Kamati: Kinyesi na Mikojo ya Mifugo ndiyo chanzo cha kufa samaki mto Mara, sio sumu ya maji ya Migodini

Hebu acheni usanii basi, mnataka kutuambia kuwa Hao ngo'mbe wakitaka kunya na kukojoa wa naenda mtoni? Hicho kinyesi hakiozi? Maprofesa wa Tanzania njaa zinawamaliza
 
Pale Dakawa njia kuu ya Moro Dom kuna ka bwawa miaka na miaka sasa,...wamasai wananywesha ng'ombe, wanakunya humour na kukojoa na zaidi watu wanafanya shughuli zao humour kama kuoga na kufua na maji hayo yametwama.

Sijawahi sikia Kambale pale wamekufa
 
Hizo data wamezichukua hapa: Cow In and Out
ila cha ajabu, je hao ng'ombe walikuwa wanashinda humo mtoni, kulala humo humo? na Je mto ulikuwa umetuama? Hawa Mapro- pesa ndio maana wanadhalauliwa na darasa la saba kama Msukuma na Kibajaji...
Yaani walipiga desa "kopiraiti"
 
hii Nchi ngumu sana walahi !

hapo watu wamepiga pesa k'ulaini kabisaπŸ€”

dah hii Tanzania ukifa masikini ni uzembe wako πŸ™Œ
 
"Ng'ombe mmoja ana toa kilo 25 za kinyesi kwa siku moja na mkojo lita 21
duu hao ng'ombe ni wa aina gani? na je wanashinda ndani ya mtoo 24hrs kiasi cha kwamba huwalazimu kila wakitaka kujisaidi wajisaidie ndani ya maji au kila wakiona maji choo huwabana. prof anataka tuanze kukagua vyeti vyake? ndiyo maana mbunge Msukuma anawazihakigi hawa wasomi.
 
 
Musoma. Kamati maalum ya kitaifa iliyoundwa na serikali kuchunguza mabadiliko ya maji ndani ya mto Mara, imetoa taarifa ya chanzo cha mabadiliko katika mto huo yaliyosababisha maji kuwa meusi na kutoa harufu...
Tuanze na KG 25 zakinyesi hao ni ng'ombe au Tembo?Tuangalie na tulinde maisha ya watu wetu bila mizahaa
 
Maprofessa wapumbavu Kama Hawa Ndo wanaishushia hadhi elimu yetu
Professorior rubbish in Lisu voice hata wale wa makinikia walituambia tunadai Mihela kibao tukaishia kudanganywa.
 
Jamaa mwenyewe alikuwa anaongea kwa aibu.
Hata yeye haamini kitu alikuwa anasoma.
 
Shangaa
 
Nitashangaa maximo kufuta ukweli kuhusu kila jambo na matokeo.

sisi ndio wachangiaji ila itafika mtakosa watu kuficha ukweli labda kuogopa au kuweka tanzania kuwa kweli.

mtaki kuwa sema kweli kutokana na watu wachache au kuwa nyie bora kuogopa watu fulani.

ziwa linategemea kinyesi na sio madawa na hii kama mkipinga napeleka sehemu maalumu mtakuja kujuta
 
Tumefuga ng'ombe ... Sijawahi ona ng'ombe anajisaidia kinyesi kilo 20-25 kwa siku. Hamna waache kutuona sisi wapuuzi

Halafu mkojo lita 21? Kweli? Kwa nini wanafikiria sisi ni wajinga kiasi hiki?

So ikitokea ng'ombe hajanya au kukojoa kwa siku anakuwa na ongezeko la kilo zipatazo 30-40? Inawezekana kweli?

Jamani msitutukane kiasi hiki. Mtuheshimu kidogo. Huyo ng'ombe wa kutoa kinyesi cha kg 25 kwa siku. Hivi wale ambao tumefuga ng'ombe wa maziwa lets say 10. Kwa siku wana produce kinyesi kilo 250? Kwa siku 10 ni Tani 2.5? Kwa mwezi tani 7.5 ? Kwa mwaka ni zaidi ya Tani 87 ya kinyesi kwa ng'ombe 10. Kweli?

Profesa pleaaseeee....nakuomba propesa usitufanyie hivyo. Nasi tumeenda enda shule kidogo.
 
Taarifa labda imewagusa moderator...πŸ˜‚

Mi mwenyewe nilishawahi tenda dhambi mpaka shetani akasema "WOW IT'S AMAIZING!"..πŸ˜…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…