Mbona US anaendeleza operation zake Yemen kwa kutumia kivuli Saudi Arabia na kuua raia wasio na hatia lkn mpaka mda huu dunia ipo kimya.
Ndio huwezi kuhalalisha ubaya kwa ubaya,ila tukitaka dunia iwe salama basi UN,US na EU waache unafiki, kwani wao ndio wameacha majanga makubwa kuanzia Iraq,Libya, Afghanistan nk ambapo mamilioni ya watu wamekufa na hizo nchi hazitawaliki, zimekuwa machaka ya kigaidi ambayo wanasambaza itikadi za kigaidi mpaka kwenye nchi zetu za Afrika kuna vikundi vinawatii ISIS.
Nchi kama Libya ni sawa na Jehanum iliyopo dunia,magaidi kibao, biashara ya viungo vya binadamu na vita isiyokuwa na mwisho. US anapigania haki ya Ukraine, wakati ICC wameomba uchunguzi ufanyike kwa raia 24 waliokufa Yemen (BBC Panorama),wakawawekea vikwazo wale majaji. Ila siku na saa uchunguzi ukifanyia Iraq,Libya na Afghanistan utapata picha halisi ya unyama wa kutisha kwa mamailioni ya raia waliokufa wasio na hatia na ndio maana US na washirika wake akiibuka mtu yoyote kuhoji lazima wamuwekee vikwazo.
Hivi ina mamilioni ya watu waliokufa Iraq, Afghanistan na Libya hawana thamani, vipi watoto? Haki yao wataipata lini.