Artifact Collector
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 6,617
- 10,205
Na hapo marekani ndo anapowazid maadui zake amejaza vibaraka wake kila kona European union ni kibaraka wa marekani, Korea kusin, Japan, gulf countries n.kAlichofeli Putin ni kitu kimoja tu kushindwa kuweka vibaraka kwenye uongozi wa nchi zinazomzunguka ambazo awali zilikua chini ya USSR.
Hii vita ilipaswa kupiganwa kijasusi zaidi kwa kuwaingiza madarakani viongozi watakaokubali kuwa vibaraka wake, kuliko kuingiza jeshi vitani.
Hapa Putini anaonekana ni dictator au mkoloni kwa kuilazimisha nchi nyingine yenye mamlaka kamili kufuata kile anachokitaka yeye kwa kutumia mabavu.
Hapa ndipo USA amempiga gape kubwa kwenye suala zima la ushawishi kwa kutumia vitengo vya kijasusi na propaganda kutekeleza matakwa yake.
Huwezi kuwa super power na kuicontrol dunia kwa kutegemea mabavu ya kijeshi peke yake bila ya kua na mbinu za ushawishi zitakazo kuongezea washirika watakao kua na wewe bega kwa bega kwenye ajenda zako.
Namuona Mchina ameshalishtukia hili sasa hivi, anatumia nguvu nyingi zaidi kuzishawishi nchi ziwe na ushirika na yeye.