Kama Wakenya wameweza, sisi tunashindwa kwenda kujifunza kwao?

Kama Wakenya wameweza, sisi tunashindwa kwenda kujifunza kwao?

2021 22 Julai

Natengeneza Millioni Ishirini kwa Mwezi - Kyando

View: https://m.youtube.com/watch?v=ABgMyvX3FxE

Kutana na Ezron Satoki Kyando Mkulima na mwanachama wa TAHA kutoka Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani nchini Tanzania ambaye ameanza kuona matunda ya kilimo cha horticulture. Kyando ameweza kubadilisha maisha yake huku akikiri kuwa hata mshahara wake haujawahi kufikia faida anayopata hivi sasa kupitia kilimo cha horticulture.
Source : TAHA ONLINE TV
 
Hata life style yao
Wakenya hawana mambo ya kununuliana vyakula au kupeana hela,kupigana mzinga kule wanakaushiana
Mbongo mtu anaweza amka asubuhi mpaka jioni yeye ni kupiga vizinga tu siku inaenda

Ova
Mambo Kenya ni magumu mno. Lazima wawe wachoyo.
 
Ni sera ya serikali. Tz biasharq yoyote ya mazao kwenda nje ya nchi lazima ipitie bodi ya mazao na vyama vya ushirika ili serikali inyonye pesa ya kutosha. Wenzetu hakuna huu ujinga.
 
Hata life style yao
Wakenya hawana mambo ya kununuliana vyakula au kupeana hela,kupigana mzinga kule wanakaushiana
Mbongo mtu anaweza amka asubuhi mpaka jioni yeye ni kupiga vizinga tu siku inaenda

Ova
Hii Ina thibitika beyond a reasonable doubt naunga mkono hoja😔😔😊😊☺️☺️🤓🤓
 
Na kweli chek kuanzia namanga mpaka karibia Nairobi Kuna ka ukame flani hivi ka mda wote...
Eneo kubwa la Kenya ni jangwa. Sehemu nzuri iliyobakia ni mbuga za wanyama,ardhi ya vigogo, wawekezaji na eneo dogo lililobakia ndio wananchi wanaishi.
Kenya kuna maisha MAGUMU sana. Halafu jamaa wana ukabila promax na uchoyo wa kiwango cha lami. Kule hakuna mdau wa kukupa hata buku la maji au mama ntilie wa kukupa ukoko wa buku siku ikaisha. Hakuna cha mjomba, shangazi wala Kaka, wala Baba mdogo. Baba wenye nyumba ni wa kenya ni wakali mno waanaitwa Landlord, nyumba zao wanaziita bedstitter, ukichelewesha hela siku moja unakuta vitu nje, na kashaingia mpangaji mpya.
Kule kwao mambo ni magumu mno. Kile kingereza chao kisikubabaishe wao wanasema Mambo kwa ground ni hard

Ndio maana Mkenya akija Tanzania anafanya kazi wa nguvu zake zote. Na ndio maana wamejanjaruka mno kutokana na shida.
 
Anakupaje kwanza? Maana ujinga wetu ndio mtaji wao.... Na jamaa wa binafsi Sana, kumbuka kule kunaukabila hata biashara utakua mkikuyu kwa mkikuyu na mluo kwa mluo.. Sembuse uje weye Mtanzania... Hapa ni sisi watanzania kubadili mtizamo... Tukitumia umoja wetu kuchangiana ujuzi na mtaji tungekua mbali... Tatizo roho za kila mtu kutakua awe bora zaidi na mashuhuri zimetufanya kila mtu afe kivyake... 😢😢
Sidhani kama ukabila unaweza kuwa kikwazo kwa Mtanzania anayetaka kwenda kufanya biashara Kenya. Kule pia kuna Wazungu, Waarabu, Wachina , Wahindi, Watanzania n.k., wanaofanya biashara huko. Mojawapo wa Watanzania waliowekeza huko ni Rostam Aziz. Hilo la ukabila wala si kikwazo kiongozi. Dhubutu kujitosa bila hofu.
 
Eneo kubwa la Kenya ni jangwa. Sehemu nzuri iliyobakia ni mbuga za wanyama,ardhi ya vigogo, wawekezaji na eneo dogo lililobakia ndio wananchi wanaishi.
Kenya kuna maisha MAGUMU sana. Halafu jamaa wana ukabila promax na uchoyo wa kiwango cha lami. Kule hakuna mdau wa kukupa hata buku la maji au mama ntilie wa kukupa ukoko wa buku siku ikaisha. Hakuna cha mjomba, shangazi wala Kaka, wala Baba mdogo. Baba wenye nyumba ni wa kenya ni wakali mno waanaitwa Landlord, nyumba zao wanaziita bedstitter, ukichelewesha hela siku moja unakuta vitu nje, na kashaingia mpangaji mpya.
Kule kwao mambo ni magumu mno. Kile kingereza chao kisikubabaishe wao wanasema Mambo kwa ground ni hard

Ndio maana Mkenya akija Tanzania anafanya kazi wa nguvu zake zote. Na ndio maana wamejanjaruka mno kutokana na shida.
Ndio ni kweli ....nahisi shida imefanya Kila mtu awe na ajili..
Huku Tanzania ukiwa chawa tu unaishi vizuri kuliko muajiriwa
 
WaTanzania wachangamke, tuache kuwa lialia. Fursa kibao. Tujiongeze katika matumizi ya TEHAMA tekenelojia ya Habari na mawasiliano - ICT katika sekta kilimo cha kuuza kibiashara kuvuka mipaka.

View: https://m.youtube.com/watch?v=6DRlX5vIOE0
Pia turasimishe shughuli zetu kupitia mifumo ya vikundi, majukwa, brandi na kutumia benki ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kujieleza unapofuatwa na mwekezaji wa ndani na nje ya nchi. Tuache kufanya mambo kienyeji ambapo hakuna kumbukumbu ...
 
Inasemekana, kuna wakati Wakenya walikuwa wanakuja Tanzania, nafikiri Gairo, kununua viazi mviringo na kwenda kuvifsafisha, kuvigrade, na kuvifanyia packaging kisha kuvisafirisha kwenda sokoni Dubai.

Inasemekana, Wakenya hua wanavifuata vitunguu Tanzania, si kwa ajili ya kuviuza Kenya, bali nchi za nje hasa Dubai.

Inasemekana, hata Wachimbaji wadogo wa madini ya Tanzanite, kwa miaka ya nyuma, walikuwa wanapendelea zaidi kuuza madini yao Kenya kuliko nchini. Inaonekana kulikuwa na cha ziada walichokuwa wanakipata huko, vinginevyo, wasingejihatarisha kiasi hicho kutorosha madini mpaka Kenya.

Inasemekana, miaka ya nyuma , Kenya ilikuwa ikisafirisha Tanzanite nyingi zaidi kuliko Tanzania, nchi pekee duniani Tanzanite inakopatikana.

Inasemekana, miaka ya nyuma, Wakenya walikuwa wakifuata parachichi nchini Tanzania. Kipindi hicho, parachichi zilikuwa na bei nzuri, lakini walipoacha kufanya hivyo, wakulima wa Tanzania wakaambulia maumivu. Na hayo maparachichi, Wakenya walikuwa wakienda kuyasafirisha kwenda "ng'ambo".

Inavyoonekana, Wakenya wako vizuri zaidi kwenye biashara za "Kimataifa" kuwazidi Watanzania.

Wakenya ni "ndugu" zetu, kama wao wameweza, kwa nini sisi tushindwe?

Haitakuwa jambo jema endapo tutaamua kwenda kujifunza kwao?

Binafsi ninafikiria nimtafute Mkenya aliye vizuri kwenye hilo eneo ili nimfanye "mentor" wangu.

Tanzania tuna fursa nyingi sana. Tunachohitaji ni IDEA EXPLOSION!
Nasafirisha Parachichi za Burundi kwenda Uholanzi kama vile zinatokea Tanzania biashara sio kulia lia bali ujanja
 
Back
Top Bottom