Kama unasafiri Kilometa zaidi ya 800 kwa basi wewe ni masikini tafuta hela

Nauli ya ndege haiwezi kuliwa labda uwe ndezi sana..ndege unatuma tiketi mkuu.
Demu yeyote akijifanya sijui hana nafasi kabanwa na kazi.
Fanya booking mtumie copy ya tiketi tayari nafasi imepatikana[emoji23][emoji23]
Ha ha ha ha
 
Kwa kwetu afrika usafiri wa anga bado haujafunguka ipasavyo, kupata ticket tu ya ndege kasheshe na utalipa mara 3 au 4 ya nauli husika.
Labda kwa nchi za Amerika na Ulaya ambapo unaweza pata ticket ya ndege mpaka kwa USD50.
Huku afrika nadhani mpaka kufikia 2070 itakua afadhali usafiri wa anga utafunguka mashirika yataongezeka na nategemea mpaka nauli kupungua na usafiri wa anga hautokua anasa tena.
Lakini kwa wakati huu kama mtu ndio unajitafuta bado hujajipata endelea kutumia tu bus, mpaka mambo yatakapo kunyookea.
 
Sawa tajiri😁
 

Kabisa mkuu,ila nasikia DRC wao wanatumia sana ndege kwa trip za ndani maana kuna maeneo hayafikiki kirahisi kwa bus
 
Binafsi napenda kutumia bus kuangalia mandhari ya nchi yangu
 
Ukweli mchungu,tutakupinga ila ulichokisema nikweli....bus linachosha asikwambie mtu...... niliwahi kusafiri Dar-sumbawanga daah saa 12- saa. 7 Usiku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…