Kamati: Kinyesi na Mikojo ya Mifugo ndiyo chanzo cha kufa samaki mto Mara, sio sumu ya maji ya Migodini

Ukisikia ungese basi ndio huu. Kinyesi na mkojo vimekuwepo toka enzi na enzi na samaki hawajawahi kufa ndo waje wafe leo?
Ujinga na upumbavu wa wasomi wetu ndivyo vitatumaliza. Wale wote waliokuwa kwenye kamati ya uchunguzi wanastahili kuchomwa moto.
 
Wengine wanabisha tu
Profesa kafanya utafiti
Ila hapo kwenye kilo 25 kwa siku hata mimi naweza kubisha

 
Ndoo ya lita 20 ongezea lita tano..ndio kinyesi cha ng'ombe..nahisi walikosea kusema hapo walimaanisha kifaru ama tembo.

Daah..tushauzwa tayari sana.

Lakini kwa mswahili wala sishangai
Labda wamepima utumbo mzima machinjioni hapo ningekubali
 
Woi woi

Kwahiyo Ngombe anatoa sumu ya kuua samaki??

Only in Mara.

Hawa jamaa itakua wamejificha mahali wamegoogle na kuja na ripoti.
 
Wewe mbwa mwitu unae bisha tu kwa siku kama unakunywa maji inavyotakiwa,unatakiwa ukojoe liya 2 kwenda 3 na kimba lako kama unashiba siyo chini ya kilo moja,angalia mwili wa ng'ombe na anavyokunywa maji
 
Washapewa pesa hao wanaleta siasa kweli mkojo na kinyesi ??!! Mbona wafiga samaki wanatumia hivo vitu na samaki hawafi
 
Enzi za marehemu ripoti kama hii ilikuwa inaondoka na profesa wa michongo.
 
Tuambie Sasa ukweli unaoufahamu kuhusu chanzo cha vifo vya samaki na maji kubadilika rangi.
 
Hii ni ripoti au ni utopolo!! Yaani wanataka kutuambia hao ng'ombe muda wote walikuwa wako mtoni wanakunya hizo kg 25??! Mimi ni mfugaji nijuavyo ng'ombe anakunya zaidi usiku akiwa amepumzika pia kinyesi chake akiwezi kuwa sumu ya kuua samaki pia mto mara unatiririsha maji muda wote hivyo si rahisi kinyesi kikakaa sehemu moja kwa miezi 8 kama ripoti inavyotaja. Ni aibu kubwa kwa Prof. kutoa ripoti yenye walakini kiasi hiki hata hao wafugaji na wakulima wa maeneo wangefanya utafiti wao wangeleta taarifa ya maana kuliko hii.
 
mmm kwa hiyo kesi inaenda kwenye wizara ya maliasili na mazingira maana ndio jukumu lao.
 
Ha ha ha ha Watanzania TUMELAANIWA RASMI!

Hawa Wasomi hawa!...kuna siku mtu unaweza kujilipua tu!

Yani kinyesi na Mkojo wa ng'ombe ndio uue samaki upande huo wa mto Mara na upande mwingine samaki wanaendelea kula bata tu kama kawaida?

Hivi wawekezaji wanaweza wakatupa kiasi gani cha fedha kuficha ukweli na kutunga uongo wa kiwango hiki cha mtoto wa darasa la awali?

Shenzi kabisa!
 
Kishimba hoyee profesa mayele huyu huyu wa yanga au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…