Kamanda Mambosasa: Mwandishi Erick Kabendera anahojiwa uraia wake

Kamanda Mambosasa: Mwandishi Erick Kabendera anahojiwa uraia wake

Full comedy, onamaana ni lazima kwamba matokeo ya upelelezi yakikamilika yainyeshe kuwa si raia?
Kama upelelezi utakuwa huru kwanini wang'anganie kuwa watampeleka mahakamani?
Polisi wetu na viongozi wa siasa, kiujumla, huwa wanaongea kama vile hawajui sheria wala katiba.

Mara nyingine hata kutumia neno "mtuhumiwa" tu (katiba inasema kila mtu anachukuliwa kama hana hatia mpaka mahakama impate na hatia, kiingereza "presumption of innocence") wanashindwa, wanavyo mu address mtuhumiwa ni kama washamuhukumu tayari, mahakamani anaenda kumalizia procedure tu!
 
Kama angekua raia halali angetii wito tu. Ni either raia mkorofi au uraia wake una walakini au sio raia kabisa
 
Movie nyingine inaanza!!!

Msishangae pia waandishi wenyewe wakashindwa kumuhoji maswali ya msingi kama vile ni kwanini wamkamate kama jambazi badala ya kumtaka afike Polisi.
Wewe unene wako unanitia shaka kama huna mtindio. Kasema amepewa wito wa kaeaida akakataa tena karudia zaidi ya mara moja. Soma uelewa.
 
Tanzania banaa, unakamatwa kwanza na kutupwa lupango then ndio uchunguzi unaanza. Tena bahati yako upige kelele wakati unakamatwa ili angalau majiranu wema watoke ndani na kuzipiga picha sura za wakamataji pamoja na namba za gari. Otherwise hutopatikana tena.
 
Yule ni baba yake nasikia. Nimegoogle. Huyo baba alijirusha lake Victoria baada ya kuambiwa sio raia. Alipiga kura uchaguzi 2000.Alishitakiwa akaishia kujiua. View attachment 1167100
Victoire bwana!! Hayo ni majina tu yanafanana. Baba wa huyu kabendera in 2013 huko kwa Bukoba alikamatwa na kuhojiwa kuhusu uraia wake na mwanaye na alielezwa kua sababu ya kuhojiwa ni mwanae. Lakini liliisha nadhani walimrudishia pia passport yake. Nashangaa wameifufua tena!!!!
Kabendera shinani wa BBC ana mtoto wake wa kike anatangaza kwenye TV huko Rwanda.
 
tukianza kupekua makaburi ya uraia unaweza ukashangaa hata magogoni watu wakatafuta pa kujificha
 
Nimejiuliza, mpaka mtu ashukiwe "uraia" kuna vigezo gani vinaangaliwa? Maana wengine tusiojua breki ya mdomo tunaweza kuunganishwa humo kama hakuna misingi ya kueleweka.

Nina shaka sana kama waandishi wa kibongo wameuliza hili.

Ingawa hata wao wamo katika hatari ya kushukiwa "uraia" siku yoyote.

Bora Praise Team akina Mzee Mwanakijiji aka MAGATA wanaishi zao nje.
 
Hii inadhihirisha kuwa watanzania ni vilaza,mtu akiwa anaandika habari za uchunguzi lazima wahoji uraia wake maana watanzania kazi yao ni kuandika habari za mara zari sijui Tanasha sijui Diamond. Hongera Eric wewe ni kipanga si mchezo kuandika nakala kwenye gazeti la The Economist.
Kumbe ni ile makala yake kwenye gazete la economist, hapo lazima tofali na uraia likugonge kichwa.
 
Victoire bwana!! Hayo ni majina tu yanafanana. Baba wa huyu kabendera in 2013 huko kwa Bukoba alikamatwa na kuhojiwa kuhusu uraia wake na mwanaye na alielezwa kua sababu ya kuhojiwa ni mwanae. Lakini liliisha nadhani walimrudishia pia passport yake. Nashangaa wameifufua tena!!!!
Kabendera shinani wa BBC ana mtoto wake wa kike anatangaza kwenye TV huko Rwanda.
Ok Asante.Mimi nikajua labda ni baba wa huyu Eric pia. Maana hata huyo Journalist wa Rwanda nimesoma mahali kuwa walishaishi Tanzania.
 
Nimejiuliza, mpaka mtu ashukiwe "uraia" kuna vigezo gani vinaangaliwa? Maana wengine tusiojua breki ya mdomo tunaweza kuunganishwa humo kama hakuna misingi ya kueleweka.

Nina shaka sana kama waandishi wa kibongo wameuliza hili.

Ingawa hata wao wamo katika hatari ya kushukiwa "uraia" siku yoyote.
Ndio hata mimi huaga najiuliza; hivi wakinikamata kwamba sio raia, nitaonesha nini ili wao wajue kama mimi kweli ni mtanzania pure nisie na hata chembe za impurities!? Au wanapima MKO.jo!?
 
Ni mwendelezo wa kujitia aibu tu kwa jeshi la polisi, uwezi kuamua tu kumuita fulani aje umuhakiki uraia chini ya katiba inayotambua raia wote sawa; kwanini iwe fulani tu?

Hii ni ‘selective justice’ which is injustice ni kitu ambacho mahakama makini inatakiwa kutupilia mbali shitaka kama hilo hakuna zoezi la jeshi la polisi rasmi linaloendelea la kuhakiki wananchi waliozaliwa Tanzania why iwe kwa huyo bwana Bendera. Kama hana mwanasheria mzuri this is selective prosecution from the outset

Isitoshe sio kazi yao kama angekuwa anatakiwa kutoa maelezo ya uraia si angeitwa na uhamiaji polisi inahusu vipi; ata mpakani au maeneo yenye matatizo ya raia wageni mazoezi huwa tunaona yakiendeshwa na maafisa wa uhamiaji polisi wao wanakabidhiwa mtu uhamiaji wanapojiridhisha ameingia kiholela.

Shame on the police force
 
Ndio hata mimi huaga najiuliza; hivi wakinikamata kwamba sio raia, nitaonesha nini ili wao wajue kama mimi kweli ni mtanzania pure nisie na hata chembe za impurities!? Au wanapima MKO.jo!?
Swali muhimu na la msingi sana, ila Mambosasa anaweza kuitisha press conference halafu asiulizwe.
 
Ok Asante.Mimi nikajua labda ni baba wa huyu Eric pia. Maana hata huyo Journalist wa Rwanda nimesoma mahali kuwa walishaishi Tanzania.
Huyo Kabendera shinani wa BBC nae babake alikua mtanzania na alizaliwa na kusoma elimu yake yote Tanzania ila mamake ndo alikua Mnyarwanda. Kwa sasa amebaki binti yake anaitwa Tidjara.
IMG_20190730_162146.jpeg
 
Ni mwendelezo wa kujitia aibu tu kwa jeshi la polisi, uwezi kuamua tu kumuita fulani aje umuhakiki uraia chini ya katiba inayotambua raia wote sawa.

Hii ni ‘selective prosecution’ ni kitu ambacho mahakama makini inatakiwa kutupilia mbali shitaka kama hilo hakuna zoezi la jeshi la polisi rasmi linaloendelea la kuhakiki wananchi waliozaliwa Tanzania why iwe kwa huyo bwana Bendera.

Isitoshr sio kazi yao Kama angekuwa anatakiwa kutoa maelezo ya uraia si angeitwa na uhamiaji polisi inahusu vipi; ata mpakani au maeneo yenye matatizo zoezi huwa tunaona mazoezi kama hayo yakiendeshwa na maafisa wa uhamiaji polisi wao wanapewa tu wakishamalizana nae.

Shame on the police force
Tatizo jeshi la polisi likipelekwa kwa "amri kutoka juu" haya yote linayafumbia macho.

Wewe hushangai wanaohojiwa uraia karibu wote wanasiasa wa upinzani kuanzia kina Kabourou, wafanyabiashara, wandishi wenye kukwaruzana na watawala kina Ulimwengu na huyu tu?
 
Back
Top Bottom