Kamanda Mambosasa: Mwandishi Erick Kabendera anahojiwa uraia wake

Kamanda Mambosasa: Mwandishi Erick Kabendera anahojiwa uraia wake

Mambo baadae bana.
Anayeikosoa sirikali ndio wakushukiwa uraia wake?
Wanajifanya hawajui kuwa kwenye yard za wadosi na wasomali wamejaa immigrant kibao
Kamanda Mambosasa anasema:

Erick Kabandera alikamatwa nyumbani kwake baada ya kukataa wito halali wa Jeshi la Polisi

Awali aliandikiwa barua ya wito ajili ya mahojiano lakini alikaidi kutii wito halali wa Polisi

Jeshi la Polisi likimwita mtu kwa hiari akikaidi, sisi tunamwezesha atii

Baada ya kukamatwa tumesikia watu mbalimbali wakidai ametekwa. Niseme hajatekwa lakini kwa jeuri akawa amekaidi kutii wito.

Aliitwa kuhusiana na Utata wa Uraia wake. Kwa kushirikiana na Uhamiaji, tunafuatilia uhakika wa uraia wake pale atakapotoa vielelezo mbalimbali kuthibitisha uraia wake. Sasa tunaye, taratibu nyingine za kiupelelezi zinaendelea.

Hajatekwa, amekamatwa na tunaye Central Police.

Upelelezi unaendelea, tukikamilisha upelelezi matokeo ya upelelezi ni kupelekwa mahakamani

Kwakuwa alikaidi wito, hatukuwa na namna zaidi ya kumkamata na kumshikilia

=====

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUKAMATWA KWA ASKARI BANDIA ALIYEVALIA CHEO CHA MKAGUZI MSAIDIZI WA POLISI.

Jeshi la Polisi kanda maalum Dar es Salaam linamshikilia DAUDI RAMADHANI IDDY (23) mkazi wa Tabata Segerea kwa kujifanya ofisa wa Polisi, akiwa amevaa sare za Jeshi la Polisi na cheo cha mkaguzi msaidizi wa Polisi( Assistant Inspector).

Mnamo tarehe 19.07.2019 Jeshi la Polisi lilipata tarifa toka kwa askari wa Jeshi la kujenga taifa (JKT) makao makuu Mlalakuwa, kuwa kuna kijana mmoja amevaa sare za Jeshi la Polisi wana mashaka naye.

Makachero wa Jeshi la Polisi walifika makao makuu ya JKT Kumkamata na kufanya naye mahojiano,mtuhumiwa alikiri kujifanya yeye ni afisa wa Polisi na kufanya utapeli.

Pia alikiri kupitia mafunzo Jkt huko Mafinga mwaka 2006 na kujitolea kwa mujibu wa sheria katika kambi hiyo.

Mtuhumiwa alifanyiwa upekuzi na kupatikana na vifaa vifuatavyo;
1.sare moja ya Polisi aina ya kaki

2. vyeo vya(Cpl, Sgt na cheo cha mkaguzi msaidizi

3 pea moja inaya kombati Jungle green.

4.pingu moja.

5.kofia moja ya askari wa usalama barabarani.

6.radio ya upepo moja aina ya motorola.

7 mikanda miwili ya Jkt.

8.mkanda mmoja wa bendera wa Jeshi la Polisi, buti na viatu vya kawaida.

Upelelezi wa kina unaendelea na mtuhumiwa atapelekwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili.

KUKAMATWA KWA MWANDISHI WA HABARI.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linamshikilia ERICK KABENDERA, (39) mkazi wa Mbweni, Mwandishi wa habari, kwa mahojiano.

Mnamo tarehe 29/07/2019 mtuhumiwa alikamatwa nyumbani kwake na Jeshi la Polisi baada ya kukataa wito wa Jeshi la Polisi.

Aidha mwandishi huyo awali aliandikiwa barua ya wito kufika Polisi kwa ajili ya mahojiano lakini alikaidi wito huo.

Ndugu waandishi wa habari niseme utii wa sheria bila shuruti ni muhimu sana kuzingatiwa kwani ukishindwa kutii sheria inakuwa shuruti. Baada ya kukamatwa mwandishi huyo tumesikia taarifa mbalimbali zikisambaa kuwa mwandishi huyo ametekwa, niseme kuwa mwandishi huyo hajatekwa ila tumemkamata kwa mahojiano. Aidha mtuhumiwa huyo kuna mashaka makubwa kuhusiana na uraia wake tutakapobaini mara moja tutamkabidhi kwenye idaya ya uhamiaji ili kushughulika naye na ndiyo maana alikuwa akikaidi wito wa polisi na kujihami kuwa ametekwa.

LAZARO B. MAMBOSASA – SACP KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.
30.07.2019
 
Wewe mmojawapo wa wasiojulikana?

Tehtehteh...Jamani acheni ku-exaggerate mammbo...Huyo ameitwa polisi kuhojiwa...Ni amri halali ya Jeshi la Polisi...Analisaidia Jeshi la Polisi kwa mambo muhimu...Tuwaache polisi wafanye kazi zao...Bila shaka watamrudisha kwake au kumpeleka mahakamani ...
 
Asubuhi wanakana kuwa na mtu jioni wanakiri kuwa wao ndio wanae!!!
Mungu atuepushe na kikombe hiki laa si hivyo basi mapenzi yake na yatimie...
Huyu bahati yake majirani walitoka mapema na wakapiga picha. Otherwise angepkotwa ufukweni kama kawaida. Sijui utawala huu umeingiliwa na nini
 
Tatizo limeanzia hapa

ohoooooooo....... aisee huyu asipokubali ukimbizi anapotezwa..... KWA NINI ALIANDIKA HIVI HUYU JAMAA??? au anadhani watu hawajui kiingereza???
 
Police siku hizi ndo wanahoji uraia wa watu.
 
IMG_3079.JPG
IMG_3081.JPG
 
Ukifuatilia utakuta hata Mambokale ni raia mwenye asili ya jehanamu sasa na yeye tukitaka kum deport sijui atakubali.
 
Aisee ni kituko baada ya kituko..yaani ni kama naisikia sauti ya yule dada isemayo....Kituo kinachofuata ni Urafiki.
 
Tatizo limeanzia hapa

Kweli kabisa hili ndo chimbuko la tatizo lake
 
Back
Top Bottom