Kama Wizara ya Maliasili na Serikali hawana mkakati wa kutokomeza kunguru weusi, tuwape tenda wachina

Kama Wizara ya Maliasili na Serikali hawana mkakati wa kutokomeza kunguru weusi, tuwape tenda wachina

Bilioni saba duh mbona hayo mabilioni yangetumika na program nyinginezo mji wa dar ungekuwa safi na wa kupendeza mnooo
Kunguru hao wangekuwa wa kutafuna mbu wa Dar mbona huo mradi ungekuwa bomba.
 
Hao kunguru ni codes moja mbaya sana watu hawajui tu. Wanaweza kuja tumika kama biological weapon siku ukitaka angamiza wtz.
 
Kuna eneo limaitwa Sultan lipo Mrogoro(M) aisee ile barabara ya Mangesho ni hapafai ukipita pale unapita kimchale chale. Miti inapendezesha sana lile eneo ila kero kubwa imekuwa ndio makazi ua kunguru wale. Mpaka barabara imechafuka tokana na kinyesi chao
 
Kuna eneo limaitwa Sultan lipo Mrogoro(M) aisee ile barabara ya Mangesho ni hapafai ukipita pale unapita kimchale chale. Miti inapendezesha sana lile eneo ila kero kubwa imekuwa ndio makazi ua kunguru wale. Mpaka barabara imechafuka tokana na kinyesi chao
Uchafuzi wa mazingira
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] eti wananizomea lakini ulishajua nia yao haikua kumwaga pombe yako bali ilikua kupata maji, ndio maana nikasema hawa kinachowasumbua sana ni kiu cha maji ndio maana wanakua na vurugu,

Wasamehe sababu wote ni viumbe wa Mungu na Rizki yao inatokana na sisi.
Kunguru hafugiki wala sio wa kumkaribisha kwako
 
Kunguru hafugiki wala sio wa kumkaribisha kwako
Na mimi sijawafuga wala kuwakaribisha ila nimeweka huo utaratibu wa kuwapa maji kwenye chombo chao maalum na maji hayo hawayatumii tu Kunguru kuna Ndege wengine wanakunywa, Paka, na wadudu
 
Jaman kumbe wamefikia hatua ya kula pembejeo!? Huko buza wanaiba sana chupi zilizoanikwa hasa zile tandabui kama barakoa! Wanazichukua wakizani utumbo
We utakuwa mkulima wa pdf,yaani hujui hata maana ya pembejeo? Karanga si pembejeo.Mfano wa pembejeo ni mbolea,mbegu za kupanda,sumu za wadudu waharibifu n.k
 
I've rescued this baby bird today, baada ya matone kadhaa ya maji kakapata nguvu na kuruka kurudi kwa familia yake [emoji3059]
Snapchat-1068493258.jpg
 
Kama nchi ningeshauri tujifunze kushughulika na kero hata kama hazina madhara ya moja kwa moja!
Huko ulaya wenzetu huwa wanafanya oparesheni ya kuondoa paka, mbwa na ndege wasio natija!

Hata hapa kwetu sioni kama inashindikana kuwaondoa kitaalam hawa kunguru weusi!

Historia inasemekana wazo la kuleta mbegu ya hawa kunguru weusi lilifanyika katika utawala wa CCM chini ya waziri mkuu wa zamani EDWARD LOWASSA ambapo liligharimu bilion 7.5 Wakiwa na lengo kwamba Kunguru hawa weusi wangesaidia kula uchafu huko mahospitali!

Bahati mbaya maamuzi hayo yalifanyika pasipo utafiti wa kitaalam!
Kundi la kwanza lilimwagwa Zanzibar! Na baadae wakazaliana na wengine walisafili kuja Tanzania bara kwa kudandia meli na majahazi baharini!

Hivi sasa kunguru hawa ni kero kubwa sana kwa taifa na wananchi!
1. Wanapiga makelele baadhi ya makundi mahospitalini
2. Wanachafua mazingira ya miti na kujisaidia ovyo.
3. Wanaharibu miundombinu ya umeme na kusababisha ukosefu wa umeme kwa dharula (wanabeba vipande vya waya wanapotua kwenye nyaya za tanesco wanagonganisha waya transfoma zinazima-KERO)
4. Wanachafua nguo za wananchi zilizoanikwa juani!
5. Wanawasumbua sana walevi na wapenda nyama choma huko bar
6. Wana wanyea mav hasa wanapoona mtu kavaa vizuri hususan MTU akivaa nguo nyeupe au ya kung'aa
7. Wanapokonya chakula watoto wadogo
8. Wanaipua mboga jikoni na kula hata kama ilifunikwa
9. Wakifa Hawaozi haraka
10. Ni hatari kwenye baadhi ya injini hasa maeneo ya uwanja wa ndege

Kiufupi hawa kunguru weusi wana kero nyingi ambazo lazima serikali ifanye mpango mkakati kuwatokomeza kabla hawajaongezeka!

Kama serikali itashindwa basi tenda wapewe wachina watuondolee huu upuuzi unaozidi kuzaliana!

WATU WAZURI HUSHUGHULIKIA KERO ZA WATU ILI WAKUMBUKWE KWA MAZURI NA SI KWA MABAYA
Rai yako ina manufaa, lakini hili la Waziri mkuu Lowasa kuleta Kunguru ni uzushi.

Uwaziri mkuu wa Lowasa ni wa juzijuzi hapa, wakati kunguru hao wana zaidi ya miongo miwili!
 
We utakuwa mkulima wa pdf,yaani hujui hata maana ya pembejeo? Karanga si pembejeo.Mfano wa pembejeo ni mbolea,mbegu za kupanda,sumu za wadudu waharibifu n.k
Hahah asante afisa kilimo
 
Hata mimi hawaniogopi, naweza nikawa nje nimekaa wakawa pembeni yangu ila akitokea mtu mwingine wanaondoka,

Napenda sana Ndege na Wanyama.
Ogopa sana kunguru wanamagonjwa mengi ..coz wanasafiri umbali mrefu na kula kila Aina ya uchafu
 
Sipikii nje sababu sina jiko la nje, hawaingii ndani na nafua kila siku hawajawahi kunyea nguo zangu na hata ikitokea wamenyea so what? Mavi ya Kunguru yana madhara gani hadi inifanye niwachukie?
Kwa watoto wadogo wanaweza kata watoboa macho
 
Back
Top Bottom