Kama ushawahi kuachwa kihivi, njoo utupe mkasa

Nilipo kuwa chuo niliachwa kwa sms, nakumbuka ilikua mida ya saa12 jioni, Mara sms ikaingia, kusoma naona risala ndefu yakuachwa bila sababu yoyote, mwishoni anaandika eti usichukue maamuzi mabaya. Nilicheka moyonj nikasema huyu hanijui Mimi. Basi sikuwaambia hata room mates wangu, nilichofanya nilibeba madesa yangu nakuelekea seminar rooms kusoma, nikasema nikienda library naweza kuonana nae. Room mates walienda library, akawafata nakuwauliza , mbona mmemwa cha mwenzenu peke yake je ! akifanya jambo baya la kujidhuru?, wakamuuliza kwani kafanya nini? akajibu nimemwacha. Wakabaki wanashangaa , wakamwabia mbona hayupo room ameenda kusoma, alivyo sikia vile hakuamini ilibidi anitafute , ahakikishe, alinikuta napiga kitabu na niko norm. Akabaki anashangaa, tukapiga story mbili tatu, wala sikumgusia kuhusu kiniacha. Yaani nilikua na hasira moyoni, na hasira yangu iliishia kwenye kitabu, nahivi tulikua tunajiandaa na UE. Matokeo yalipo toka nilipiga balaa kuliko mitihani yote, yeye akapata sup 3, wale wenzangu nao wakawa na sup za kutosha. Alipoona matokeo yangu hakuamini, akanipigia na kusema hakufikiria kama nitafaulu vile alijua nitadisco .Tukabakia marafiki tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alilenga kukufelisha mpuuzi huyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
Kwa hiyo kugegeda uliendelea....safi sana
 
Hafai hata kuws rafiki yako
 
Aise huyo mwanamke ni fala sana, alikuwa na nia mbaya uharibikiwe!
Huyo asipokuja kuwa mchawi lazima atakuwa mganga wa kienyeji anawapigia watu ramli chonganishi.
Safi sana Mzee kwa kukamua vizuri!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana kaka
 
Danadana zilianza kwa kunikwepa kuonana,ukafika muda akachoka kunikwepa siku moja nikamuuliza (kwa sms)kwani D kama mapenzi yangu na wewe yameisha si uniambie tu maana hujawahi kunizungusha kwenye appointment namna hii.
Akajibu "Merua tatizo umechelewa kujua mbona mimi nilishakuacha zamaaani"

Nilirudia kusoma kama mara tano hivi,haikuwa rahisi kuamini maana mahusiano yalikuwa na miaka mitatu yakiwa kwenye level ya juu sana,yalishuka kama mwezi mmoja tu kumbe ndani ya huo mwezi ndiyo alikuwa ameshaniacha tayari bila mimi kujua.

Nikakaa wiki nzima bila kumtafuta wiki ya pili nikasikia anatoka na don mmoja pale mtaani,basi nikaamua kufuta namba na kila aina ya mawasiliano,na maisha yakaendelea nilienda mkoa wa mbali kiutafutaji,nakuja kurudi baada ya miaka miwili alishaolewa na huyo don third wife maana jamaa alikuwa na wake wawili yeye akawa wa tatu,
Kwa sasa ana watoto watatu na mimi nina miaka mitano kwenye ndoa,sijawahi kumchukia kwa uamzi wake kwa kuwa aliangalia maslahi ya maisha yake pengine na future yake,maana mimi kwa kipindi hicho nilikuwa bado najipanga pengine aliona namchelewesha.
Kuachana siyo uadui.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangawizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ntakufikiria kilichonitoaa kwako ni uongo kama umejirekebisha ntakufikiria
Sent using Jamii Forums mobile app
 
subamiiti mjifunzage na kuacha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
uache uongo na umbea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo alikuwa shetani aise kwa hiyo alitaka u disco manina walahi ulikuwa una date na jini mahaba

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nasikia we jamaa kwa fix kiboko


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…