Uchaguzi 2020 Kamanda Mambosasa: Mbowe na wenzake kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi, walipanga kulipua vituo vya mafuta

Uchaguzi 2020 Kamanda Mambosasa: Mbowe na wenzake kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi, walipanga kulipua vituo vya mafuta

Kupanga kuchoma vituo ni maneno ya kutunga au tuseme ni ule mwendelezo wa kesi bambikizi.
Tulifikiri kuwa Tanzania ingejirudi na kuacha kubambikiza watu kesi ila sasa jawabu la mambo gaya ni kwamba Serikali imejipanga kutumia mabavu maradufu ya yaliyoyarumia huko nyuma ili kulinda maovu yake.
Hebu fikiria polisi anasema et kuna mty katuambia wamepanga kuchoma vituo. Sasa kumbe hizi ni gabari za kuambiwa?
Na kama ni mtu kama Gwajima amewaambia ukweli wa ushuhuda wake una uhalali kiasi gani?
Jeshi la polisi au investigator yoyote ataitreat habari yoyote kama kweli mpaka atakapojiridhisha pasipo shaka kuwa habari ile si kweli.

Mimi nikisema nimemuona mtu mwenye shati jekundu akiambatana na mtoto wako alipokuwa akitoka shuleni na kitendo kile kilinipa wasiwasi maana si kawaida yake... Wewe kama mzazi utasema ni habari za kuambiwa!?

Kwani kuchoma kituo kunahitaji nini!? Na unajua ni vituo vingapi viko huko nje!? Unajua watachoma kipi!?

Ikiwa wakiachwa kisha wakachoma kweli!? Hata kwa kufuata mkumbo tu.. maana maandamano yaleta watu wa kila namna na often kuyaitisha unakuwa na mpango ila yakishaanza huwezi kuyaongoza tena... Special interest zinaanza kujitokeza....

Kila mahali hata waongozaji wa maandamano wamekiri sehemu kubwa ya vurugu haikuwa mipango yao...sema ikishatokea hawawezi kuizima na ndio inakuwa vurugu tayari. Sasa kama tumeona matokeo yake kote kwanini tujaribu !?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kupanga kuchoma vituo ni maneno ya kutunga au tuseme ni ule mwendelezo wa kesi bambikizi.
Tulifikiri kuwa Tanzania ingejirudi na kuacha kubambikiza watu kesi ila sasa jawabu la mambo gaya ni kwamba Serikali imejipanga kutumia mabavu maradufu ya yaliyoyarumia huko nyuma ili kulinda maovu yake.
Hebu fikiria polisi anasema et kuna mty katuambia wamepanga kuchoma vituo. Sasa kumbe hizi ni gabari za kuambiwa?
Na kama ni mtu kama Gwajima amewaambia ukweli wa ushuhuda wake una uhalali kiasi gani?
How sure are you kwamba hizo kesi wamwbambikiziwa ?
 
CHADEMA acheni wananchi wapuuzi wa nchi hii waisome namba, mnajitoa kwa ajili yao ila hakuna support yeyote. kiufupi huwezi kumpigania mtumwa ambaye aliyozea utumwani.
 
"Mbowe na wenzake watashitakiwa kwa makosa ya ugaidi kwa sababu kuna mtu ametupa ushahidi kuwa walipanga kulipua vituo vya mafuta jijini Dar na kuleta maafa makubwa" SACP Lazaro Mambosasa.

C57F3512-AB55-4517-A2EE-B3F055ECA3B0.jpeg
 
Lowassa alisema kulinda kura wamwachie. Lissu akaja na ukipiga kura linda kura. The rest is history.
 
UPDATE

"Mbowe na wenzake watashtakiwa kwa makosa ya ugaidi kwa sababu kuna mtu ametupa ushahidi kuwa walipanga kulipua vituo vya mafuta jijini Dar na kuleta maafa makubwa," Lazaro Mambosasasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM.

=====

Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam ACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia watu kadhaa wakiwemo viongozi watatu wa CHADEMA.

Viongozi wa CHADEMA wanaowashikilia ni pamoja na Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Godbless Lema na Boniface Jacob.

Amesema wanawashikilia viongozi hao kwa kuwa wanahatarisha usalama wa Raia na mali zao kwa kuwa Novemba 2 walipanga kuwatumia vijana kuchoma moto miundominu na vituo vya mafuta.

Aidha kwa usiku huu wanaendelea kuwatafuta watu ambao wanawashawishi vijana kushiriki maandamano ambayo Polisi wamesema ni ya Vurugu na si amani kwa kuwa wanaoshawishiwa ni vijana wavuta bangi.

Amesema hayo katika kipindi mubashara kilichorushwa na ITV.

PIA SOMA
= > Uchaguzi 2020 - Dar es Salaam: Watu watatu zaidi wakamatwa kuzuia maandamano
Wangeacha waandamane kuondoa ghadhabu.. au wanataka yale ya MKIRU?!

Huwezi kuchemsha maji huku umeziba kabisa kuzuia mvuke kutoka, afu ww ubaki salama.

Wananchi walio wengi Wana hasira juu ya matendo ya watawala waovu hawa.
 
chadema acheni wananchi wapuuzi wa nchi hii waisome namba, mnajitoa kwa ajili yao ila hakuna support yeyote. kiufupi huwezi kumpigania mtumwa ambaye aliyozea utumwani.
Hao ✌wanafanya haya yote Kwa maslahi yao wenyewe na hasa ni kwakuwa wamekosa ubunge mana kama wangepata wasinge Fanya yote haya.
 
Eti vijana wavuta bangi! Imenikumbusha Gaddafi ndivyo alivyokuwa akisema wakati Libya inaanza kuanguka! Alisema ni vijana wamepewa madawa ya kulevya wafanye fujo na maandamano!

😀😀😀😀😀😀😀😀😀
 
UPDATE

"Mbowe na wenzake watashtakiwa kwa makosa ya ugaidi kwa sababu kuna mtu ametupa ushahidi kuwa walipanga kulipua vituo vya mafuta jijini Dar na kuleta maafa makubwa," Lazaro Mambosasasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM.

=====

Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam ACP Lazaro Mambosasa amesema wanawashikilia watu kadhaa wakiwemo viongozi watatu wa CHADEMA.

Viongozi wa CHADEMA wanaowashikilia ni pamoja na Freeman Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Godbless Lema na Boniface Jacob.

Amesema wanawashikilia viongozi hao kwa kuwa wanahatarisha usalama wa Raia na mali zao kwa kuwa Novemba 2 walipanga kuwatumia vijana kuchoma moto miundominu na vituo vya mafuta.

Aidha kwa usiku huu wanaendelea kuwatafuta watu ambao wanawashawishi vijana kushiriki maandamano ambayo Polisi wamesema ni ya Vurugu na si amani kwa kuwa wanaoshawishiwa ni vijana wavuta bangi.

Amesema hayo katika kipindi mubashara kilichorushwa na ITV.

PIA SOMA
= > Uchaguzi 2020 - Dar es Salaam: Watu watatu zaidi wakamatwa kuzuia maandamano
Mungu aliumba watu wamtumikie, serikali zinaumba magaidi zipambane nao!
 
How sure are you kwamba hizo kesi wamwbambikiziwa ?
Toka masheiki wa uamsho washtakiwe kwa makosa ya ugaidi ni nini kimeshindikana kwa zaidi ya miaka saba kuhukumiwa na mahakama za sheria?
Huu ni uhakika kuwa kesi zao ni za kubambikiwa kwa sababu tu za kisiasa.
 
Mkuu sina hiyo sheria kwa sasa lakini hiyo sheria ipo hata wewe unaweza kuitafuta. Hizo sheria zipo nchi zote duniani zinatumika.
Mwambie mimi ninayo ila kwa leo nimeisahua nyumbani, nitamletea kesho.
 
Back
Top Bottom