Kama Yesu Kristo alikufa Msalabani ili tukombowele katika utumwa wa Dhambi mbona bado dhambi zinazidi kuongezeka?

Asante
 
1)Kwa sababu Yesu Kristo hakuja kufuta dhambi bali kulipa gharama ya dhambi.

2)Siyo wote wanaomini Yesu Kristo alikufa halafu akafufuka kwahiyo ni lazima watu waendelee kuishi katika dhambi..

Kwa leo tuishie hapo
 
A good Thought here
 
Kwa sababu Mungu ni mwanademocrasia.amemleta yesu ili kila anayemwamini anaokolewa.lakini hajamlazimisha mtu yoyote amuamini yesu.maovu yanazidi kwa sababu hofu ya Mungu inapungua mioyoni mwa watu.
 


Kuna maji ya Kilimanjaro dukani ambayo unatakiwa kununua unywe upone.

Yesu ameyatoa hayo maji bure unaweza kunywa na ukapona kabisa bila shida.

Kitu Yesu ambacho hawezi kufanya ni kuyachukua na kukuleta na kukulazimisha unywe.

Dhambi zipo na zitaendelea kuwepo sababu wanadam hawajachukua hatua kumfuata Yesu na kupata ukombozi.
 
Narudia tena, ni mchongo tu, hakuna Mungu wa kweli anaemtoa mwanae kafara. Aumbe dhambi na atume mwanae kuondoa dhambi, inaingia akilini kweli? Ila imesukwa kiasi karibu nusu ya ulimwengu umeamini, hasa ulimwengu wa tatu kwa waliokata tamaa na maisha.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Mungu ameumba dhambi?Mungu hakuumba dhambi acha upotoshaji.Ni mtu mjinga tu ambaye haamini uwepo wa Mungu.
 
unachaganya habari za Yesu na za Mpinga kristo
 
Wanaokolewa wale wanaotaka Chief. Kama hutaki hulazimishwi. Usisahau humu dunian kuna watu wa Mungu pasee na washetan pasee. Na ndio maana ya ule mfano wa kuyaacha magugu na ngano zikue pamoja cku akija Bwana wa mavuno ndio atayatenga.
 
Watu Woote Ni wa MUNGU, ila wanaoipokea kafara ya Yesu Kristo wanafanywa kuwa watoto wa MUNGU...
 
Niliwaambieni kila swali gumu niulizwe mimi maana wakristo na waislamu wa sasa awana akili kabisa na hata wasio wakristo au waislamu ni hivyo hivyo .....ILO SWALI LAKO LINATOKANA NA KUTOKUJUA KRISTO ALISULUBIWA KWA SABABU GANI ? UKIJUA SABABU YA KWELI UTAKUWA UMEPATA JIBU SAHIHI LA ILO SWALI LAKO ....WENGI WANA MASWALI KUTOKANA NA MAFUNDISHO POTOVU YA INJILI FEKI YA MAKANISANI .
 
Si kweli! Una maana wasiomwamini kuwa ni mwana wa Mungu hawatakombolewa? Mungu aliumba ili awapoteze? Dini zimechongwa tu na wajanja!
 
Dhambi ni kwenda kinyume na maagizo ya Mungu ,(Allah)

Kuoa wake wengi sio utaratibu wa Mungu.............
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…