Kamanda Mambosasa: Mwandishi Erick Kabendera anahojiwa uraia wake

Kamanda Mambosasa: Mwandishi Erick Kabendera anahojiwa uraia wake


Asubuhi wanakana kuwa na mtu jioni wanakiri kuwa wao ndio wanae!!!
Mungu atuepushe na kikombe hiki laa si hivyo basi mapenzi yake na yatimie...


Mie nilivyo na chuki nao..ningeenda na petrol kituon..yaan unaamua kufa tu..shebzy zao
 
Kamanda Mambosasa anasema:

Erick Kabandera alikamatwa nyumbani kwake baada ya kukataa wito halali wa Jeshi la Polisi

Awali aliandikiwa barua ya wito ajili ya mahojiano lakini alikaidi kutii wito halali wa Polisi

Jeshi la Polisi likimwita mtu kwa hiari akikaidi, sisi tunamwezesha atii

Baada ya kukamatwa tumesikia watu mbalimbali wakidai ametekwa. Niseme hajatekwa lakini kwa jeuri akawa amekaidi kutii wito.

Aliitwa kuhusiana na Utata wa Uraia wake. Kwa kushirikiana na Uhamiaji, tunafuatilia uhakika wa uraia wake pale atakapotoa vielelezo mbalimbali kuthibitisha uraia wake. Sasa tunaye, taratibu nyingine za kiupelelezi zinaendelea.

Hajatekwa, amekamatwa na tunaye Central Police.

Upelelezi unaendelea, tukikamilisha upelelezi matokeo ya upelelezi ni kupelekwa mahakamani

Kwakuwa alikaidi wito, hatukuwa na namna zaidi ya kumkamata na kumshikilia
Hivi hawa wajinga hafahamu kuwa watanzania wengi tuna elimu na tuna iq kuwazidi wao
 
Uraia pacha,utamaliza haya mambo ya kuhojiana uraia.
Nchi hii hata ukiwa na uraia pacha hata kama uliwahi kuwa ngazi ya juu siku ukisigana nao UTAHOJIWA URAIA TU!!!
Wakaazi wa Ujiji ambapo watu na mababu wa babu zao walizaliwa na kuzikwa hapo WANALIJUA VEMA HILO MAANA WALIPELEKWA KONGO WASIKOKUJUA WALA KUTAMBULIKA KWA NGUVU... KISA KUCHAGUA KISICHO CHAMA CHAO!!!
MWISHO WA SIKU WALIREJESHWA KIMYAKIMYA!!!
TUNAJENGA NCHI TUKIIMARISHA UPENDO NA AMANI!
 
‘....ukikataa kutii wito halali wa Polisi tunakuja kwako kukusaidia kutii wito...’

Hatare sana Wallah
 
NI fimbo ya hovyo sana hiyo, Chiluba alijaribu kuitumia hadi kwa raisi mstaafu wa nchi hiyo Mzee Kaunda kwa kumuita eti ni Mmalawi, lakini kilichomtokea yeye mwenyewe Chiluba baada ya kutoka madarakani ni somo kwa viongozi wote wa Afrika
Saa zingine mtu unawaza "...sijui naishi nchi ya kipumbavu... au tungali athari za mashenzini!?"
 
Hii tabia ya watu wanaokosoa serikali mnatumia Fimbo ya Uraia au Kuhujumu uchumi hizi ni Tabia za kishamba tukianza kutafuta uaria wa kila mmoja hii nchi itajikuta amna Raia
 
Kwa hiyo zile makala za Economist huyu jamaa ndio alikuwa muandishi 😂...
Bila shaka Acacia ndio wamemchoma baada ya kumalizana na Barrick, kwa yale maneno ya dharau na kebehi acha na yeye apate haki yake kidogo.
 
kwa Akwilina alisema "Kati ya risasi zilizopigwa juu moja ilimpata" wakati Akwilina alikuwa kwenye hiace wala haiko kwenye flyover. mwenyewe nasubiri jibu la swali lako
Elimu isihusishwe katika hili maana wengine walielimika mpaka ngazi ya juu kabisa wakanadi wametoka jalalani!!! Ila kuna uwezekano "ubongo na kichwa" vilishajitenga...
 
Hii tabia ya watu wanaokosoa serikali mnatumia Fimbo ya Uraia au Kuhujumu uchumi hizi ni Tabia za kishamba tukianza kutafuta uaria wa kila mmoja hii nchi itajikuta amna Raia

Hata Rais ukute atakuwa sio mtz😏..mie nisingejibu kitu..ningekaa kimya mwanzo mwisho
 
Back
Top Bottom