Kama Wakenya wameweza, sisi tunashindwa kwenda kujifunza kwao?

Kipindi gani hicho mkuu? Mimi ninachofahamu ni kuwa Waisraeli ndiyo waliokuwa wakiwasaidia Watanzania kujenga scheme ya umwagiliaji.

Walikuja kujifunza au walikuja kujitolea kufundisha?
Baada ya kujifunza kwetu mkuu fuatilia historia vizuri na kuna kiongozi alienda hko alipofika aliambiwa mbona wataalam wote wametoka Tanzania kipindi cha kikwete alienda nje akakuta wakuu wengi wa mashirika wanatoka Tanzania akiwemo professor musa asadi na Omar nundu na wengine wengi akawaahidi warudi nyumbani atawapa nafasi kubwa kwenye serikali yake kuna watanzania wengi tu wapo nje wanafanya vizuri ila siasa ndio inaharibu nchi yetu.
 
Elewa wazi kenya ni blockers wa mazao nafaka yote afrika mashariki kama mahindi na nk


Kingine usichokijua kwa Afrika mashariki Freeman aikael mbowe na uhuru kenyatta ndo

Wauzaji mazao mbogamboga ulaya yote kutokea Afrika mashariki na kati
Nilisikia Serikali iliiharibu bustani ya Mbowe. Kwa hiyo ni kweli alikuwa akifanya hiyo biashara, lakini ni kweli alikuwa akiuza Ulaya? Yeye aliwezaje?
 
Inawezekana siyo wachoyo mkuu ila tu umekutana na mchumi makini🀣
Tena wachumi haswa
Uchoyo wao naujua sana tuko tofauti mkuu
Mtanzania atakugawia hata karanga au mhogo
Ila wao ukienda kwao bila taarifa utakaa sitting room na gazeti utapewa, wao wanakula na hawakuiti n'goo

Kweli wako makini kwa maisha ila sio kwa roho ya hivyo
Hawana ukarimu kabisa hilo ndio tunalotofautiana nao
Naweza kuweka akiba na nikalisha watu bila kuathiri mali zangu ila kwao mwiko
 
βœ…πŸ™πŸ™πŸ™
Halafu kuna kitu kingine, wakenya wanakopeshwa sana hela nyingi na mabenki yao sanasana Equity Bank Kenya inawapa sana mikopo. Yule Ceo wa Equity Bank Kenya ni mjanja na mbunifu kufinance wafanyabiashara Kenya.
 
Mkuu, mbona mimi nawaamini sana Wakenya?.

Siamini kama kuna mtu anyeweza "kunipiga"

Anipige mimi nikiwa wapi? Kika kitu tutaifanya kwa kuzingatia kanuni, taratibu, na vigezo.
Nakuhakikishia kwa elimu yetu na uoga tuliofundishwa wabongo,usitegemee kufanana na Mkenya. Sisi wanyenyekevu waoga kwa kila kitu. Mkenya amefundishwa hata jinsi ya kuishi nje ya nchi yake. Atakupiga ktk biashara hiyo hiyo utakayomshirikisha. Sisi hatujui hata namna ya kuwa pattiner na mwingine kibiashara. Tumeweka mbele kuaminiana tu. Unamwamini mwenzio ksbb ya mazoea. Tatizo linapokuja kwenye pesa hakuna mwaminifu hapo. Ksbb utamwamini mwanzo,huko mbele mkenya anaweza kuja kukuachia manyoya
 
Si uchoyo huo mkuu, ni utamaduni wao! Watakuwa wameutoa kwa Wazungu.
 
Si uchoyo huo mkuu, ni utamaduni wao! Watakuwa wameutoa kwa Wazungu.
Haswa wazungu wako hivyo sana tu
Ila na mimi kuna wazungu huwa nawapa halafu nawaambia sharing is caring naona baadhi wanaelewa ila utaambiwa kwa mfano chakula kina nini ndani yake usije kupaliwa au hutumii
Sisi bado tuna utamaduni wa kiafrika nafikiri ni mzuri zaidi
 
Siasa! Ndiyo kusema tatizo letu kubwa ni ukosefu wa Siasa safi?
 
Tanzania pesa ipo nyingi sana tatizo uvivu wa kufikili ila pesa ipo bro miezi miwili ukoumiza kichwa wewe bilionea
 
Ni kweli, utamaduni wa Kiafrika ni mzuri zaidi. Tena, tukienda mbali zaidi, naweza nikakuambia kuwa utamaduni wa kabila letu ni mzuri zaidi kuliko la kabila lingine lolote lile.

Ila cha ajabu sasa, na Wazungu nao wanaona wa kwao ni bora kuliko wa Waafrika. Kilichopo ni kujielewa na kuwaelewa wengine. Kufanya hivyo kutatuepusha kuwalaumu wengine.
 
Nao wako sawa kwa upande wao, kwa mfano unaweza kumpa mtoto chocolate halafu kumbe ana allergies nazo akafa lawama inakuwa kwako
Ndio maana hata watoto wakienda kwa jirani hawawapi chakula mpaka wapate idhini ya wazazi kwanza

Ni vizuri pia maana wao wanaangalia yasije yakawakuta
Mambo mengi sana wanajitahidi kwa mfano mwingine hawawezi kuzika maiti mpaka ipelekwe hospitali ikafanyiwe uchunguzi hata kama amefia nyumbani kifo cha kawaida
Ni lazima akafanyiwe uchunguzi
Ila sisi utasikia tu kuna kilio kwa fulani na jioni au baada ya masiku mtu anazikwa
Na kesi za mirathi na mauwaji yapo kibao
Hebu fikiria kila maiti ikichunguzwa wangapi wataumbuka?

Hata waarabu pia wanapeleka hospitali pia ndio wanazika kwa baadhi yao
Sisi bado mengi sana ila silaumu ni maisha yetu haya ya kuzika tu hata kama mzee alinyongwa na mwanae usiku au ulipewa sumu na mkeo sawa tu
 
πŸ™πŸ™πŸ™
 
Lugha ni kisingizio.
Mbona wachina wanasoma kwa kichina na wanaongea kwa kichina, ila wanazalisha bidhaa wanauza dunia nzima? Vipi kuhusu, Japan, Korea, Uturuki?



Lugha sio sababu
Wewe na wengine mnaojifananishaga na China huwa mna akili ndogo sana... unajua hadi China kafika hapo alifikaje? Sisi twende kwa njia zetu tunazoweza kwenda nazo ikiwemo hiyo ya lugha... tutakuwa wapumbavu kujimwambafy kuwa kiswahili kinatosha huku tumeshasaini mikataba kibao na mabeberu wenye lugha yao. Kwa tulipofikia hatuwezi kuwavimbia wazungu. Twende nao kijanja
 
Sawa Mkuu
 
Wanasema mchawi mpe mwanao akulelee! Hatuwezi "kuwarubuni" Wakenya ili watupatie maujuzi yao?
Anakupaje kwanza? Maana ujinga wetu ndio mtaji wao.... Na jamaa wa binafsi Sana, kumbuka kule kunaukabila hata biashara utakua mkikuyu kwa mkikuyu na mluo kwa mluo.. Sembuse uje weye Mtanzania... Hapa ni sisi watanzania kubadili mtizamo... Tukitumia umoja wetu kuchangiana ujuzi na mtaji tungekua mbali... Tatizo roho za kila mtu kutakua awe bora zaidi na mashuhuri zimetufanya kila mtu afe kivyake... 😒😒
 
Kikwazo namba 1 ni serikali hii ya ccm

Kuna mfumo uko nchi hii wa kuwakombatia watu fulani
Mtu wa kawaida akisema aanze ataletewa zengwe mpaka basi

Unapoandika uzi huu sshv kuna wakenya nawajuwa wanakuja kununua nanasi kiwangwa

Ova
 
Serikali yao imewasimamia kuhusu upande wa ku export na hayo mambo mengine uliyosema
Sisi huku tuendele kufungua bar,watoto wakatike mauno misomisondo honey ndiyo ajira mpya

Ova
 
Serikali hii ya ccm ni waoga sana
Kuona watu wengi wakiwa na kipato kikubwa cha pesa

Ova
 
Anza na Comoro sheh

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…