29 November 2023
SABABU ZA KADHAA CCM KUTEUA WAGOMBEA NGAZI ZA WENYEVITI WA MIKOA NA WILAYA
CCM Wilaya ya Kusini Unguja itafanya uchaguzi baada ya kufariki ndugu Mgana Zidi Khamis aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.
Kutoka wilaya ya Mpanda habari ni kuwa CCM inategemea kumpata mwenyekiti mpya
Mwenyekiti CCM Wilaya ya Mpanda marehemu Method Mtepa enzi za uhai wake. Picha na Mtandao
Huku CCM wilaya ya Mpanda
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Ccm wilaya ya Mpanda Bw. Method Mtepa alifariki dunia tarehe 19/09/2023 baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Picha: Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza ndugu Sixbert Jichagu (katikati) akiwa na mkuu wa mkoa CPA Amos Makala (kushoto), wakati mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza,alipofika ofisi za CCM kujitambulisha.
Na kwa uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, unakuja baada ya mwenyekiti wa mkoa wa Mwanza ndugu Sixbert Jichagu kuteuliwa kuwa DED mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi. Ndugu Sixbert Jichagu alichaguliwa kwa kishindo kikubwa mwezi September 2022 lakini mwenyekiti wa taifa akampangia kituo cha kazi mwaka 2023 kuwa DED halmashauri ya Masasi.
View attachment 2829053
Picha: mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya ndugu Dr. Stephen Mwakajumilo.
Wakati kwa mkoa wa Mbeya, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya ndugu Dr. Stephen Mwakajumilo aliye mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC alileta mtafaruku kwa kuhoji sababu za miradi mingi kusimama baada ya Magufuli kufariki.
Pia mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Mbeya ndugu Dr. Stephen Mwakajumilo alisema kunahitajika mjadala mpana kuhusu mkataba wa bandari na kuungana mkono wananchi walioomba kupatiwa sababu za, uhalali wa bandari kupewa DP World kwa mkataba ulioolekana kuwa na utata. Msimamo wa ndugu Dr. Stephen Mwakajumilo ukaistua CCM na hata makamu wa rais akasema kuwa wanaCCM hawana utamaduni wa kuhoji waziwazi bila kupitia vikao vya ndani vya CCM kama alivyofanya ndugu Dr. Stephen Mwakajumilo mbele ya vyombo vya habari.
Na mwisho CCM mkoa wa Arusha walimpoteza mwenyekiti wao wa mkoa, Kamishna Mstaafu Zelothe Stephen ambaye alifariki dunia hivi karibuni mwaka 2023.