Kamati Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti Samia yaridhia Daniel Chongolo kujiuzulu Ukatibu Mkuu

Kamati Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti Samia yaridhia Daniel Chongolo kujiuzulu Ukatibu Mkuu

Jamaa kishaandika barua ya kujiuzulu na imeletwa kwenu na imepokelewa , mmemkubalia, sasa mnachunguza kitu gani tena?

Hakuna haja ya kupoteza muda kuchunguza yanayojulikana, hivi Kinana akijiuzulu kesho kutwa ( kama tunavyotarajia ) naye atachunguzwa?

Acheni kutupotezea muda, jazeni nafasi zilizoachwa wazi
Msiingilie mambo ya ndani ya Chama tawala.

Nyie huko kwenu msichunguze mtu akiwachia ngazi.
 
Daniel Chongolo - Ni Hatari Kuwa Kiongozi Wa Mtu, Badala Ya Kuwa Kiongozi wa Chama au Jumuiya


View: https://m.youtube.com/watch?v=N6D3fArqs_Y

Katibu mkuu Daniel Chongolo aliyasema hayo akizungumza hivi karibuni na viongozi vijana wa jumuiya ya chama yaani UVCCM waliojazana ukumbini hivi karibuni kupata nasaha za namna ya kuwa kiongozi mzuri wa chama au jumuiya za chama .... na kusisitiza ukijidanganya ukawa kiongozi mfuasi wa mtu, siku akiondoka yule mtu unayemtegemea utakwenda na maji anasisitiza katibu mkuu wa CCM ndugu Daniel Chongolo.... hivyo viongozi kitumikieni chama maana chama hakiondoki na kama utakuwa mzuri katika kukitumikia chama basi utadumu katika uongozi na kukua .....
 
Makala / Uzi kwa hisani kubwa ya mwanaJF Mindi iliyoandikwa mwaka 2018 :

Orodha kamili ya makatibu wakuu wa CCM tokea ilipoanzishwa mwaka 1977​

Kwanza nianze kwa kutoa orodha kamili ya makatibu wakuu wa CCM tokea ilipoanzishwa mwaka 1977 baada ya kuungana na ASP:

kw.png

Ukiacha Pius Msekwa na Rashid Kawawa, Mwenyezi Mungu amweke mahali pema, hao wanaofuatia hakuna aliyeondoka vizuri katika nafasi yake. Horace Kolimba nadhani hapo hakuna mjadala, maana ile kauli yake kali aliyoitoa kwamba CCM HAINA DIRA, ndiyo ilianzisha kile kinachoitwa KUKOLIMBWA. Jamaa Walimkolimba. Mungu amweke mahali pema. Lawrence Gama, Mwenyezi Mungu amweke mahali pema, nakumbuka kulikuwa na figisufigisu wakati wa uchaguzi mkuu wa 1995, alikwaruzana sana na JK, ambaye alikuwa anaongoza kwenye kura za ndani ya CCM mpaka pale Nyerere alipoingilia kati.
Inaaminika Philip Mangula alikuwa moja ya makatibu wakuu bora na imara wa CCM. hakuwa na maneno mengi hadharani lakini alikuwa mtendaji mzuri sana ndani ya CCM, na aliijua vema. lakini alitupwa nje na Kikwete, tena kwa kejeli na manyanyaso. pamoja na kuwa mtendaji bora, hakwenda sawa na mfumo wa JK. JK akaona zee la mjini Makamba ndiyo chaguo sahihi.

Kwa maoni yangu, Makamba alikuwa Katibu Mkuu mbovu kuliko wote waliowahi kushika cheo hicho. alilea mfumo wa rushwa katika CCM, na malalamiko ya ubaguzi na utendaji mbovu yalishamiri enzi zake. JK alijaribu kukiokoa chama kwa kuja na sera ya KUVUA GAMBA, ambayo ilikuwa matokeo ya utafiti uliofanywa na tume ya Wilson Mukama. Huyu alipewa kazi ya ukatibu mkuu ili atekeleze sera aliyoifanyia utafiti. lakini hakuwa na nguvu za kisiasa ndani ya CCM, na hapakuwa na utayari wa kisiasa kumuunga mkono kati ya vigogo wa CCM. akakwamba na CCM ikazidi kuyoyoma. Akiwa desperate, JK ndipo alipomleta Abdulrahman Kinana.

Kinana anatajwa kama Katibu mkuu bora kabisa katika orodha ya makatibu wakuu wa CCM. anajumlisha uzoefu katika uongozi wa serikali na chama, kukielewa chama, kiwango cha juu cha upevu na hekima. ukiacha tuhuma mbalimbali kuhusu nyara za serikali, ni mtu anayekubalika na wengi katika ngazi mbalimbali za chama. ni Kinana ambaye ameshindwa kwenda na kile kinachoitwa "kasi" ya Rais Magufuli. ilionekana wazi kwamba Kinana haivi na JPM. mitizamo na staili ya Kinana ni tofauti kabisa na ya JPM. Kinana amenukuliwa akisema wazi kwamba kiongozi hawezi kuhodhi ukweli, kwamba ni lazima awe tayari kusikiliza maoni tofauti. inajulikana kwamba JPM anahitaji kusifiwa daima, yeye hakosei, neno lake ni amri.

Sasa Bashiru Ally anaingia kwa mfano wa nani hapo? Bashiru kaingia kwa staili ya Wilson Mukama. wote walipewa kazi ya kuongoza "kamati maalum" na kutoa ripoti, ambayo ilipelekea wao kukabidhiwa kazi ya kutekeleza hayo waliyogundua. lakini tofauti ni kwamba Bashiru hakupata nafasi ya kuwashughulikia waliohodhi mali za chama. Bashiru pia siyo mtu wa ndani katika CCM, japo anadai kwamba amekuwa ndani ya CCM kwa miaka kadhaa.

Kwa kipindi cha mwanzo, Bashiru alionekana kufuata amri za Mwenyekeiti wake na kuzitekeleza, hata pale ambapo zilikuwa kinyume na katiba ya CCM. Bashiru ametetea utaratibu wa kuwaruhusu wanaoguswa na utendaji wa JPM na kujiuzulu ubunge au udiwani, kugombea tena nafasi hizo ndani ya CCM bila kupitia mchakato wa kura za maoni. Bashiru pia amekubali na kubariki wizi na uporaji katika sanduku la Kura, ili kuhakikisha kwamba CCM inashinda viti vyote katika chaguzi ndogo. mwenyewe amejenga hoja kwamba hii ni dalili ya kukubalika kwa chama!

Lakini inaonekana hata yeye haamini hayo, kwa kauli zake za hivi karibuni. anaonekana kujiondoa taratibu kwenye "uJPM" na "uMakonda", kwa kuwa na msimamo unaoendana na hali halisi zaidi, msimamo unaoakisi maoni ya watanzania walio wengi. si wengi wanaoingizwa mjini na kauli za "kuguswa na utendaji wa JPM", kiasi cha kuliingiza taifa katika gharama za uchaguzi ambazo wala hazina sababu, na wala hazina mantiki hata kwa akili ya kawaida tu. eti "DEMOKRASIA NI GHARAMA!!!" EBO!

Sasa swali linakuja, kama Bashiru anaanza kuwa na mawazo ya ki-Kinana Kinana hivi, mwisho wake ni upi? atajiuzulu au atangojea kutumbuliwa? au ndio ameamua kutumia nafasi hii "kuibadilisha CCM" jambo ambalo siyo rahisi hivyo, lakini pia inawezekana. hasa kama atakuwa mjanja wa kutafuta uungwaji mkono na watu muhimu ndani ya chama. inajulikana kwamba wengi katika CCM hawafurahishwi na mambo yanavyokwenda. lakini hii inahitaji tahadhari kubwa. kwa kuonesha mwelekeo mapema hivi, ataweza kweli kufaulu kugeuza mwelekeo wa manowari hii kubwa? Tujadili

Source : Orodha kamili ya makatibu wakuu wa CCM tokea ilipoanzishwa mwaka 1977
 
Ccm wamepoteza hamasa ya siasa hapa nchini, matokea yake wamebaki kubahatisha kuwa wananchi wanataka nini, ndio maana wanalazimisha matukio ili watrend. Kwa bahati mbaya wanashindwa kuamini na kukubali kuwa hiki sio kizazi Cha ccm, na hakitakaa kipate tena mvuto zaidi ya kutumia shuruti kubaki madarakani.
Kwasasa chama gani kina mvuto hapa Tanzania?
 
ataweza kweli kufaulu kugeuza mwelekeo wa manowari hii kubwa? Tujadili

Nimeangalia jedwali la makatibu wakuu wa CCM , kwa jinsi mambo yalivyo sasa ni wakati wa katibu mkuu wa CCM atoke Zanzibar.

Maana toka chama dola kongwe kianzishwe mwaka 1977 jedwali linaonesha hakuna mzanzibari aliyepata kushika nafasi hiyo.


Sasa ndugu Daniel Chongolo amejizulu, je ni nafasi historia kuandikwa ?


View: https://m.youtube.com/watch?v=NFgO2UBWVEI
 
ile ni connection kaa connections zingine acha akangalie nayeye ile ya chongolo
 
Sikuogopa 22 November 2022

MZEE MANGULA: NILIJUA MAPEMA/ SIKUMUOGOPA / NILIRUDI SHAMBA KULIMA

View: https://m.youtube.com/watch?v=oYGno3IV2Ls

Ni kazi ngumu kudeal na watu ndani ya CCM wanaotaka uongozi, ningetoka hapa nimejeruhiwa ... 1995 kuifanya CCM iweze kuwa kama taasisi moja na kurejesha maamuzi kwa wanachama badala ya kuhodhi na viongozi wachache ...
 
Jamaa kishaandika barua ya kujiuzulu na imeletwa kwenu na imepokelewa , mmemkubalia, sasa mnachunguza kitu gani tena?

Hakuna haja ya kupoteza muda kuchunguza yanayojulikana, hivi Kinana akijiuzulu kesho kutwa ( kama tunavyotarajia ) naye atachunguzwa?

Acheni kutupotezea muda, jazeni nafasi zilizoachwa wazi
Sawa CHADOMO
 
Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kilichofanyika leo tarehe 29 Novemba, 2023 Jijini Dar es salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kimeridhia kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Comrade Daniel Chongolo

Taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda imeeleza walioteuliwa kugombea nafasi ya Uenyekiti kwa mikoa ya Arusha, Mbeya na Mwanza pamoja na Wilaya za Mpanda na Kusini Unguja.


---
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameijulisha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kupokea barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, na ameridhia ombi hilo.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda amesema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa kuhusu Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichoketi leo Jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kimejadili hali ya kisiasa ndani ya Chama na nje ya Chama hicho nchini na kimefanya uteuzi wa mwisho wa Wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya Chama kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo na uteuzi wa nafasi nyingine.

Pia soma:
- Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo aandika barua ya kujiuzulu

View attachment 2828888View attachment 2828889
Sabaya ndiye anafaa na akiungana na Makonda watamtengeneza Magufuli mpya.
 
Back
Top Bottom