Nakumbuka siku moja nilimtembelea ofisini kwake pale Moshi, kiukweli jicho lilizama kwa lineup ya polisi wa kike, nikamtania imetokea tuu au amechagua? .
Akanitania naijua shida yako kwa sababu naujua ugonjwa wa Wasukuma!. Akasema CCP iko Moshi, hapa ndipo jikoni penyewe, naingia mwenyewe jikoni kuchagua! .
Kamanda Chicco alikuwa rafiki wa waandishi wa habari, rafiki wa wote, always smilling. He was simply a man of the people nna sisi Wakristu tunaamini mtu anaokolewa kwa neema na sio kwa matendo.
Inna li Llahi wa Inna Ilayhi Rajiun.
RIP Kamanda Mohammed Chicco
Paskali