Uchaguzi 2020 Kamanda Mambosasa: Mbowe na wenzake kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi, walipanga kulipua vituo vya mafuta

Uchaguzi 2020 Kamanda Mambosasa: Mbowe na wenzake kushtakiwa kwa makosa ya ugaidi, walipanga kulipua vituo vya mafuta

Hivi kwa mfano, ukawa umedhamiria kufanya kitu ambacho wakati mwingine (na si wakati wote), kinachukuliwa kuwa ni kinyume cha sheria, ikitokea ukashindwa kukitekeleza kwa sababu tu ya kuwekewa mazingira pingamizi, kisheria unakuwa huna hatia? Mfano ulidhamiria kwenda kuiba nyumbani kwa A, bahati mbaya ukakuta mazingira hayaruhusu, ukashidwa kuiba, je unakuwa huna hatia katika mazingira hayo, assuming umejulikana?..
Wanevunja sheria gani?

Hujajibu swali.
 
IGP simama nafasi yako, hayo ya ugaidi yasiyothibitika ni hatari tunawafundisha Watanzania chuki na kuanza rasmi kwa mambo hayo hatari kwa amani ya taifa letu.
 
Na utakuwa mpumbavu wa kiwango cha lami kwenda kuandamana wakati ulitimiza wajibu wako.

Mawakala wenu mnawachagua kisha kura zikiibwa wananchi waandamane! Kwanini wasianze mawakala na viongozi wa VYAMA vilivyoibiwa kura!?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Acha uboya, Mawakala walitolewa kwenye vituo na Pol
 
Watakao amini hiyo taarifa ya Policcm ni Wale Tu, walioamua kuishi Kwa kumwaga Damu za watu
 
Sasa ni officially tumeingia kweny udikteta rasmi.... tusilalamike tena, nawashauri wapinzani wanyamaze wasiendelee tena kupambania Demokrasia. Acha wote tuje kuongea lugha moa mbeleni. Nyerere alisema siku watanzania mkifikia kusem 'maweeeee' hapo ndipo tutajua kuwa tunaumia.... im done
Ukishajua nini maana ya Demokrasia hutaongea ,wale wanapigania Maslahi yao.

Demokrasia sio lazima Wapinzani washinde elewa hivyo ,Democracy is
a system of government by the whole population or all the eligible members of a state, typically through elected representatives.

Kama ni serikali iliyowekwa na watu kwa njia ya kufanya uchaguzi basi ni halali ,ila ingetokea kujiweka bila sanduku la kura ingekuwa ni ya kidikteta sasa tumepiga kura kashinda hata kama kuna kasoro sawa hizo huwa zipo Tume inaweza kuahidi kuzitatua na mchezo ukaisha.Demokrasia sio Mbowe kwenda bungeni na kwa taarifa tu mgombea wao alieshinda kule Nkasi Kaskazini kakubali kuingia bungeni sasa hiyo ndio Demokrasia sio akina Lissu wanayotuambia ya kuandamana bila kibali cha polisi.
 
Mpendwa za kuambiwa changanya na za kwako nadhani huwajui hao watazamaji wakujitegemea ni kina nani wanaitwa Tanzania El watch(TEW) ni hao hao wanavuruga tweeter ni Maria na kundi la kama huyo anaejita Kigogo ni Propaganda ambazo CDM imekuwa inafanya badala ya kuunda taasisi na Harakati.

Kama ni kweli basi wasingechoma ushahidi ,pia kama ulienda kupiga kura nadhani uliona kadi waliandika wapi kama hawakuridhika wangeiomba tume wahesabu kitabu na idadi ya kura(walio piga) ili kujua walipata ngapi lakini hawakufanya hivyo wakachoma ushahidi.

Karatasi ya kura ilichanwa kilichobaki pale ndio ushahidi kuwa ulipiga kura kweli na huo ndio ushahidi wa kura halali kwa hiyo halima hakujua hivyo.

Mawakala katika vituo 80 na zaidi kweli unaamini Mbowe aliwalipa Mawakala wote hao utakuta hata hawakufika elfu 20 na kama waliweka wote basi hata chakula hawakula watakuwaje na integrity.
Pengine hujui kitu katika enoe hili. Hata hivyo unaruhusiwa kuedeleza ushabiki wako kwa watawala
 
Argumentum ad hominem...
Mkuki mtamu kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu.

Wewe ulikuwa hujui ulianza hili mwenyewe?

Nakupeleka ignore list. Sitaona utakachoandika.

Maana hujafikia kiwango cha kujadiliana nami.
 
Jeshi la polisi au investigator yoyote ataitreat habari yoyote kama kweli mpaka atakapojiridhisha pasipo shaka kuwa habari ile si kweli.

Mimi nikisema nimemuona mtu mwenye shati jekundu akiambatana na mtoto wako alipokuwa akitoka shuleni na kitendo kile kilinipa wasiwasi maana si kawaida yake... Wewe kama mzazi utasema ni habari za kuambiwa!?

Kwani kuchoma kituo kunahitaji nini!? Na unajua ni vituo vingapi viko huko nje!? Unajua watachoma kipi!?

Ikiwa wakiachwa kisha wakachoma kweli!? Hata kwa kufuata mkumbo tu.. maana maandamano yaleta watu wa kila namna na often kuyaitisha unakuwa na mpango ila yakishaanza huwezi kuyaongoza tena... Special interest zinaanza kujitokeza....

Kila mahali hata waongozaji wa maandamano wamekiri sehemu kubwa ya vurugu haikuwa mipango yao...sema ikishatokea hawawezi kuizima na ndio inakuwa vurugu tayari. Sasa kama tumeona matokeo yake kote kwanini tujaribu !?

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Kwanini hutaki kutenda Haki ili kuzuia vurungu??
 
Kwani ukipewa mshahara au malipo yako, anayenufaika ni nani, aliyekupa au wewe? Una uhakika kura yako wewe moja imeibiwa au ilimuwezesha mgombea wako kushinda?

Tatizo lililopo kulazimisha tuamini kuwa adui yako ni adui yangu. Na hata hao kina Zito wanajua hakuna adui wa kudumu wala rafiki wa kudumu. Hadi sasa wameshindwa kunionyesha namna kura yangu ilivyoibiwa.
pole ndugu
 
Eti vijana wavuta bangi! Imenikumbusha Gaddafi ndivyo alivyokuwa akisema wakati Libya inaanza kuanguka! Alisema ni vijana wamepewa madawa ya kulevya wafanye fujo na maandamano!
Kanali alikuwa sahihi
 
Mkuki mtamu kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu.

Wewe ulikuwa hujui ulianza hili mwenyewe?

Nakupeleka ignore list. Sitaona utakachoandika.

Maana hujafikia kiwango cha kujadiliana nami.
Sawa...

Ila sijakutukana...wewe umenitusi hata kabla ya mjadala kuiva..
Huko nyuma tushawahi kujadiliana kwa muda mrefu tu ukaishia matusi na dhihaka....

Wazazi wako walipokuwa ni Watumishi pale Ikulu,humu Wala hukuwahi kutukumbusha Kuwa walisimamia POLICE STATE...
 
Wanevunja sheria gani?

Hujajibu swali.
Sheria ya jeshi la polisi ya mwaka 1961 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1995 inaelekeza ni namna gani unaweza kuandamana kwa amani ,uwe na kibali cha polisi ulichotolea taarifa siku 48 kabla ya maandamano yako.

Kinachotaka kufanyika sasa ni kwamba hawana kibali cha polisi shida ipo hapo tu.
 
Maandamano yakipangwa jeshi linatumwa kufanya usafi barabarani. Sasa hata maandamano yenyewe hayajanyika. Next time tuheshimu jeshi letu. Siyo kuwapeleka wanajeshi barabarani kusafisha kisa mkwara wa akina mange kimambi au tundu lisu.
 
Sheria ya jeshi la polisi ya mwaka 1961 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 1995 inaelekeza ni namna gani unaweza kuandamana kwa amani ,uwe na kibali cha polisi ulichotolea taarifa siku 48 kabla ya maandamano yako.

Kinachotaka kufanyika sasa ni kwamba hawana kibali cha polisi shida ipo hapo tu.
Kwa hiyo wamefungwa kwa kosa ambalo walikuwa hawajalifanya bado?
 
Vita ndogo sana,kikubwa serikali hii inachoweza kuwafanyia wapinzani ni kuwaweka jera kwa muda,hawawezi kuwapiga risasi na kuwaua,
Mandela,alifungwa na makaburu,wangeweza kumuua huko gerezani,akatoka akawa raisi wa nchi.
Mijitu Kama Ghadafi,Hussein mubarak,Omar albashir,Mugabe,kamuzu banda,Bagbo,hawakutegemea Kama Kuna siku watatoka Madarakani,yapo wapi?
 
Back
Top Bottom