Uchaguzi 2020 Kamanda Mambosasa: Mbowe na wenzake kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi, walipanga kulipua vituo vya mafuta

Uchaguzi 2020 Kamanda Mambosasa: Mbowe na wenzake kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi, walipanga kulipua vituo vya mafuta

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
UPDATE

617D7053-8232-4113-969C-38F1830D3D4F.jpeg


"Mbowe na wenzake watashtakiwa kwa makosa ya ugaidi kwa sababu kuna mtu ametupa ushahidi kuwa walipanga kulipua vituo vya mafuta jijini Dar na kuleta maafa makubwa," Lazaro Mambosasasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM.

=====

Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam ACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia watu kadhaa wakiwemo viongozi watatu wa CHADEMA.

Viongozi wa CHADEMA wanaowashikilia ni pamoja na Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Godbless Lema na Boniface Jacob.

Amesema wanawashikilia viongozi hao kwa kuwa wanahatarisha usalama wa Raia na mali zao kwa kuwa Novemba 2 walipanga kuwatumia vijana kuchoma moto miundominu na vituo vya mafuta.

Aidha kwa usiku huu wanaendelea kuwatafuta watu ambao wanawashawishi vijana kushiriki maandamano ambayo Polisi wamesema ni ya Vurugu na si amani kwa kuwa wanaoshawishiwa ni vijana wavuta bangi.

Amesema hayo katika kipindi mubashara kilichorushwa na ITV.

PIA SOMA
= > Uchaguzi 2020 - Dar es Salaam: Watu watatu zaidi wakamatwa kuzuia maandamano
 
Police Dar es salaam yaanza kuwakamata waliopanga maandamano.

Walio kamatwa ni pamoja na Aliye kua mbunge wa Arusha Godbless Lema pamoja na Mwwnyekiti wa CHADEMA taifa Mbowe
 
Wapinzani Wangeacha tu maandamano ili Goma lianze automatically.

Sasa Watanzania kesho Tunaendelea na Shughuli zetu Kama kawaida.

Nilikuwa nawaza nitaendaje kwenye shughuli zangu za kupeleka mkono kinywani huku Kuna maandamano.
 
Hili tulilitarajia ila wanazidi kuharibu. Hakuna watachowafanya zaidi ya kuja kuwaachia tu lengo likiwa ni kuvuruga maandamano ya kesho kwani hayo mashtaka hata wakiambiwa watoe ushahidi kuyathibitisha watakuwa hawa hawana.

Hata hivyo, viongozi nchi nzima ni wengi, kwahiyo; hakuna kitachoshindikana kwa kuwakamata viongozi wa juu, kwani huku ni kuchochea hasira za viongozi wa chini yao na wafuasi wao kwa ujumla.

Lissu, Mdee, Mnyika, Zitto, Hilda Newton na wengineo mjiandae kabla hakujakucha.

Mataga sasa mkome kusema makamanda waoga bali waoga wameshajionesha ni kina nani.
 
Back
Top Bottom