana chawa husifia mabwana zao hadharani ili wapate kura yao
 
Hautakiwi kumuomba Mungu,, Mungu ni wakuabudiwa na kushukuriwa Tu!!
 
Unatupanga tu kisaikolojia.

Hii kitu umeongea kuhusu ukweli wa maombi ni utetezi wa wanao lazimisha uamini kwenye maombi. Just in case ukishindwa kupata utakacho usikimbie kwenye imani yao. Ni 'fall back plan' tu ya wajanja.

Yanatokea kama yalivyo takiwa yatokee labda kwa uzembe wako au kutokujua kwako kanuni flani za mafanikio sababu ya mustakabali wako (destiny) au sababu ya Ile mnasema ulivyo pangiwa (na Asili /nature au Mungu) yaanii ilikuwa lazima iwe hivyo kutokana na urithi wa vinasaba au urithi wa laana za kifamilia (family curse) n.k.

Kwa hivyo ikiwa sababu destiny, fate au urithi hakika nakuambia utasali kwa mtindo wowote na nguvu zote hakitabadilika kitu isipokuwa utabadilika wewe kwa kukubali matokeo ya kuwa hutopata ukitakacho unaishi nalo hitaji/tatizo lako au utachanganikiwa (frustrated) kwa kuona hujasikilizwa na Mungu.

Destiny au 'fate' lazima itokee na ndiyo maana ikifika muda wa kifo hata uombe vipi utakufa au unaye mwombea asife atakufa tu. Wamekufa manabii, mitume na wanaojiita watumumishi wa Mungu akina T.B. Joshua, Mama G.Rwakatare n.k.

Ukitaka uishi kwa raha bila hofu uishi falsafa ya stoicism, ukiwa stoic hutateseka na maombi.
 
Amina, na asante kwa ufafanuzi mzuri. Nina swali moja mkuu; nimekuwa nikifuatilia ibada na maombi sehemu (madhehebu) mbalimbali, sasa katika kuomba, watu wanaingiza maneno kama "tunakubariki na tunakutukuza ee Mungu wa mbinguni".

Je, ni sahihi kusema, "tunakubariki ee Mungu wetu", ili hali sisi ni viumbe (waumbwa) wake? Maombi (kama neno lenyewe lilivyo), ni kwamba, mwenye shida ndiye anayeomba, hivyo, pamoja na mambo mengine, tunamuomba Mungu atushushie baraka, sasa inakuwaje tena sisi wahitaji wa baraka tutoe kitu ambacho hatuna (maana tunaiomba hiyo baraka)?

Hili nalitafsiri kama mtu maskini anayekwenda kutoa msaada kwa tajiri, hivi mtu mwenye mshahara (wa mwezi) wa shs 700,000/= anaweza kwenda kumpa msaada Elon Musk aongezee mtaji kwenye biashara zake?
 
Asante.
Neno kubariki kama misamiati mingine lina maana zaidi ya moja.
Moja ya maana ya neno kubariki ni kumsema mtu/kitu vizuri ( Speak well of something).

Pia hata mimi mwanzoni ilinisumbua hadi nilipogundua wanaosema hivyo wako sahihi maana kuna mafungu mengi katika Zaburi yanazungumzia kumbariki Mungu au Jina lake. Au pengine wametafsiri kama Kumuhimidi. Kuhimidi =Kubariki.

Hivyo haimaanishi kumpa vitu Mungu au kitoa msaada Mungu bali ni kumsema Mungu vizuri, na kumkubali.

Na hapa utajifunza hata wewe ukiwasema watu vibaya au ukawapiga majungu ni kuwalaani. Ukiwasema vizuri na kuwatamkia maneno chanya unawabariki.
 
Unatupanga tu kisaikolojia.

Hii kitu umeongea kuhusu ukweli wa maombi ni utetezi wa wanao lazimisha uamini kwenye maombi. Just in case ukishindwa kupata utakacho usikimbie kwenye imani yao. Ni 'fall back plan' tu ya wajanja.

Yanatokea kama yalivyo takiwa yatokee labda kwa uzembe wako au kutokujua kwako kanuni flani za mafanikio sababu ya mustakabali wako (destiny) au sababu ya Ile mnasema ulivyo pangiwa (na Asili /nature au Mungu) yaanii ilikuwa lazima iwe hivyo kutokana na urithi wa vinasaba au urithi wa laana za kifamilia (family curse) n.k.

Kwa hivyo ikiwa sababu destiny, fate au urithi hakika nakuambia utasali kwa mtindo wowote na nguvu zote hakitabadilika kitu isipokuwa utabadilika wewe kwa kukubali matokeo ya kuwa hutopata ukitakacho unaishi nalo hitaji/tatizo lako au utachanganikiwa (frustrated) kwa kuona hujasikilizwa na Mungu.

Destiny au 'fate' lazima itokee na ndiyo maana ikifika muda wa kifo hata uombe vipi utakufa au unaye mwombea asife atakufa tu. Wamekufa manabii, mitume na wanaojiita watumumishi wa Mungu akina T.B. Joshua, Mama G.Rwakatare n.k.

Ukitaka uishi kwa raha bila hofu uishi falsafa ya stoicism, ukiwa stoic hutateseka na maombi.
Hizo falsafa za kibinadamu zitakufanya uendelee kuwa inferior being. Maana unakabizi akili zako kwa mwanadamu na utunzi wake ambao umeongozwa na finite being.

Mfano unasema mambo ya laana ya ukoo. Sisi tunasema ukiwa umempokea Yesu na mtiifu kwa maagizo yake, unakuwa mtoto wa Mungu na kuwa mwanafamilia ya kifalme, Familia ya Mungu. Hakuna laana, laana unawaachia wanaozipenda na wanafalsafa.

Hii inakubadilishia maana ya maombi. Sio kutaka vitu kwa Mungu ni mazungumzo na baba yako mfalme wa wafalme. Historia takatifu inaonyesha hivyo vifilosofi vya stoic & co vinapoishia ndio sisi tunapoanzia.
 
Hautakiwi kumuomba Mungu,, Mungu ni wakuabudiwa na kushukuriwa Tu!!
Ombeni nanyi mtapewa.
Kuomba ni sehemu ya kuabudu.

Nanyi mkiwa katika kusali salini hivi...
Utupe leo riziki zetu.
 
Back
Top Bottom