Halafu maendeleo hayataki kabisa demokrasia. Huko China ukileta ujinga kama vile ufisadi adhabu ni kifo. Hawakufika hapo kienyeji kwa kupiga porojo. Watu wasijilinganishe kabisaMchina ni bonge la bepari tena
Ova
Mambo Kenya ni magumu mno. Lazima wawe wachoyo.Hata life style yao
Wakenya hawana mambo ya kununuliana vyakula au kupeana hela,kupigana mzinga kule wanakaushiana
Mbongo mtu anaweza amka asubuhi mpaka jioni yeye ni kupiga vizinga tu siku inaenda
Ova
Hii Ina thibitika beyond a reasonable doubt naunga mkono hojaππππβΊοΈβΊοΈπ€π€Hata life style yao
Wakenya hawana mambo ya kununuliana vyakula au kupeana hela,kupigana mzinga kule wanakaushiana
Mbongo mtu anaweza amka asubuhi mpaka jioni yeye ni kupiga vizinga tu siku inaenda
Ova
Eneo kubwa la Kenya ni jangwa. Sehemu nzuri iliyobakia ni mbuga za wanyama,ardhi ya vigogo, wawekezaji na eneo dogo lililobakia ndio wananchi wanaishi.Na kweli chek kuanzia namanga mpaka karibia Nairobi Kuna ka ukame flani hivi ka mda wote...
Sidhani kama ukabila unaweza kuwa kikwazo kwa Mtanzania anayetaka kwenda kufanya biashara Kenya. Kule pia kuna Wazungu, Waarabu, Wachina , Wahindi, Watanzania n.k., wanaofanya biashara huko. Mojawapo wa Watanzania waliowekeza huko ni Rostam Aziz. Hilo la ukabila wala si kikwazo kiongozi. Dhubutu kujitosa bila hofu.Anakupaje kwanza? Maana ujinga wetu ndio mtaji wao.... Na jamaa wa binafsi Sana, kumbuka kule kunaukabila hata biashara utakua mkikuyu kwa mkikuyu na mluo kwa mluo.. Sembuse uje weye Mtanzania... Hapa ni sisi watanzania kubadili mtizamo... Tukitumia umoja wetu kuchangiana ujuzi na mtaji tungekua mbali... Tatizo roho za kila mtu kutakua awe bora zaidi na mashuhuri zimetufanya kila mtu afe kivyake... π’π’
mods please mtunuku huyu jamaa tuzoInasemekana Tanzania ni chaneli ya katuni uko mbinguni
πWatanzania wengi hatuna nidhamu ya kazi. Hapo ndipo shida inaanzia
Mkuu umetishaπmods please mtunuku huyu jamaa tuzo
Ndio ni kweli ....nahisi shida imefanya Kila mtu awe na ajili..Eneo kubwa la Kenya ni jangwa. Sehemu nzuri iliyobakia ni mbuga za wanyama,ardhi ya vigogo, wawekezaji na eneo dogo lililobakia ndio wananchi wanaishi.
Kenya kuna maisha MAGUMU sana. Halafu jamaa wana ukabila promax na uchoyo wa kiwango cha lami. Kule hakuna mdau wa kukupa hata buku la maji au mama ntilie wa kukupa ukoko wa buku siku ikaisha. Hakuna cha mjomba, shangazi wala Kaka, wala Baba mdogo. Baba wenye nyumba ni wa kenya ni wakali mno waanaitwa Landlord, nyumba zao wanaziita bedstitter, ukichelewesha hela siku moja unakuta vitu nje, na kashaingia mpangaji mpya.
Kule kwao mambo ni magumu mno. Kile kingereza chao kisikubabaishe wao wanasema Mambo kwa ground ni hard
Ndio maana Mkenya akija Tanzania anafanya kazi wa nguvu zake zote. Na ndio maana wamejanjaruka mno kutokana na shida.
πNdio ni kweli ....nahisi shida imefanya Kila mtu awe na ajili..
Huku Tanzania ukiwa chawa tu unaishi vizuri kuliko muajiriwa
Mzee apewe maua yake β πMzee Mwinyi, nimeona nikatamani sasa ndani ya miezi sita navuna mapapai 40,000
View: https://m.youtube.com/watch?v=iHEsb-jtx-w
Mzee apewe maua yake β π
Aisee!Prof. Tibaijuka - Usipoelewa Mfumo wa Dunia Unavyofanya Kazi Huwezi Kutobo
View: https://m.youtube.com/watch?v=l2Zvwq_2EP4
Nasafirisha Parachichi za Burundi kwenda Uholanzi kama vile zinatokea Tanzania biashara sio kulia lia bali ujanjaInasemekana, kuna wakati Wakenya walikuwa wanakuja Tanzania, nafikiri Gairo, kununua viazi mviringo na kwenda kuvifsafisha, kuvigrade, na kuvifanyia packaging kisha kuvisafirisha kwenda sokoni Dubai.
Inasemekana, Wakenya hua wanavifuata vitunguu Tanzania, si kwa ajili ya kuviuza Kenya, bali nchi za nje hasa Dubai.
Inasemekana, hata Wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite, kwa miaka ya nyuma, walikuwa wanapendelea zaidi kuuza madini yao Kenya kuliko nchini. Inaonekana kulikuwa na cha ziada walichokuwa wanakipata huko, vinginevyo, wasingejihatarisha kiasi hicho kutorosha madini mpaka Kenya.
Inasemekana, miaka ya nyuma , Kenya ilikuwa ikisafirisha Tanzanite nyingi zaidi kuliko Tanzania, nchi pekee duniani Tanzanite inakopatikana.
Inasemekana, miaka ya nyuma, Wakenya walikuwa wakifuata parachichi nchini Tanzania. Kipindi hicho, parachichi zilikuwa na bei nzuri, lakini walipoacha kufanya hivyo, wakulima wa Tanzania wakaambulia maumivu. Na hayo maparachichi, Wakenya walikuwa wakienda kuyasafirisha kwenda "ng'ambo".
Inavyoonekana, Wakenya wako vizuri zaidi kwenye biashara za "Kimataifa" kuwazidi Watanzania.
Wakenya ni "ndugu" zetu, kama wao wameweza, kwa nini sisi tushindwe?
Haitakuwa jambo jema endapo tutaamua kwenda kujifunza kwao?
Binafsi ninafikiria nimtafute Mkenya aliye vizuri kwenye hilo eneo ili nimfanye "mentor" wangu.
Tanzania tuna fursa nyingi sana. Tunachohitaji ni IDEA EXPLOSION!