Kama Wakenya wameweza, sisi tunashindwa kwenda kujifunza kwao?

Humu jf huwa nawaambiaga watu kuwa wakenya wamejipanga kuliko watu mnavyodhani. Serikali inashirikiana na sekta binafsi ili kutafuta fursa. Kuna video niliona ya hilo jengo wanalotumia kupack maparachichi kwa ubora wa kimataifa na mitambo waliyoweka humo, nilinyanyua mikono juu 🙌🏿🙌🏿🙌🏿🙌🏿.
Hapa Tanzania maparachichi ni mengi mpaka yanamwagwa, hakuna soko
Hapa Tanzania, sijui ni akili ndogo, sijui ni wivu, sijui ni roho mbaya. Yaani kuna ujinga mwingi sana unafanyika.


Hiyo ishu ya parachichi ni rahisi. Soko china, Uarabuni, ulaya, Marekani lipo. Kwani serikali isikopeshe vijana wawe na hiyo international standard facility njombe au iringa, vijana wa sua tena wamesoma mpaka wameenda mpaka Israel ila hawana kazi, Kwani benki ya kilimo kazi yake ni nini?

Ni ujinga ujinga tu unatukwamisha.
 
Acha tuu vijana wapo...wanasisitiziwa kilimo at the end hakuna soko..kumbe masoko yako mengi nje huko..dunia bado inahitaji chakula sema ndo hivyo...
 
Ni kweli kabisa
 
China Kuna soko la parachichi sanaa...
Maana china wanaingiza na wenyewe Kwa speed ya kuzalisha organic products kama mafuta,,,sijui shampoo Wana export ulaya.....yaani vitu vya asili vya kupaka,urembo...soko ni kubwa lakini wewe kama mwananch WA kawaida kutoka njombe huwezi muuzia mchina ni ngumu...
Lazima kuweka na vitu hapo katika ambalo ndo serikali yetu iingie kati .
Kama hiyo mitambo na kadhalika na kadhalika....kumbuka kwamba parachichi ni perishable goods.....,wakenya wanaweza kwasababu serikali inatoka 50% ya mchango wao..
Kuwezesha wananchi...
Kama ushafika Kenya uanaona daladala zao nyingi zimeandikwa SACCO?
Vikundi vinajiunga serikali inawawezesha wanamiliki Hadi biashara ya usafirishaji kupitia mabank..nafikiri za watu binafsi ni chache.
Kwa kifupi serikali ya Kenya ni part and parcel ya kwanini wakenya wanaofanya vizuri kimataifa na hata ndani ya nchi...very organized country
 
Tanzania bado hatuna shida, angalia jinsi tunavyoshabikia mpira wa simba na yanga. Angalia tunavyo jadili wasanii kila kukicha. Angalia Jinsi nchi yetu inavyoongozwa kishabiki yaani wananchi wanajigawa team fulani. Kenya wanajua nini maana ya shida na kupambana. Kama una biashara yako ukiajiri mkenya atapambana na kuiendeleza kila siku na takufundisha mbinu ya kutumia vizuri rasilimali zako. Wakenya wanapiga kazi vibaya sana aisee na wanajua kujituma. Sisi watanzania tukipata hela ya kubadilisha mboga na kustarehe na wanawake tunaridhika na kuweka miguu juu. Hata ukifuatilia wanasiasa walioiba hela serikalini, mafisadi wa kenya wamefungua biashara kubwa nchi mwao huku sisi mafisadi wetu wanaficha hela nje na kununua magari ya bei mbaya badala ya kutengeneza ajira.
 
Ile nchi ina uhaba wa vitu vingi. Nahisi ile hali ya ukosefu wa vitu vingi imewafanya wawe na akili na kujipanga vizuri. Sio kama sisi, nchi kubwa halafu iko tupu, ukimaliza kimara nchi iko tupu. Inakuwa kama kubwa jinga fulani hivi 🤣🤣
 
Ile nchi ina uhaba wa vitu vingi. Nahisi ile hali ya ukosefu wa vitu vingi imewafanya wawe na akili na kujipanga vizuri. Sio kama sisi, nchi kubwa halafu iko tupu, ukimaliza kimara nchi iko tupu. Inakuwa kama kubwa jinga fulani hivi 🤣🤣
Hata life style yao
Wakenya hawana mambo ya kununuliana vyakula au kupeana hela,kupigana mzinga kule wanakaushiana
Mbongo mtu anaweza amka asubuhi mpaka jioni yeye ni kupiga vizinga tu siku inaenda

Ova
 
Mkulima Milionea wa Njombe


View: https://m.youtube.com/watch?v=MKOgPfGfVjk
Serikali kuu, pia za mikoa na mitaa ziwekeze zaidi kusambaza mitandao ya wakulima wajue kuzalisha mazao bora na pia kubaini masoko yake kimataifa ili wakulima waweze kuyafikia masoko ya kimataifa zaidi ya ilivyo sasa.

Mwalimu aliyeacha kazi, na kujikita katika kilimo cha parachichi

View: https://m.youtube.com/watch?v=0F6gGmVg8As

IJUE TAHA NA KAZI ZAKE



View: https://m.youtube.com/watch?v=B-mHb-pGlcoVipindi vingi vya online vitayarishwe wakulima wapate taarifa kupitia simu zao janja za mkononi na kompyuta.

Wakulima wajitangaze kimataifa badala ya kuwa bubu katika majukwaa ya intaneti kimataifa, ikiwezekana wajifunze lugha ngeni kubwa kuweza kufikia masoko ya kimataifa.

Ikiwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanaji brand na kufikia ulimwengu vipi halmashauri za Mbinga, Wangingombe, Meru n.k hawana idara wala maofisa kilimo, biashara na ugani kuisaidia sekta ya kilimo, uvuvi na mifugo kutangazwa kimataifa kwa lugha ya kigeni kulifikia soko la kimataifa


View: https://m.youtube.com/watch?v=CMC9P9-qel4Source : TAHA ONLINE TV
 
Ile nchi ina uhaba wa vitu vingi. Nahisi ile hali ya ukosefu wa vitu vingi imewafanya wawe na akili na kujipanga vizuri. Sio kama sisi, nchi kubwa halafu iko tupu, ukimaliza kimara nchi iko tupu. Inakuwa kama kubwa jinga fulani hivi 🤣🤣
Na kweli chek kuanzia namanga mpaka karibia Nairobi Kuna ka ukame flani hivi ka mda wote...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…