Kama Wizara ya Maliasili na Serikali hawana mkakati wa kutokomeza kunguru weusi, tuwape tenda wachina

Ninapoishi kuna Minazi mingi ndio wamefanya makazi yao, nimewawekea maji kwenye chombo maalum baada ya hapo awali kua wanafungua bomba la nje wanakunywa maji na kuacha yanamwagika.

Mabaki ya chakula hua nawawekea sehemu maalum na wakishaniona naelekea hiyo sehemu wanakuja kwa kelele kali hua natafsiri wanafurahi na kuitana, wanabeba na kula kwenye nyumba zao,

Watu wengine wanaona kero makelele yao nikagundua kinachowasumbua ni kiu cha maji.
Hapo ni kama unawafuga hivi.
Fanya maboresho ili wapungue. Kwenye maji na chakula weka sumu ili wakitumia wakafe, utakua umesaidia jamii ya hapo.
 
Kunguru wanauzao kama bata
 
Hapo ni kama unawafuga hivi.
Fanya maboresho ili wapungue. Kwenye maji na chakula weka sumu ili wakitumia wakafe, utakua umesaidia jamii ya hapo.
Sina roho mbaya hiyo, unaweza ukafanya hayo bila kushirikisha wengine.
 
Ndio maana sijasema sumu, diazepam itawasaidia ku relax na kupunguza mishe kwa kulala
Hujui kama hao Kunguru wana familia pia inawahitaji?
Wakilala bila kutafuta chochote huoni vifaranga vyao vitakufa kwa kiu na njaa?
 
Kama nchi ningeshauri tujifunze kushughulika na kero hata kama hazina madhara ya moja kwa moja!
Huko ulaya wenzetu huwa wanafanya oparesheni ya kuondoa paka, mbwa na ndege wasio natija!

Hata hapa kwetu sioni kama inashindikana kuwaondoa kitaalam hawa kunguru weusi!

Historia inasemekana wazo la kuleta mbegu ya hawa kunguru weusi lilifanyika katika utawala wa CCM chini ya waziri mkuu wa zamani EDWARD LOWASSA ambapo liligharimu bilion 7.5 Wakiwa na lengo kwamba Kunguru hawa weusi wangesaidia kula uchafu huko mahospitali!

Bahati mbaya maamuzi hayo yalifanyika pasipo utafiti wa kitaalam!
Kundi la kwanza lilimwagwa Zanzibar! Na baadae wakazaliana na wengine walisafili kuja Tanzania bara kwa kudandia meli na majahazi baharini!

Hivi sasa kunguru hawa ni kero kubwa sana kwa taifa na wananchi!
1. Wanapiga makelele baadhi ya makundi mahospitalini
2. Wanachafua mazingira ya miti na kujisaidia ovyo.
3. Wanaharibu miundombinu ya umeme na kusababisha ukosefu wa umeme kwa dharula (wanabeba vipande vya waya wanapotua kwenye nyaya za tanesco wanagonganisha waya transfoma zinazima-KERO)
4. Wanachafua nguo za wananchi zilizoanikwa juani!
5. Wanawasumbua sana walevi na wapenda nyama choma huko bar
6. Wana wanyea mav hasa wanapoona mtu kavaa vizuri hususan MTU akivaa nguo nyeupe au ya kung'aa
7. Wanapokonya chakula watoto wadogo
8. Wanaipua mboga jikoni na kula hata kama ilifunikwa
9. Wakifa Hawaozi haraka
10. Ni hatari kwenye baadhi ya injini hasa maeneo ya uwanja wa ndege

Kiufupi hawa kunguru weusi wana kero nyingi ambazo lazima serikali ifanye mpango mkakati kuwatokomeza kabla hawajaongezeka!

Kama serikali itashindwa basi tenda wapewe wachina watuondolee huu upuuzi unaozidi kuzaliana!

WATU WAZURI HUSHUGHULIKIA KERO ZA WATU ILI WAKUMBUKWE KWA MAZURI NA SI KWA MABAYA
Omba radhi, lowassa hakuwahi kufanya ujinga huu, haya mandege yaliletwa na waarabu huko Zanzibar miaka ya 1800,lango la waarabu kwa nyakati hizo ni wasaidie kula mizoga ya samaki ufukweni.
 
Nashindwa fuga kuku wa kienyeji kisa hawa.
 
Historia inasemekana wazo la kuleta mbegu ya hawa kunguru weusi lilifanyika katika utawala wa CCM chini ya waziri mkuu wa zamani EDWARD LOWASSA ambapo liligharimu bilion 7.5 Wakiwa na lengo kwamba Kunguru hawa weusi wangesaidia kula uchafu huko mahospitali!

Bahati mbaya maamuzi hayo yalifanyika pasipo utafiti wa kitaalam!
Kundi la kwanza lilimwagwa Zanzibar! Na baadae wakazaliana na wengine walisafili kuja Tanzania bara kwa kudandia meli na majahazi baharini!
Historia feki! kwa mujibu wa hadithi simulizi kunguru weusi waliletwa Zanzibar na jamii fulani yenye asili ya India mwisho wa karne ya 19, lengo ilikuwa ni kusafisha mizoga. Baadae ndiyo wakazaliana na kufikia hatua hii. Kwa zanzibar enzi ya zamani kulikuwa na kampeni maalumu ya kuua kunguru kila baada ya kipindi fulani lakini kwa sasa zoezi hilo naona halipo. Ulikuwepo hata mradi maalumu wa kudhibiti kwa mitego na kuharibu mayai yao.

Ila hilo la Lowassa naona kama munamtwisha mzigo usiokuwa wake.

Ukitaka kupunguza mazalio ya kunguru ni uharibu mayai yao labda ndio utaweza kuwapunguzaa.
 
..wapo kunguru wenye rangi nyeupe kifuani ..wamepotezwa na hivi vikunguru vyeusi tii..licha ya kuwa wana maumbo makubwa, halafu wale hawana fujo. Hawa weusi pia wamesababisha kupotea kwa ndege warukao wengine..mfano tausi waliokuwa maeneo ya mjini wamesurvive wachache( licha ya changamoto za kimazingira zingine) , ndege shorwe, viswiswi etc nadhani ipo haja wawe eliminated kabisa. They are an unnecessary.
 
Nikuweka mitego kwenye miti wanayo lala, au serikali itangaze kununua kunguru mmoja @ 500 ili watu washawishike kubuni mitego
 
..wapo kunguru wenye rangi nyeupe kifuani ..wamepotezwa na hivi vikunguru vyeusi tii..licha ya kuwa wana maumbo makubwa, halafu wale hawana fujo. Hawa weusi pia wamesababisha kupotea kwa ndege warukao wengine..mfano tausi waliokuwa maeneo ya mjini wamesurvive wachache( licha ya changamoto za kimazingira zingine) , ndege shorwe, viswiswi etc nadhani ipo haja wawe eliminated kabisa. They are an unnecessary.
Ndiyo maana kitambo sana ile species sijaiona
 
Hawa kunguru wana akili sana, km sina hakika km ndo black raven ila wana akili sana.
Km ikatokea ukamuua mmoja wakakuona... Wanakukariri ukifika tu wanaondoka km ni mtu wa kuwepo hapo muda mwingi bas wanahama kabisa.
Na mmoja akifa huwa wanazunguka hapo weee huku wanapiga kelele.
Niliwahi kuona kunguru mmoja amebeba kitu km nyama iv.. Akafika kwenye pindo ya bati akaficha.... Nikamfatilia... Baada masaa kadhaa akarud akala akabakisha akaficha tena. Nilishangaa

Sent from my SO-01K using JamiiForums mobile app
 
Historia feki! kwa mujibu wa hadithi simulizi kunguru weusi waliletwa Zanzibar na jamii fulani yenye asili ya India mwisho wa karne ya 19, lengo ilikuwa ni kusafisha mizoga. Baadae ndiyo wakazaliana na kufikia hatua hii. Kwa zanzibar enzi ya zamani kulikuwa na kampeni maalumu ya kuua kunguru kila baada ya kipindi fulani lakini kwa sasa zoezi hilo naona halipo. Ulikuwepo hata mradi maalumu wa kudhibiti kwa mitego na kuharibu mayai yao.

Ila hilo la Lowassa naona kama munamtwisha mzigo usiokuwa wake.

Ukitaka kupunguza mazalio ya kunguru ni uharibu mayai yao labda ndio utaweza kuwapunguzaa.
Yule jamaa noma... Huenda ni kweli make alitaka adi kuleta mawingu ya mvua.... [emoji1787][emoji1787]

Sent from my SO-01K using JamiiForums mobile app
 
Hawa kunguru wana akili sana, km sina hakika km ndo black raven ila wana akili sana.
Km ikatokea ukamuua mmoja wakakuona... Wanakukariri ukifika tu wanaondoka km ni mtu wa kuwepo hapo muda mwingi bas wanahama kabisa.
Na mmoja akifa huwa wanazunguka hapo weee huku wanapiga kelele.
Niliwahi kuona kunguru mmoja amebeba kitu km nyama iv.. Akafika kwenye pindo ya bati akaficha.... Nikamfatilia... Baada masaa kadhaa akarud akala akabakisha akaficha tena. Nilishangaa

Sent from my SO-01K using JamiiForums mobile app
Wana akili na shabaha wakikulenga inya hawakukosi! Hasa ukiwa unakula
 
Historia feki! kwa mujibu wa hadithi simulizi kunguru weusi waliletwa Zanzibar na jamii fulani yenye asili ya India mwisho wa karne ya 19, lengo ilikuwa ni kusafisha mizoga. Baadae ndiyo wakazaliana na kufikia hatua hii. Kwa zanzibar enzi ya zamani kulikuwa na kampeni maalumu ya kuua kunguru kila baada ya kipindi fulani lakini kwa sasa zoezi hilo naona halipo. Ulikuwepo hata mradi maalumu wa kudhibiti kwa mitego na kuharibu mayai yao.

Ila hilo la Lowassa naona kama munamtwisha mzigo usiokuwa wake.

Ukitaka kupunguza mazalio ya kunguru ni uharibu mayai yao labda ndio utaweza kuwapunguzaa.
Mtego wa mwisho kuuona ulikuwa karibu na Ofisi ya Hifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe.

Hapana shaka mitego hii ilikuwa chini ya UNDP.
 
Back
Top Bottom