Kamanda Mambosasa: Mwandishi Erick Kabendera anahojiwa uraia wake

Kamanda Mambosasa: Mwandishi Erick Kabendera anahojiwa uraia wake

Kamanda Mambosasa anasema:

Erick Kabandera alikamatwa nyumbani kwake baada ya kukataa wito halali wa Jeshi la Polisi

Awali aliandikiwa barua ya wito ajili ya mahojiano lakini alikaidi kutii wito halali wa Polisi

Jeshi la Polisi likimwita mtu kwa hiari akikaidi, sisi tunamwezesha atii

Baada ya kukamatwa tumesikia watu mbalimbali wakidai ametekwa. Niseme hajatekwa lakini kwa jeuri akawa amekaidi kutii wito.

Aliitwa kuhusiana na Utata wa Uraia wake. Kwa kushirikiana na Uhamiaji, tunafuatilia uhakika wa uraia wake pale atakapotoa vielelezo mbalimbali kuthibitisha uraia wake. Sasa tunaye, taratibu nyingine za kiupelelezi zinaendelea.

Hajatekwa, amekamatwa na tunaye Central Police.

Upelelezi unaendelea, tukikamilisha upelelezi matokeo ya upelelezi ni kupelekwa mahakamani

Kwakuwa alikaidi wito, hatukuwa na namna zaidi ya kumkamata na kumshikilia
Hamna lolote nyie ndio msiojulikana ,Kwanini hamkufuata utaratibu wakati wa kumkamata ?kujitambulisha kwa mwenyekiti wa mtaa ,Kwanini simu zake zote zilifungwa ?Nyinyi ndio msiojulikana hamna hata aibu .
 
Bwana anyoshe mkono wake aje atuokoe, watu wake tunaangamia (zwa)
madhara ya uraia amuulize Jeneral Ulimwengu na Marehemu Cisco Mtiro alitiwa kashikashi kisha akapewa ubalozi ilhali alionekana sio raia hii shida ndo wanadhani kama ndio fimbo yao ya kuwanyanyasia watu.

Hivi akiambiwa mtanzania atoke leo atatoka nani na hasa kwa watu wa mipakani? ukienda tanga wameingiliana sana na watu wa Mombasa, nenda Arusha wameingiliana sana na watu wa nairobi, sikwambii watu wa mikoa ya kigoma, mtwara,mbeya na mingineyo ifike sehemu muwe na akili japo za kuvukia barabara na wala sio za kujitambua na kujitathmini

Ina mana siku hizi hakuna maafisa wa uhamiaji mpaka akaja kushikwa na mapolisi tena ambao hawana hata vitambulisho? Kukaa kwingi ni kuonamengi Bwana Yesu rudi utuokoe watumishi wako tunadhalilika ndani ya ardhi yetu
 
Yani waandiahi wa habari watakua ni vilaza kama wasipoomba kuoneshwa copy ya barua ya wito huo...watakua ni vilaza wa mwaka...
Kuthibitisha mawazo yako ni sahihi ndivyo itakavyokua....na sio hicho hata kuhoji maswali sahihi pia hawatothubutu
 
Yani waandiahi wa habari watakua ni vilaza kama wasipoomba kuoneshwa copy ya barua ya wito huo...watakua ni vilaza wa mwaka...
Inaweza kutengenezwa sasa hivi, swali kwanza kwa maneno yake mambo leo alisema hana taarifa za kukamatwa kwake, na pia anafanya uchunguzi, ghafla yuko polisi kwa mahojiano.
 
yaani hawa jamaa, we ngoja watu wajiandae wakateke mama zao nao watoe sababu kuwa ni majizi mtaani, economist ni waUK sasa tuwasikie na wao watasema nini, ila serikali yetu nayo imezidi sana aisee, mtu kakataa kwenda ndio mnaenda kumkamata kama operation ya Osama kule pakistan
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Majitu yamefungwa sana midomo..watu wamegeuka kuwa na hofu tu..kwakwel mie navyojijua mfano ndo mume wangu anakamatwa kiwehu wehu hvyo...hahaa ntauza gazeti zao..!
Tunahitaji watu hata wachache tu wajitoe woga na akulianzisha kindakindaki ikiwa wameonewa.

Huu utamaduni wa hewala hewala na funika kombe mwanaharamu apite unatuzidishia umasikini.
 
Tunahitaji watu hata wachache tu wajitoe woga na akulianzisha kindakindaki ikiwa wameonewa.

Huu utamaduni wa hewala hewala na funika kombe mwanaharamu apite unatuzidishia umasikini.

Siku zote...wakijitokeza km 2 hiv lazima wengine wataunga tu..mie hawajanipata bado kwenye target yangu..wataniua tu..
 
Thts true..huyu mambosasa huyu!
Yani kwa sasa hii issue ya uraia inavyotumiwa kisiasa, hata siku kama kuna issue ya uraia kweli watu wakifikiri ni siasa zao tu, siwezi kuwalaumu.

Inakuwa kama ile hadithi ya mtoto aliyekuwa analia kwa uongo "mbwa mwitu , mbwa mwitu", watu wakija kumsaidia anacheka akiona kawapata kwa kulia uongo.

Siku mbwa mwitu alivyokuja kweli, akalia "mbwa mwitu , mbwa mwituu", watu wakaona huyu mtoto kazoea michezo yake ya kulialia mbwa mwitu uongo, anataka kutuchezea.

Kumbe mbwa mwitu kamvamia kweli.
 
Kamanda Mambosasa anasema:

Erick Kabandera alikamatwa nyumbani kwake baada ya kukataa wito halali wa Jeshi la Polisi

Awali aliandikiwa barua ya wito ajili ya mahojiano lakini alikaidi kutii wito halali wa Polisi

Jeshi la Polisi likimwita mtu kwa hiari akikaidi, sisi tunamwezesha atii

Baada ya kukamatwa tumesikia watu mbalimbali wakidai ametekwa. Niseme hajatekwa lakini kwa jeuri akawa amekaidi kutii wito.

Aliitwa kuhusiana na Utata wa Uraia wake. Kwa kushirikiana na Uhamiaji, tunafuatilia uhakika wa uraia wake pale atakapotoa vielelezo mbalimbali kuthibitisha uraia wake. Sasa tunaye, taratibu nyingine za kiupelelezi zinaendelea.

Hajatekwa, amekamatwa na tunaye Central Police.

Upelelezi unaendelea, tukikamilisha upelelezi matokeo ya upelelezi ni kupelekwa mahakamani

Kwakuwa alikaidi wito, hatukuwa na namna zaidi ya kumkamata na kumshikilia
Full comedy, onamaana ni lazima kwamba matokeo ya upelelezi yakikamilika yainyeshe kuwa si raia?
Kama upelelezi utakuwa huru kwanini wang'anganie kuwa watampeleka mahakamani?
 
Pascal Mayalla alitoa andiko kubwa kuhusiana na weledi na ukanjanja wa waandishi baada ya kupigana vikumbo kule kwa dada Irene. maeneo haya ya kutumia weledi huwa sikusikii kaka either ukiuliza maswali ya maana au kukosoa weledi wa tasnia... kulikoni?
 
Kamanda Mambosasa anasema:

Erick Kabandera alikamatwa nyumbani kwake baada ya kukataa wito halali wa Jeshi la Polisi

Awali aliandikiwa barua ya wito ajili ya mahojiano lakini alikaidi kutii wito halali wa Polisi

Jeshi la Polisi likimwita mtu kwa hiari akikaidi, sisi tunamwezesha atii

Baada ya kukamatwa tumesikia watu mbalimbali wakidai ametekwa. Niseme hajatekwa lakini kwa jeuri akawa amekaidi kutii wito.

Aliitwa kuhusiana na Utata wa Uraia wake. Kwa kushirikiana na Uhamiaji, tunafuatilia uhakika wa uraia wake pale atakapotoa vielelezo mbalimbali kuthibitisha uraia wake. Sasa tunaye, taratibu nyingine za kiupelelezi zinaendelea.

Hajatekwa, amekamatwa na tunaye Central Police.

Upelelezi unaendelea, tukikamilisha upelelezi matokeo ya upelelezi ni kupelekwa mahakamani

Kwakuwa alikaidi wito, hatukuwa na namna zaidi ya kumkamata na kumshikilia

Min nadhani jambo moja ambalo polisi hawatutendei haki watanzania ni hii staili ya ukamataji. kwa sababu wanajua fika siku hizi matuykio ya utekaji raia na hili kundi la watu wasio julikana umekuwa kwa kiwango kikubwa sana kiasi kwamba naweza nikafananisha na donda dungu la boko haram kule Nigeria lakin cha ajabu kabisa wakiwa wanalijua hilo bado na wao wanaenda bila kufuata mfumo ambao utawaondolea shaka raia ili kujilidhisha kwamba waliokwenda kumkamata huyo mtu na raia yeyote yule ilitakiwa watu wajilidhishe pasipo shaka kwamba hawa kweli ni polisi. lakini sasa unaona kwa mujibu wa maelezo haya hivi ni nani pale angeweza kutofautisha kama hawa ni polisi au WATU WASIOJULIKANA? tutaishia maisha haya ya hofu na mashaka mpaka enzi zipi zije jamani. mbona ni jambo dogo sana. hebu fikilia watu wanakuja na private car. istoshe unakuta baadhi yao wamevaa kininja, hivi kweli utakuwa ni malaika kuweza kujua hawa ni polsi. Hatupingi mtu kukamatwa kabisa kwanza sisi watanzania tupo mstari wa mbele kufanya kazi na polisi lakini huu uninja mwisho wake lini au mpaka nini kitokee ndo wajifunze kwani kumkamata mtu kama huyo hata wangeenda askari wa kawaida kabisa asingeweza kukataa. Hata kama unasema umemiuta halafu kagoma sasa unapokuja style ya kimafia inaleta picha gani kwenye jamii. Maana hata kama ungeenda na sare na kitambulisho ukaenda ukamchukua mjumbe mkaingia pale angewezaje kukataa? hii ni nchi yetu sote na katiba ndo msingi wake. Hii hali ya leo kila siku utekaji unaweza kumwamini mtu yeyote kweli?

Kmanda...Chukua askari wako wa kawaida tena wawili tu bila silaha wakifika pale wanamwambia twende kwa utaratibu akakataa sasa kuanzia hapo unaweza kuomba reinforcement ambayo hata ikija tayari unakuwa umeondoa tension kwa raia.
Hata wangeenda askari wa tigo tu wangemchukua hakika hakuna mwenye ubavu wa kushindana na dola hayupo hata kama angekuwa vipi.

Kwa mwendo huu hawa watekaji wasiojulikana watakuwa bado wana nafasi kubwa sana ya kutamba kwa saabu polisi wanacheza ngoma yao na wao wanachukua hiyo nafasi kujificha humo humo. Watu wa kawaida wanabaki kwenye dilema ni polisi au watekaji? Tayari mtu alishakwenda mtamkuta kesha tupwa maiti au apotee moja kwa zote.
 
Mwisho wa season watatujulisha,watz.siyo wajinga kiasi hiki is beyond too much now.
 
Ni vyema polisi wangekuwa wanavaa sare zao na kutumia magari yao yanayojulikana wanapoenda kukamata watu kama hivi,vitambulisho pekee havitoshi kwanza ID og ya kughushi raia hawezi kuitambua.
 
Maswali anayopaswa kujibu Mambo sasa:
1. Jana alipohojiwa alikana kufahamu kuhusu "Kukamatwa" kwa Erick alisema hafahamu chochote, imekuwaje leo anafahamu kisa kizima?
2. Utaratibu wa kukamata Watuhumiwa nchini Tanzania umebadilika? Askari walipaswa kujitambulisha, walipaswa kuwa na Hati ya Kumkamata, walipaswa kwenda na msimamizi wa Amani wa eneo hilo, haya yote yalifanywa? Kwa mujibu wa mashuhuda, haya hayakufanyika, na mawasiliano yote yalifungwa, WHY?
3. Suala la uraia la Kabendera liliwahi kushughulikiwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi mwaka 2013, na alikuwa cleared na kurudishiwa uraia na Passport yake, what is so special now?
4. Iko wapi barua ya wito anayosema ilitumwa kwa Kabendera? Ki wapi kiapo cha mpeleka wito aliyepeleka wito kinachoonesha kuwa Kabendera alikataa kupokea wito?
 
Back
Top Bottom